Naomba ushauri jinsi ya kuuza nguruwe

Naomba ushauri jinsi ya kuuza nguruwe

Mapondo Mapoka

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2015
Posts
274
Reaction score
135
Wakuu natumaini hamjambo.
Kichwa cha habari chajieleza hapo juu.
Naomba kueleweshwa,ni njia gani kati ya kuuza nyama ya nguruwe kwa kilo jumla na kuuza nguruwe mzima mzima. Ipi ni njia nzuri na yenye faida?

Asanteni.
 
Mradi wa nguruwe upo Mpanda Katavi. Kwasasa kuna nguruwe wakubwa kumi ambao wako tayari kwa kuliwa na watoto 11 wenye miezi 3 pia ni mbegu kubwa.
Karibu tufanye biashara.
 
Kuchinja na kuuza kwa kilo ndo unapata bei ya uhalisia zaidi na naweza kusema inalipa japo sijajua gharama ulizotumia.
 
Wakuu natumaini hamjambo.
Kichwa cha habari chajieleza hapo juu.
Naomba kueleweshwa,ni njia gani kati ya kuuza nyama ya nguruwe kwa kilo jumla na kuuza nguruwe mzima mzima. Ipi ni njia nzuri na yenye faida?

Asanteni.
Daaah! Umenitoa mate asb yote hii [emoji39][emoji39][emoji39]
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Umejuaje? Nimetoroka ofisini nipo sehemu naishushia na kasparletta. Ingekua insta huku ningekutumia kapicha kuthibitisha.



Hahaa,umekosea kidogo sana kwa kushushia na sparleta. Ungetupia safari mbili au balimi moja ya baridi,saiz ungekua na confidence za kutosha.
 
Weka mzigo kwenye mzani halafu piga bei ya JUMLA. Yaani kama kwenu kilo ni 8000 kama huku kwetu, we uza kilo 5000 ila iwe baada ya kutoa kilo 3 za Mafuta na mifupa na kilo 2 za mbolea. Asante
 
Unauzaje akiwa mzima boss na wana kilo ngapi?
Wakuu natumaini hamjambo.
Kichwa cha habari chajieleza hapo juu.
Naomba kueleweshwa,ni njia gani kati ya kuuza nyama ya nguruwe kwa kilo jumla na kuuza nguruwe mzima mzima. Ipi ni njia nzuri na yenye faida?

Asanteni.
 
Mkuu, huwa una mahitaji ya wastani wa nguruwe wangapi kwa kipindi cha muda gani?.

Je unawafuata mwenyewe mikoani au?

Wastani wa nguruwe 21 kwa miezi 3. Mm ni mfugaji pia ni mnunuzi wa nguruwe wakubwa kwaajili ya kuwapandisha na kuzaa kwa kipindi kifupi. Hivyo, nina nguruwe wa rika zote Kambini kwangu,na mradi huu upo Mpanda Katavi. Kwasasa nguruwe 10 wanaofaa kuliwa wanauzwa ,na wengine 12 ni watoto wa zaidi ya miezi 3 .
Kama uko maeneo hayo karibu pm tufanye biashara mkuu.
 
Back
Top Bottom