Naomba ushauri jinsi ya kuongea na binti anayekua

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,557
45,871
Damu ni nzito kuliko maji leo nimeumia sana.

Kuna Kaka yangu aliachana na mkewe kitambo sana mtoto akiwa na 2 yrs, yule Mama akamuacha mtoto. Mtoto kalelewa na baba yake since then Wala bro hajaoa tena masikini sijui alipigwa tukio gani.

Changamoto binti amekuwa ana 12 yrs sasa, nyumbani kwao yupo na baba na dada wa kazi tu. Leo alikuja kuniona nimeona mabadiliko makubwa kwa mtoto chunusi,ckifua etc nikajua huyu tayari. Ila nimeogopa kumuuliza, pia kumshauri Kama mama.

Naombeni ushauri sitaki niece wangu apate changamoto za kimwili kama Mimi aunty yake sitaki apitie maisha yangu. Kusema kweli sikufundishwa chochote na mtu japo simlaumu mtu kwa niliopitia ila sitaki mwingine yampate.
 
Zamani kulikua na mradi wa kufundishia vijana changamoto na mabadiliko ya balehe. Walichapisha vitabu vidogo vidogo. Vilieleza mabadiliko tangu kuanza kwa gololi kwenye matiti, korodani na kuota nywele.

Hivi vitabu vilifundisha wet dreams na kujifungia taulo ukiwa mwezini. Kwangu mimi vilinisaidia sana.
 
Navikumbuka sijui nitapata wapi me pia nilijifunza humo
 
Mfundishe kuvaa pedi.

Mwambie ajue kua kutokwa na maji maji ukeni ni kawaida unless kama yana rangi au harufu.

Mfundishe kuhesabu siku.

Mwambie kuhusu magonjwa ya ngono.

Nilishiriki mwezi uliopita katika kuelezea magonjwa ya ngono kwa mtoto wa shemeji, binti wa la sita tayari anaingia mwezini.
 
Kwa kwel mm nikiangalia wanangu nawaza wakifika huko nitaanzia wapi, japo watoto wa siku hizi wanajua mengi sasa kwenye hayo mengi kuna mabaya funga rroho sema nae maana dunia yenyewe hii mambo yamekua mengi hasa
 
Mfanye awe rafiki yako kabla ya chochote...awe comfortable kwako,ajisikie huru sana kuwa nawe.Utajua hulka yake,urahisi wake kupokea mambo au ugumu wake na itakusaidia kujua namna au lugha ipi utumie kumfikishia mambo.Then itakuwa rahisi kuongea nae chochote,atakueleza chochote,atakueleza anayowaza, anayopenda, anayohofia, anayosikia, na itakupa mwanga wa kujua wapi ufundishe,urekebishe,au ukazie,au umuepushe.
 
Mpeleke washauri wa masuala ya uzazi ..
Si kila siku mnatangaziwa mabinti wapelekwe huko wasije pata mimba

Wapewe ushauri mapema wa kitaalam
 
Tengeneza mazoea nae(urafiki kwanza) ili ajiachie asikuogope then mwambie kila kitu unachoona anapaswa kukitambua.Maana huenda hapo alipo rafiki yake mkubwa ni binti wa kaz aliyemlea so kama binti wa kaz tabia yake ni njema bas kamjaza mema pia
 
Mfanye awe rafiki yako kabla ya chochote...awe comfortable kwako,ajisikie huru sana kuwa nawe.Utajua hulka yake,urahisi wake kupokea mambo au ugumu wake na itakusaidia kujua namna au lugha ipi utumie kumfikishia mambo.Then itakuwa rahisi kuongea nae chochote,atakueleza chochote,atakueleza anayowaza, anayopenda, anayohofia, anayosikia, na itakupa mwanga wa kujua wapi ufundishe,urekebishe,au ukazie,au umuepushe.
I agree. Ninaye dada angu ambae ni kama mama yangu tu.

Huyu dada anajua mambo mengi sana kuhusu changamoto za vijana na ukuaji. Yeye ana approach kama hii ya kubefriend watoto na vijana. Yani ukimkuta amekaa na vijana wanapiga story utafurahi.

Lakini katika njia hii kumemuwezesha kuwa karibu na their psychology. Anajua nini cha kuongea, kwa wakati upi. Hilo limemsaidia sana kuwalea watoto wake wote.

Ukiwa mzazi rafiki sometimes ni rahisi sana kudeal na matatizo ya watoto katika ukuaji. Lakini pia wengine wanaweza kuwa na other suggestions. I stand to be corrected.
 
Damu ni nzito kuliko maji leo nimeumia sana.

Kuna Kaka yangu aliachana na mkewe kitambo sana mtoto akiwa na 2 yrs, yule Mama akamuacha mtoto. Mtoto kalelewa na baba yake since then Wala bro hajaoa tena masikini sijui alipigwa tukio gani.

Changamoto binti amekuwa ana 12 yrs sasa, nyumbani kwao yupo na baba na dada wa kazi tu. Leo alikuja kuniona nimeona mabadiliko makubwa kwa mtoto chunusi,ckifua etc nikajua huyu tayari. Ila nimeogopa kumuuliza, pia kumshauri Kama mama.

Naombeni ushauri sitaki niece wangu apate changamoto za kimwili kama Mimi aunty yake sitaki apitie maisha yangu. Kusema kweli sikufundishwa chochote na mtu japo simlaumu mtu kwa niliopitia ila sitaki mwingine yampate.
The only person atakayeweza mpatia ushauri mzuri na akausikiliza ni baba yake mzazi tu. Baba akae na mwanae wa kike na wazungumze. Hakuna mwingine. Hata mama yake hawezi kumsaidia chochote. All the best.
 
Back
Top Bottom