Eversmilin Gal
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 778
- 269
Naishi na mke wangu vizuri tu siku nyingi, lakini familia yangu ni kubwa kiasi kwamba kila baada ya muda fulani napata mgeni wa kuja kututembelea. Kama ni mwanaume kidogo afadhali hata watasalimiana na atamuhudumia at least kiroho safi, mbaya zaidi ni wa jinsia ya kike. Hata kama anajua kabisa ni ndugu japo wa mbali kidogo anakuwa mzito sana kumuhudumia kwa vikwazo kibao mara oooh naumwa/sijisikii vizuri/n.k. ilihali sura ikionyesha dhahiri kwamba hajafurahia ujio wa huyo mtu.
Sasa nimepata bahati ya kuwapata watoto wawili wa kike wa kaka zangu, kutoka kijijini ili waje kujiendeleza kielimu, mmoja ni mdogo yuko darasa la II na mwingine amemaliza la saba nataka angalau apate kozi za kujiendeleza hapa mjini. Sasa wife ananambia ye ataki kuwaona la sivyo ataondoka, na nnavyoandika hapa, ameamua kuondoka kweli leo hii. Lakini siku mbili baada ya hawa watoto kufika kwangu, na mdogo wake pia ambaye amekuja kusoma chuo naye alifika kwangu na anaishi kwangu na anasoma chuo kwa gharama zangu!
Hivi ni kweli niachie hawa watoto warudi nyumbani ili nikae na mke na shemeji yangu ndani, au nimwachie mke aende sababu njia zote za kujaribu kumwelimisha mke wangu juu ya jukumu na umuhimu wangu kuwasaidia watoto hawa amezikataa, hataki kabisa kuongea juu yao.
Naomba ushauri wenu.
ahaaaaaaaaaaaa! Ticha ndo umetema vitu hizooooo design za kifisadi kama mtoto Nata??????????? Daaaaah! I cant believe this!!!!!!!!!!!
naombeni msininione binafsi,aa... ila kuishi na ndugu wa mume ni lawama maana waweza kujitoa kwa roho yako yote lakini hawaridhiki,mi niliishi na shem angu mwaka jana akiwa form two alikua jeuri,kiburi aambiwe kitu na kaka yake lakini sio mimi,nimeumwa mimi ye alikua likizo basi hata anisaidie chochote hamna anaenda kuzurura,lakini angekua mdogo wangu hapo angenisaidia,ila kiukweli tunamkaribisha shetani mana hamuwezi kujinafasi na mume wako
nachoshauri ni kuwasaidia wakiwa kwa wazazi wao au wapelekwe bording au hostel uwahudumie huko
Naomba Unisikilize kwa makini,
Katika dunia hii mara nyingi binadamu tunapata riziki kwa sababu maalumu,tunapata riziki amabzo so zetu.wakati mwingine unaweza pata fedha kumbe fedha hizo ni kwa sababu ya watu flani ambao wamekuwa wakimwomba Mungu awasaidie kujikwamua,na sasa mungu ameangalia mahala pa kupitishia/Kujibu maombi yao akaaona apitishie kwako.Sasa basi unajukumu la kufikisha kile ambacho umetumwa na mungu,na baada ya kufikisha utalipwa na yeye kwa kile utakachokiua umefanya,
lakini pia,umekua unaweza kumudu gharama zote hizo kwa msaada wa Mungu,inafikia siku sasa Mungu anaitaji kuona wewe unamrudishia nini Mungu.Katika hali hiyo tegemea shetani hafurahishwi na mahusiano mazuri yaliopo katiu yako na Mungu kwakua mungu anakuwezesha na wewe unamtolea kwa njia ya kuwasaidia wasiokua na uwezo.kwa sasabuhiyo basi shetani lazima ajaribu kuingilia kati ili kuvuruga na shetani kaaamua kumtumia wakala wake.
Sasa basi, uwamuzi unao wewe,...ushauri wangu ni kwamba yakupasa kua mtu mwenye msimamo wa kukata shetani kukupelekesha,najua sheji anakubip,wewe usimpigie, akitest wewe fanya kweli,usimtafute,usimfate,piga kimya,amin unachofanya wala si unachopelekwa kama remote,
Ndugu yangu ukiyumba tu ndio umasikini umekukuta
Tatizo kubwa hapo ninaloweza kuliona ni mke wako kuogopa mzigo wa ulezi.
Kulea mtoto wa darasa la pili, na mwengine aliyepo katika umri ambao watoto wengi huwa wakaidi, si jambo dogo na inawezekana ikawa hilo linalomuogopesha japo kuwa hajachukua njia sahihi kufikisha ujumbe wake (kama hajakueleza hili)
Mkilizungumza suala hilo linaweza kukusaidia kidogo
Naishi na mke wangu vizuri tu siku nyingi, lakini familia yangu ni kubwa kiasi kwamba kila baada ya muda fulani napata mgeni wa kuja kututembelea. Kama ni mwanaume kidogo afadhali hata watasalimiana na atamuhudumia at least kiroho safi, mbaya zaidi ni wa jinsia ya kike. Hata kama anajua kabisa ni ndugu japo wa mbali kidogo anakuwa mzito sana kumuhudumia kwa vikwazo kibao mara oooh naumwa/sijisikii vizuri/n.k. ilihali sura ikionyesha dhahiri kwamba hajafurahia ujio wa huyo mtu.
Sasa nimepata bahati ya kuwapata watoto wawili wa kike wa kaka zangu, kutoka kijijini ili waje kujiendeleza kielimu, mmoja ni mdogo yuko darasa la II na mwingine amemaliza la saba nataka angalau apate kozi za kujiendeleza hapa mjini. Sasa wife ananambia ye ataki kuwaona la sivyo ataondoka, na nnavyoandika hapa, ameamua kuondoka kweli leo hii. Lakini siku mbili baada ya hawa watoto kufika kwangu, na mdogo wake pia ambaye amekuja kusoma chuo naye alifika kwangu na anaishi kwangu na anasoma chuo kwa gharama zangu!
Hivi ni kweli niachie hawa watoto warudi nyumbani ili nikae na mke na shemeji yangu ndani, au nimwachie mke aende sababu njia zote za kujaribu kumwelimisha mke wangu juu ya jukumu na umuhimu wangu kuwasaidia watoto hawa amezikataa, hataki kabisa kuongea juu yao.
Naomba ushauri wenu.
Inavyoonesha Mkeo Hajakataa Kuwapa Msaada Hao Nduguzo,Tatizo Hawi Huru Iwapo Nduguzo Mtaishi Nao!
Kama Kuna Uwezekano Wa Kuwahudumia Nduguzo,Waki Mbali Na Nyumba Yako!..Basi Waondoe Nyumbani Na Endelea Kuwasomesha Wakiwa Mbali!
Msikilize Mkeo Banah!
baadhi ya wanawake ni kama watoto, anapima kina cha maji.
Ila angalia pia kakulia mazingira gani, kama kwao alizoea kuishi wao wa familia yao tu, basi lazima aone mzigo kuishi na nduguzo.