Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
- Thread starter
-
- #21
Asante rafiki, nitafanya hivyompangie binti yako muda wa kufanya kazi za shule mfano baada ya chakula cha jioni au mchana na umwambie dada wa kazi kuwa wakati huo ni wa binti yako kujisomea!so kama kuna kazi za ziada dada achukue jukumu la kuzifanya wakati huo!
sasa mimi nisikae na binti jamani?mpeleke kwa bibi akakae huko
najionaje mwepesi sasa mdogo wangu! asante sana kwa huu ushauri.Mpangie binti yako majukumu yake tena ambayo yatamfanya aweze kumaliza mapema na hivyo kupata muda wa kusoma na kupumzika pia na kuhusu huyo dada wa kazi mweleze kuwa hatakiwi kutaka usawa na binti yako kwani yeye unampa pesa kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kazi za ndani,muulize binti yako unamlipa shilingi ngapi?kama ni mwelewa na hana gubu atakaa chini na kutafakari na kisha kuchukua hatua nzuri.
na wala hutakiwi kuwa na hofu kuwa unamharibu bnitiyo kwa kumpa muda wa kupumzika na kujisomea nadhani mpaka hapo ulishamkunja angali mbichi na ndio maana umeona matunda yake kuwa ni mchapa kazi so naamini kamwe hatobadilika kwa huo msingi mzuri uliomwekea,ila kwa situation aliyonayo sasa hana budi kupitwa na baaadhi ya kazi ili ajisomee ni haki yake dada Fixed Point.
kumbe jambo ukilitoa kwa watu inakuwa kitu rahisi tu.....Usiwaze sana best ni simple sana , Fixed Point wewe ni mama mzuri unayejua malezi na ninategemea wewe ni rafiki
kwao si adui,ongea nao wote wawili wakiwepo na panga majukumu as mama kwa upendo kabisa as family talk,mueleweshe
binti yako kwamba anahitaji kuwa na muda mzuri wa kusoma yupo likizo lakini masomo hayako likizo,akishamaliza
yale majukumu yake apumzishe mwili then asome na anaposoma haitajiki mtu yeyote kumsumbua hii iwe ni Strict to
all family members. Muelimishe dada pia umuhimu wa kufanya kazi kwa wakati na kumaliza mapema ili awe na muda wa
kupumzika. ALL THE BEST.
karibu,asante nawe pia kwa kufunguka maana kupitia uzi huu wengi wataelimika.kumbe jambo ukilitoa kwa watu inakuwa kitu rahisi tu.....
nimewaza sana nifanyaje ili kutatua hili.
Asante sana rafiki kwa ushauri
ha haaaa, ngoja nitengeneze work permit, lol!
tatizo ni hilo la kuonea aibu dada wa kazi....Mueleze uyo dada wa kazi wala usione aibu,mm pia nina mtt ww dada angu,ilikua kama ww,dada wa kazi anataka waende sawa,juzi ninemuita,kwa upendo nikamwambia flani ni mwanafunzi,kazi zake nampangia mm,na akumbuke namlipa yy na c huyo mtt wa dada,so afanye kazi zake!na imekua hivyo,mueleze kwa upendo bila ukali!
mwanangu halalamiki, na wapo marafiki tu.Kwani huyo mtoto wako analalamika pindi afanyapo kazi pasu na huyo dada wa kazi??? Kama hanung'uniki mwache amsaidie dada kazi inaonekana kwanza wanaelewana vizur pili mwanao anajua wajibu wake kama mtoto wa kike sijaona ubaya wowote mdada!!
Jamani, mimi ni mama..... ndo maana naongelea mambo ya kazi za nyumbani......Samahani Fixed Point wewe ni baba au mama?
Nivizuri watoto wanapokua likizo wakafanya pia majukumu ya nyumbani wakishirikiana na wasaidizi wetu....na pia ni muhimu kwa mzazi kujua kwamba watoto wana JUKUMU KUBWA pia la Kujisomea na kufanya marudio ya masomo wawapo nyumbani.
Hapohapo ni muhimu wasaidizi wetu watambue kwamba wapo hapo kwa ajili ya kazi inayowapa kipato nikimaanisha kwamba wanatakiwa wayajue majukumu yao na kuyafanya ipasavyo
Binti yako anaweza kufanya kazi ambazo hazichukui muda mwingi kama kufanya usafi na kuendelea na kujisomea wakati msaidizi ataendelea na hizo nyingine - ikizingatiwa umesema hakuna kazi nyingi
unajua napenda dada naye ajione yupo nyumbani....Inakuaje binti yako afanye kazi sawa au zaidi ya msichana wa kazi? manake kaja hapo kwaajili ya kazi na mshahara analipwa, mimi kwetu tulikuwa na msichana wa kazi lakini pia mama yetu hakutaka kutulea malezi ya kutokufanya kazi kabisa alijitahidi tujue kazi, na tulijua lakini si kwa kufanya kazi sawa na mfanyakazi wetu, sana sana ilikuwa nguo zetu tunafua wenyewe, chumba chetu tunasafisha wenyewe, na kupika ilikuwa ni kumsaidia usiku tu tena yeye akipika mboga tutamsaidia kupika wali au chochote kile ambacho kinalika usiku huo au yeye akipika wali tutasaidia mboga lakini asilimia 90 ya kazi alikuwa anazifanya yye manake ndo zilizomleta
Asante mamii....karibu,asante nawe pia kwa kufunguka maana kupitia uzi huu wengi wataelimika.
Ila nimefurahi sana na ninakupongeza kwa kuuona umuhimu wa mtoto wa kike kujua kaz za nyumban,maana malezi ya siku hizi......??? Binti anakuja kuolewa hajui hata kudeki kisa masomo.
Big up mamaa na endelea kuwa mama mzuri!
Asante rafiki, nitajitahidi........hongera kwa kumfundisha binti yako kazi. suala simple tu, muite dada wa kazi, mwambie anatakiwa ajue majukumu yake vema hata kama binti atamsaidia. mwambie lipi atasaidiwa na lipi atatkiwa kulifanya mwenyewe. mwambie ukweli unataka binti yako nae apate muda wa kupumzika.