cacashian01
Member
- Mar 3, 2016
- 76
- 62
Habari wanajamvi.
Naomba msaada wa kufahamisHwa kisheria, nina Ndugu yangu alikua anafanya kazi kwenye mgahawa alikua anaaminika na Bosi wake pamoja na wafanyakazi wenzake,kwa pamoja wakaamua kuanzisha mchezo wakupeana Hela(upatu)ambapo yeye (Ndugu yangu) ndio aliyependekezwa na wenzake pamoja na bosi wake awe anaweka hela,
Waliendelea na mchezo na akawa anawakabidhi hela wale wanaopokea wakabaki watatu yani Bosi wake na wafanyakazi wengine wawili,na wakati huo mchezo ukiwa unaendelea Bosi akikwama anawaambia waazime hela kwa Ndugu yangu, na ndugu yangu alikua anaandika kila anachomkopesha bosi.
Sasa biashara ikawa sio nzuri Bosi akawasimamisha huku mchezo (upatu haujaisha) kwahiyo kwenye mahesabu Bosi anasema anadai Mil.1 wakati ndugu yangu kwenye hela alizo msainisha Bosi anatakiwa alipwe Laki 5 tu, na wingine wawili wanadai jumla ya laki . Sasa Bosi anamlazimisha Ndugu yangu alipe wakati wanaotakiwa kulipa kazi wamesimamishwa na yeye ndugu Yangu hadaiwi kwenye huo mchezo. Bosi anasema atampeleka polisi.
Msaada wenu afanyaje?