Bila shaka Wote Mupo salama.
Naomba ushauri wenu, Mwanangu kwa sasa ana miaka mitatu na nusu ila nimeamua nisimpeleke shule hizi za kawaida kusoma Darasa la kwanza Hadi la Saba na kuendelea.
Nimeona ikiwezekana nimpeleke akasomee ufundi moja kwa moja Kwa vitu ambayo ataweza kuvifanya hata akiwa na umri mdogo.
Mfano naweza kumpeleka chuo cha Urembo, au Music, ama Video and productions au mapishi ama Utangazaji.
Nyie wakuu Muna lipo la kumshauri Je inawezekana? Nini faida na hasara zake.
NB: anajua kusoma na kuandika.