Naomba ushauri juu ya mpenzi wangu.

Naomba ushauri juu ya mpenzi wangu.

adviceseeker

Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
5
Reaction score
0
Wana JF naomba mnisaidie mawazo na maamuzi.

Mimi nina msichana ambae ni mpenzi wangu tuna miaka saba kwenye mahusiano na mikwaluzano ipo ya hapa na pale ila tunaimaliza.Sasa kuna kipindi nilitaka kusafiri nikawa nimemtambulisha msichana kwa ndugu yangu wa karibu wa kiume umri sawa ikiwa nw kupeana namba za simu kama shemeji,baada ya utambulisho mwanzo kulikuwa hakuna uficho wakionana hata njiani wataniambi baadae nikasafiri nyuma wakawa wakutana na kutoana out sometimes wanasema wananitaharifu sometimes hawaniambii.Nikaja kurudi kutoka safari mambo nikakuta yamebadilka unajua msichana uliekaa nae muda mrefu kitu kikibadilika utaona dalili na kujua.Ikaanza mawasiliano baina ya huyo ndugu yangu yakawa siri kubwa na kifanikiwa kushika simu inakuwa balaa nikilazimisha kwa nguvu nakuta wanachat ndugu yangu pia akawa anaenda kwa huyo msichana kimya kimya nikigundua nikimuuliza msichana ananiambia angeniambia nikawa nimemaind sana then nikamuambia na kumuonya kuwa sitaki uficho tena na ndugu yangu pia nilimuambia the same,kuna siku msichana akampa kitu kikubwa ndugu yangu kimya kimya ila mimi hicho kitu nikaja kukijua maana nakifahamu na mbaya zaidi ndugu yangu alikileta nyumbani kwa kuficha nilipohisi nikampigia simu nakumuambia nimeona hiki na hiki alishituka na kuniambia samahani angeniambia then katika chunguza chunguza zangu nikakuta ndugu yangu kabadilisha jina la huyo msichana....

Nimeelezea kwa kifupi tu nisiwachoshe je mwana JF ungenishauri nifanyeje kama ungekuwa wewe?
 
unakaa na mtu kwenye mahusiano miaka 7 bado unamuita mpenzi?????
acha tu usaidiwe you deserve kwakweli
alichokosea ni kuwa tu na ndugu yako unless otherwise sioni tatizo hapo!!!!!!!
 
Mueleze huyo msichana kuwa unamuacha kwa kuwa anatoka na ndugu yako
 
Inaonekana jamaa situation ilimtokea muda kidogi na ameishafanya maamuzi dat y tenses zinakuwa zunaingiliana ila ninachiweza kukushauri huyo msichana sio mkweli atakuwa anaficha mengi piga chini huyo msichana utapata mwingine miaka ni namba tu hili undugu uendelee sio issue.
 
Sidhani kama unategemea watu wakushauri ya kwamba Uendelee kuwa nae ...si ndio Jibaba?
1069365_563734773690870_1485415470_n.jpg
 
Inaonekana jamaa situation ilimtokea muda kidogi na ameishafanya maamuzi dat y tenses zinakuwa zunaingiliana ila ninachiweza kukushauri huyo msichana sio mkweli atakuwa anaficha mengi piga chini huyo msichana utapata mwingine miaka ni namba tu hili undugu uendelee sio issue.

asante mkuu.
 
^^
Ngoja nikuitie Kaunga atakusaidia na akija msikilize kwa umakini
^^
 
Last edited by a moderator:
miaka saba ni mingi sana kwa uchumba, kama unampenda kalipe mahari kwao na uoe kabisa, kisha utakuwa umamdhibiti ndugu yako kuanza kurusha ndoana, chelea chelea utakuta mwana si wako. Hata hivyo binti kakusitahi sana 7 yrs................??? sidhani kama ningeweza na ukiendelea kuomba ushauri utakuta nduguyo keshawahi kumlipia mahari, kalagabaho!!

ila karibu jf maana umejiunga leo na moja kwa moja umeingia chumbani kabla hata ya kukaa sebleni looh!!
 
^^
Ngoja nikuitie Kaunga atakusaidia na akija msikilize kwa umakini
^^

Yaani nimechoka mwili akili na roho hata kumsoma dogo nimeshindwa.
We mshauri tu, nitarudi baadaye.
 
Last edited by a moderator:
Utawala wako umeshindwa, hapo hamna maswal ... piga chn kabla haijala kwako mazima!Kama ni mchezo wa draft then mwenzio ana king 4 we una 1, panga kete tu kaka!!!!
 
Kwa kweli kaa na mpnz wko ujue msimamo wake kwako kama unachako au la!
 
Piga chini miaka 7 uliochezea hiyo kitu yake inatosha. Utamu wote umeula

Mwachie huyo ndugu yako ale makombo yako. Tafuta tena mwingine.


"Sizitaki mbichi hizi".
 
Yaani nimechoka mwili akili na roho hata kumsoma dogo nimeshindwa.
We mshauri tu, nitarudi baadaye.

^^
Nakuaminia ujue linapokuja suala la guidance and counselling juu ya matatizo ya wanawake!
^^
 
Wana JF naomba mnisaidie mawazo na maamuzi.

Mimi nina msichana ambae ni mpenzi wangu tuna miaka saba kwenye mahusiano na mikwaluzano ipo ya hapa na pale ila tunaimaliza.Sasa kuna kipindi nilitaka kusafiri nikawa nimemtambulisha msichana kwa ndugu yangu wa karibu wa kiume umri sawa ikiwa nw kupeana namba za simu kama shemeji,baada ya utambulisho mwanzo kulikuwa hakuna uficho wakionana hata njiani wataniambi baadae nikasafiri nyuma wakawa wakutana na kutoana out sometimes wanasema wananitaharifu sometimes hawaniambii.Nikaja kurudi kutoka safari mambo nikakuta yamebadilka unajua msichana uliekaa nae muda mrefu kitu kikibadilika utaona dalili na kujua.Ikaanza mawasiliano baina ya huyo ndugu yangu yakawa siri kubwa na kifanikiwa kushika simu inakuwa balaa nikilazimisha kwa nguvu nakuta wanachat ndugu yangu pia akawa anaenda kwa huyo msichana kimya kimya nikigundua nikimuuliza msichana ananiambia angeniambia nikawa nimemaind sana then nikamuambia na kumuonya kuwa sitaki uficho tena na ndugu yangu pia nilimuambia the same,kuna siku msichana akampa kitu kikubwa ndugu yangu kimya kimya ila mimi hicho kitu nikaja kukijua maana nakifahamu na mbaya zaidi ndugu yangu alikileta nyumbani kwa kuficha nilipohisi nikampigia simu nakumuambia nimeona hiki na hiki alishituka na kuniambia samahani angeniambia then katika chunguza chunguza zangu nikakuta ndugu yangu kabadilisha jina la huyo msichana....

Nimeelezea kwa kifupi tu nisiwachoshe je mwana JF ungenishauri nifanyeje kama ungekuwa wewe?
.


Pole, huyo keshakuacha na huyo nduguyo ndo kashika usukani muhimu angalia mbele tafuta mwingine maisha yaendeleee
 
Back
Top Bottom