Naomba ushauri juu ya online business

Naomba ushauri juu ya online business

Hot27

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2020
Posts
448
Reaction score
782
Habari wakuu wa JF nyote. Nipe mbele yenu nahitaji ushauri, mawazo na hata connection juu ya masuala ya online business.

Mimi ni kijana na nilipo nina access ya internet (kuanzia saa tatu asubuh hadi saambili usiku) hivyo naona kutumia fursa hii kuangalia tu video tiktok na kuzunguka mitandaoni ni vyema nijumuike kujifunza na hata kutizama uwezekano wa onlind hustling.

Nimepitia nyuzi nyingi humu ila nadhani bado nahitaji madini zaidi na hata connection yawezakuwa ni mambo ya online ama hata harakati nyingine.

KUNIHUSU
Mimi ni kijana wa miaka 23, ninaishi Buguruni, Dar es salaam. Niseme nakaribia kuhitimu chuo (ilibidi nihitimu mwaka jana ila nilipata changamoto hivyo nadaiwa kufanya mitihani miwili chuoni Mwanza) nimesomea masuala ya Mawasiliano ya Umma (Mass Communication).

Nina ujuzi wa masuala yote ya uandishi wa habari, kutoa huduma kwa wateja (kama sijakosea), graphics design (kwa kiasi chake), MC, mahesabu pia naweza kutumia lugha mbili pekee (Kiswahili na Kiingereza).

Natumaini naweza pata msaada kwenu, natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu.
 
Back
Top Bottom