Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
-
- #101
umenisaidia sana kupanga......basi kama hvyo mpangie kazi zake awe anazifanya na kupata muda wa kupumzka na kujisomea. Labda, usafi wa baadhi ya sehemu za ndan, either sebulen na koridoni, then hadi vyombo vya jioni au kupika mboga jioni au viwe vina-rotate kupka na vyombo.
Haitamchosha mwanafunzi na pia dada ataona anasaudiwa
ha haaa, rafiki kesho nikienda job wanangu watakaa na nani home?Huyo ulitakiwa umfukuze toka asubuhi..
Huyu kama ukaanza ujeuri usikute hata Watoto anawatesa usipokuwepo so bora ufukuze kwanzaha haaa, rafiki kesho nikienda job wanangu watakaa na nani home?
natafuta mwingine ndo nifukuze huyu
h haaaa, sawa rafiki. hilo la kuondoka halina mjadalaHuyu kama ukaanza ujeuri usikute hata Watoto anawatesa usipokuwepo so bora ufukuze kwanza
unajua nashindwaga kuelewa kwa nini kuna wamama wanakuwa na urafiki na wadada wa kazi wa nyumba za jirani na wakati maboss wao hawajawazoea
huyo mzuri......Wanafanya hvyo sababu hawana kazi za kufanya,kwa mama aliye bize hawez kufanya upumbavu huo.
Mie nina majirani vimeo acha tu,nashukuru Mungu amenipa moyo wa pekee,nashukuru Mungu mdada wa sasa ana msimamo chochote wanachochokonoa lazima aniambie na hatoi ushirikiano kwao.
hiyo imekaa vizuri sana. Nadhani itakuwa sulihisho la matatizoumenisaidia sana kupanga......
atasafisha chumba chake na bathroom yao, na kwa vile anapenda kupika basi atapika jioni tu.
kuosha vyombo kazi ya dada, lol!
Hahahaah!! sikupatii picha ilikuwaje? na ka muda kangu kachache mie nimeamua nijifuliage tuu nguo zangu na za
hubby maana unaweza pata murder case bure!!!, niliwahi kukaa na binti wa Mtwara mbona nilikoma! chochote
kinachofanyika ndani kiwe kizuri au kibaya lazima kifike kwa majirani,sebulani kukawa jumba la sinema,mie
nikipita zangu kuelekea job watu wananing'ong'a tu wanajua a-z yangu, vitu vya ndani wanapewa majiran ukiuliza
mara kimevunjika,mara kimepotea, nilikuwa nalisha familia tatu bila kujua mchele unaweka ndani hata mwezi
haufiki,nilivyokuja kugundua kesho yake fasta nikarudisha kwao, sasahivi niko na wa Kigoma namshukuru Mungu siyo
mbaya sana yanavumilika.
unajua nashindwaga kuelewa kwa nini kuna wamama wanakuwa na urafiki na wadada wa kazi wa nyumba za jirani na wakati maboss wao hawajawazoea
kigoma ndio mpango mzima, mie sikuwahi kuzoea kukaa na wadada aisee, huyo wa kigoma ndio huyo huyo nimekaa nae mpaka alivyoniaga akaendeleze kijijini kwao huko sasa,tulipokuwa wapenzi na msukuma nilimkuta na houseboy wa kigoma,nimeolewa/nimezaa ndio akatuambia na yeye anataka kufanya biashara zake lakini kwa kutusaidia atamleta mke wake aje afanye kazi, watoto waliachwa na bibi yao kigoma, alikuwa bonge ya mdada, aisee hatakaa atokee, siku ananieleza ya kuondoka nilishindwa kujizuia kwa uchungu, niliumia sana, ni mdada ambae wote mpo safari na mna amani tele, anapenda watoto kupitiliza, nyumba ilikuwa kama yake, anafanya kitu kwa roho moja, sasa hivi nashindwa hata kwenda hapo njoro tu lazima nibebane na watoto, namwamini nani sasa?
ha haaaa, leo ndo nimeweza kupata nafasi ya kuweza kuwapa mrejesho................Aisee! duh!! kwa huyo hata mie ningelia, pole sana Mungu atakupatia mwingine. Fixed Point tupe mrejesho kikao ulikiweza au ndiyo huruma zilikuzidia tena mammy!(jocking)
ha haaaa, leo ndo nimeweza kupata nafasi ya kuweza kuwapa mrejesho................
Ukweli siku ile baada ya kumaliza sala za Usiku na wengine kuingia vyumbani, nilikaa na wasichana wangu na kuongea nao. Kila mtu alionyesha kuelewa na kuridhika na maamuzi yangu. Binti ana kazi za usafi asubuhi na kupika jioni, mchana anajisomea. Kazi nyingine zote za dada.
Jana nilitoka na binti, akaniambia ukweli alikuwa anashindwa kuacha kufanya ninapotuma hasa kama sijataja jina maana yeye pale ni nyumbani na dada ni mpita njia tu, hataki kunikwaza kama nimetuma na kitu hakijafanyika (UKWELI NAJIONA NIMEBARIKIWA SANA KUPATA HUYU BINTI).
Dada pia yupo na amani na anafanya kazi zake bila kunung'unika na tunaongea poa tu.
Nichukue muda huu kuwashukuru woooote mlionipa ushauri kwa hili. Mungu awabariki sana wapendwa wangu. Naamini pia wengine wenye changamoto kwa hili wanaweza kupata mwanga.
Amina na asante sanaSafiii na Hongera sana!! Mungu azidi kutawala amani,upendo na furaha vidumu katika familia yako.
una bahati kupata huyo binti. mi alikuja mtt wa wifi akiwa teenager, alikaa kwangu muda wa kutosha tu, mbona nilijuta. akiamka asubuhi anawasha TV miguu juu ya sofa anasubiri dada apike chai. Hata akikuona mama mwenye nyumba unachakalika yeye hajali. kumuuliza mbona humsaidii dada hata kupika chai, akanijibu yeye dada ndio msaidizi wa kazi, ndio majukumu yake.ha haaaa, leo ndo nimeweza kupata nafasi ya kuweza kuwapa mrejesho................