Naomba ushauri jinsi ya kumuacha huyu Mwanamke mwenye upendo wa dhati

I hope hamjambo ndugu zangu wote wana JF.

Naomba kutanguliza samahani kwa yoyote nitakae mkwanza juu ya hili naomba ushauri wenu nifanye nn? Mnivumilie sio mwandishi mzuri sana. Katika mishe zangu za kila siku nilitokea kuonana na mdada fulani kiukweli mzuri wa kila kitu na mwenye kazi yake na sehemu yake ya kuishi na mwenye dini haswa na mwenye kujistiri.

Kikweli baada ya kumuona nilitokea kuvutiwa naye na kuongea naye na kuchukua number yake na alivutiwa na mimi tangu siku ya kwanza tu kuongea naye she’s was so happy kuongea na mimi.

Tuliendelea kuongea kawaida as friends after 3 weeks nijaribu kufikisha hisia zangu juu yake nieleze kiasi gani nimevutiwa nae na kutokea kumpemda toka the first day kuonana nae.

Tuliingia kwenye mahusiano rasmi ya kimapenzi. Kiukweli sikuwa nimempenda zaidi ya kumtamani mwili wake. Kadri siku zinavyozidi kwenda nikiona anazidi kunionesha kunipenda na kujail zaidi kuhusu mimi kuletewa zawadi kama t-shirt, saa na viatu nikiwa sijawahi kumpa chochote na zaidi hali yangu ya kiuchumi nimemzidi kwa kila kitu

After many days tulikutana kimwili zaidi ya mara tatu after that nilianza kuwa busy hata nikiona simu yake nahisi kama ananisumbua hata kujibu text nashindwa na hachoki kutuma texts wala kupiga anaishia kulia kila siku. Sometimes naumia kumuona hivyo ila i want her to move on na maisha yake kizazaa kilianza hapa.

Kwa yote niliyofanyia hakuweza kuniacha wala kuniambia sikutaki aliendelea kunivumilia mengi niliyofanya sidhani kama kuna mwanamke anaweza kuvumilia na kuendelea kuwa na mwanaume huyo. Niumia zaidi kumuona akiteseka niliamua kumwambia tuachane hataki kusikia hilo wala kuelewa alisema siwezi kuachana na wewe na weka akilini mwako. Niliamua kumblock number zake maybe angekuweza ku-move on ila hali kutokea hilo alianza kunitafuta na kila number anaweza hata akaomba hata number ya mpita njia anipigie mimi na kuanza kulia hata mbele za watu kwanini nimemblock.

Kila siku anasema mimi siwezi kukuacha kamwe na nipo tayari kwa kila kitu hata ukioa mwanamke mwingine zaid yangu nipo tayari kukuzalia ila kuwa na mwanaume mwengine siwez btw nimeshindwa kumuacha wala kuniacha na hakuwahi kula hela yangu hata siku moja zaid ya kulipia hotel tulale. Naomba radhi juu ya hili ni hisia tu.

NAOMBA USHAURI NIFANYE NINI NA SIPO TAYARI KUWA MUME WAKE NA ANAJUA HILO.

USIOE MWANAMKE KWA KUWA UNAMUONEA HURUMA sikikiza moyo wako na uingie kwenye maombi mkuu.
 
Yan kumbe wanaume wa ajabu mpo wengi tu kama dudu inakuwasha nenda kanunue Dada poas huko kuliko kucheza na hisia za mtu, kumdanganya mdada wa watu unampenda mwisho wa siku unamdump with no reasons
Wacha agongwe afu apite hivi.
 
Amini usiamini huyu mwanamke ukimuacha ipo siku haya na wewe yatakurudia utakutana na mwanamke unayemuona ni sahihi kwako na yeye hatakuwa na chembe ya upendo kwako atakuja kukusumbua sana na utamkumbuka huyu unayetaka umuache,,upendo wa kweli wakati mwingine unahitaji muda,,kadiri muda utakavyokuwa unaenda ipo siku utajikuta unampenda
 
Ngoja nikwambie kitu nikiwa kama mzazi wako kama siyo babu yako (Nina miaka 76!)

Huyo mwanamke muoe kama unaweza. Huyo ni soulimeti wako na huwa wanakuja mara moja tu maishani mwetu. Ukimwachia basi jua imekula kwako na hakuna rangi ambayo utaacha ona hapa duniani katika tasnia hii ya mapenzi. Mpaka utasingizia amekuroga kumbe ni Karma tu inafanya kazi yake.

Fanya hivi: Mchunguze kama kweli hana wanaume wengine. Peleleza historia yake vizuri. Ukikuta kila kitu kinatiki basi peleka posa mapema na kabla ya mwaka huu haujaisha weka pisi ndani ule mema ya nchi. Na umpende kwa moyo wako wote na kumheshimu. Mtafika mbali sana!

Na labda nikuulize: kwa nini unakazana kumuacha? Ana tatizo gani? Hakidhi viwango vyako ama? Mnatofautiana dini? Kwa nini unapambana kumuacha?

Umeokota lulu ya thamani sana katika shimo la takataka japo hujui. Amka!
Ngosha umenena. Kuna jamaa nakumbuka na nikacheka sana, alisema huna kupindisha pindisha. Huju jamaa asipo kuelewa basi kichwa chake ni mapera.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huyo mwanamke anashida anahitaji ushauri haya mambo ya sijui umri umeenda sijaolewa wala kuzaa ndo yanawafanya watu wawe kama vichaa,
 
Hata mimi niliwahi kutongoza singo maza bila kujua alikua mzuri sana bi dada baada ya muda akaniganda balaa nilivyo gundua ana mtoto nikamwambia tuachane we nenda kwenye familia yako muelewane na baba mtoto wako, maana siyo ndoto yangu kuwa na mwanamke aliezalishwa na mtu Mwingine sitaki migogoro.

Cha ajabu akaanza kunitishia eti atajiua kisa mi nataka kumuacha nilicho mwambia ni kuwa Kama anataka kufa asipate shida twende nimsindike baharini akajirushe ila mimi sipo tayari kuoa singo maza.

Akaniambia Kama simtak basi anaomba hata awe na uhusiano wa Siri tu na mimi, siku moja nikamshrikisha mama mmoja hiv jiran kuhusu hiyo stori bila kumwambia kuwa ni mkasa wangu, yule mama akanijibu mwanamke Kama humtaki na umeshamwambia ila anakung'an'gania hakikisha humrudii utalogwa.
 
Hata mimi niliwahi kutongoza singo maza bila kujua alikua mzuri sana bi dada baada ya muda akaniganda balaa nilivyo gundua ana mtoto nikamwambia tuachane we nenda kwenye familia yako muelewane na baba mtoto wako, maana siyo ndoto yangu kuwa na mwanamke aliezalishwa na mtu Mwingine sitaki migogoro.

Cha ajabu akaanza kunitishia eti atajiua kisa mi nataka kumuacha nilicho mwambia ni kuwa Kama anataka kufa asipate shida twende nimsindike baharini akajirushe ila mimi sipo tayari kuoa singo maza.

Akaniambia Kama simtak basi anaomba hata awe na uhusiano wa Siri tu na mimi, siku moja nikamshrikisha mama mmoja hiv jiran kuhusu hiyo stori bila kumwambia kuwa ni mkasa wangu, yule mama akanijibu mwanamke Kama humtaki na umeshamwambia ila anakung'an'gania hakikisha humrudii utalogwa.

kwhy mkuu nitalogwa nn mm.
 
Furushi, halafu baadae jitu linakuja na thread "wanawake siku hizi hakuna" kumbe unachuma malipo ya matendo yako.
Mwambie tu ukweli kwamba humtaki ili uwahi kwenda kukutana na balaa lako linalokungoja huko.

Afanye haraka awahi ili at least ateseke bado akiwa kijana...akijichelewesha balaa litamkuta kawa babu
 
Shukran sna kwa ushaur wako ukiwa kam mzazi wang sidhan kam mzee wng umri huo amefika.

Mwnamke hana tatz lolote n she’s good for everything. Na pia dini sawa muslim wote. Ila kikubwa kutaka kuachana sikuwh kumpend zaid ya kumtamn kila ninaemuosha mtu anasem nimuoe she’s so cute.

Nilikutana nae nikiwa na mataminio ya kimwili tu n nikiwa n mwanamk mwengn nahitaji kumuoa coz ndo ninaempnd na kuw na malengo nae but hanipend kama anavyonipnd huyo girl.

Espy Atoto Balaa unalolizungumia hilo hapo tayari analo.. ..
 
Back
Top Bottom