Naomba ushauri kwenye hii ya Upakaji rangi Magari

adidas power

Member
Mar 13, 2020
33
37
Ndugu wana JF,

Katika harakati zangu za utafutaji nimepata kama 7 million, nikafikiria biashara ya kifanya nikapata wazo la biashara ya UPAKAJI RANGI MAGARI.

Naomba kupata gharama wa hii biashara na vipi waliowahi au wanaoifanya inalipa?
 
Suala la uuzaji wa rangi pia ni zuri nalichukua mkuu, ila kuna vijana wapo wenye ujuzi wa upakaji rangi tutasaidiana nao mimi nitakuwa msimamizi
Kwa biashara hiyo sidhani kama watakubali wafanye kazi halafu wewe uje tu uchukue cha juu. Na vipi siku wakiamua kuondoka? Labda ufanye mchakato tu ujifunze na wewe.
 
Katika kazi/biashara yoyote unayofanya/unayotaka kuifanya hakikisha unaifahamu vizuri na pia unaipenda hio kazi. Faida(hela) ni nyongeza baada ya kuwa unafanya kitu unachokipenda na kukifahamu kiundani.
 
Kufanya unachokipenda ni mlengwa wa umasikini.

Penda unachokifanya mlengwa utajiri.
 
Usiweke malengo yako juu ya malengo ya watu wengine,siku malengo yao yakisambaratika na wewe ya kwako yatasambaratika.
 
Back
Top Bottom