Naomba Ushauri jinsi ya kudai deni Bila kupoteza urafiki

Tall Guy fam

JF-Expert Member
Jan 16, 2017
917
1,093
Habari zenu, Bila kupoteza muda, Ningependa nianze na historia kidogo.

Nina rafiki yangu naweza sema ni the best friend I have, tulikutana miaka ya nyuma kipindi tunasoma a level kama miaka 12 iliyopita, immediately tukawa marafiki, Mpaka sasa navyozungumza. Bado ni marafiki ingawa ninaona Kuna uwezekano urafiki ukaisha endapo sitatumia busara.

Mwaka jana mwezi wa nane, rafiki yangu aliniomba nimkopeshe kiasi flani cha pesa, ni kawaida mimi na yeye kukopeshana na Hua tunalipana. Safari hii aliniomba laki 4 nikampa 3 kwa makubaliano anirudishie mwezi wa kumi mwaka jana.

Muda ulipofika, akashindwa kunipa he apologized and told me alikosa mkopo so instead of kunirudishia ameitumia kucover some of the costs. He promised by Dec atakua amerekebisha.

Dec ikafika, sikutaka kumpressure sana, ni Ile nampigia namwambia vipi hela ananiambia nitakutumia namuacha tunaendelea kuwasiliana kama kawaida talking about other stuffs.

Muda ukaenda, Hatukuwasiliana kwa weeks kadhaa, Ilipofika mid Jan 2017 nikampigia kumwambia anitumie hela cause nimekopa kwa mtu ananidai (which is true) so he told me atanitumia kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Jan.

Ikapita Jan, ikafika Feb 3, kimya. Sasa ikawa kila nikampigia hapokei, texts hajibu tena, yupo kimya tu. Mpaka tar 7 bado akawa kimya ingawa hapo kati alinipigia kuniambia atanicheki jioni ya hiyo siku which he didn't. So Nikaanza kupata hasira na kulose patience. Nikajitahidi kadri ya uwezo wangu kuidhibiti hiyo Hali na naweza sema kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa.

Tangu tar 8 Mpaka Leo sijamtafuta na yeye hajanicheki. Niliamua kukaa kimya kwanza na kuomba Ushauri maana hasira nilizonazo naweza sema maneno yasiyo na staha. Kwa kifupi sitaki kupoteza urafiki, ni mtu wangu wa karibu mno na pia ninataka pesa yangu.

Naombeni Ushauri nifanye nini ili anilipe Bila ya kupoteza urafiki huu? Najua ni ndefu sana ila kama umefika hapa, karibu.
 
Mkuu Kama kweli unataka huo urafiki uendelee mwambie umemsamehe hilo deni.

Vinginevyo kinyongo na uchungu havitakuisha ukichanganya na hasira hapatakua na urafiki hapo Bali unafiki.

Kulipa madeni ni kipaji, sio kila mtu anaweza.
 
sikia mwanangu..unajua kukopa pesa ni rahisi sana kuliko kutudisha??? na hakunaga uaminifu kwenye pesa hata kama ni ndugu wa damu(kaka or dada)...unavomkopesha ndugu make sure kuna maandishi na mashaidi...au unahold kitu(asset) chochote chenye thamani zaidi ya deni....kwa hali hii ya sahvi pesa ni ngumu kupatokana, so mi nakupa tu pole mkuu kuna uwezekano mkubwa ukampoteza rafiki na pesa pia usipata..mimi nimepotezana na marafiki kibao kutokana na kuwadai kikubwa samehe tu na Kama riziki utapata tu pesa nyingine
 
sikia mwanangu..unajua kukopa pesa ni rahisi sana kuliko kutudisha??? na hakunaga uaminifu kwenye pesa hata kama ni ndugu wa damu(kaka or dada)...unavomkopesha ndugu make sure kuna maandishi na mashaidi...au unahold kitu(asset) chochote chenye thamani zaidi ya deni....kwa hali hii ya sahvi pesa ni ngumu kupatokana, so mi nakupa tu pole mkuu kuna uwezekano mkubwa ukampoteza rafiki na pesa pia usipata..mimi nimepotezana na marafiki kibao kutokana na kuwadai kikubwa samehe tu na Kama riziki utapata tu pesa nyingine

Asante, mkuu. Kiukweli nimejifunza Hakuna uaminifu kwenye pesa.
 
Mwaka 2009 nilikopeshaga rafiki yangu shilingi lako 5 kwamba baada ya mwezi atanirufishia hela yangu! Niliona lakini hiyo hela nilianza kulipwa baada ya miezi 4 tena nikawa nalipwa elfu 50-50. Lile deni lilichukua mda mrefu kumalizika kulipwa na hata hela iliyokuwa inarudishwa nilishindwa kuitunza nikilipwa hicho kidogo nakila mpaka deni likaisha na mimi nikawa sina hata hiyo laki 5.
Tatizo jingine marafiki hupenda penda sana kukopa hata kama shida aliyonayo wala si ya mhimu kiviile, yaani anaweza akaipotezea. Sasa mimi nilishaacha kukopesha, na nikiamua kukuoopesha basi ni kiasi kidogo sana hata kama ukknidhurumu basi hakiniumi kwani huwa nimejiandaa kwa hilo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom