Mkuu nazungumzia Mamilioni ya pesa, sio kumi, ishirini. na ninaangalia huko nako kwenda, nataka kusitisha upotevu wa pesa, nilitegemea nikioa, nitazidisha nguvu za kutafuta pesa alafu kuna mtu wa kuzisimamia.
Utafutaji wangu wa pesa ni wa kukaa ofisini asubuhi hadi usiku, na muda unavyokwenda nahitajika kukaa ofisini zaidi, niliacha kazi ili niweze kusimamia pesa mwenyewe kwa kufanya mambo yangu binafsi, nimelazimika kurudi kwenye ajira, nimempa kazi ya kusimamia ujenzi wa nyumba, sikumuambia atafute pesa za kujenga nyumba lakini ameshindwa.
basi usimpe pesa bana, yanini ugomvi fanya kama vile uanishi na katoto ambako hakajui matumizi ya hela halafu fanya kila kitu mwenyewe..naamini unaweza..halafu baada ya miaka 2 mkalishe chini umpe tathmini ya kabla ya ndoa, baada ya ndoa na baada ya wewe kumnyima fursa ya kushika pesa zako..ulinganishe maendeleo yenu yalivyo..
wala uismdai hizo hela ulizompa wewe mwache afanye hayo mabiashara yake na wala usimfuatilie, anza upya as if umeibiwa a utafanikiwa, na yeye ataona aibu km ana mshipa wa fahamu..
wanawake wengine bana wanatia kichefchefu kweli..sijui kwa nini sisi hatupati waume wa staili hii
Pole ndugu,pesa anazo na akimaliza mipango yake anakumaliza.muombe Mungu akunusuru
Thanks. Hili nimeishalianzisha, sasa kazi yake au nafasi yake kwenye familia inakuwa nini?
Ndugu yangu mi naona hapa mambo yooote haya na hasira zooote hizi ni kutokana na mitihani uliyoipata ya kiafya na Utafutaji pesa wako bahati mbaya umeshuka na si kama zamani. Wewe jiulize mbona ulivyokuwa unaingiza kwa wingi haya matatizo yooote hukuyaona?
Mke ana wajibu mkubwa sana kutambua na kutoa mchango mkubwa pale ambapo hali ya kiuchumi itashuka ndani ya nyumba. Mambo yaliyopita yamepita ila anatakiwa atoe mchango wake ndani ya nyumba ili angalau muishi kwa amani. Mpe majukumu ya kulipia vitu humo ndani ya nyumba na mueleze kuwa uwezo wako kifedha ukirudi kama zamani utampokea. Uking'ang'ania kuingilia biashara zake mtagombana maana sasa hata heshma kwako imeshuka atakuwa anakuona kama uko chini yake kwa kuwa yeye huenda anajiona ana pesa na afya kuliko wewe.
Kipindi hiki muombe anunue labda chakula, amlipie ada mtoto na kwa kadri siku zinavyoendelea muongezee majukumu ya ndani kwa kufanya hivyo utakuwa unarudisha jasho lako kidogo kidogo.
Anyway. Nimekuta anachat na wanaume wawili tofauti, akiwatumia na picha kuonyesha mwili wake.
Biashara alianzisha nikiwa safarini, mawasiliano huvunjika pale anaposhindwa kutoa accounting ya pesa, nimeishamkaliza zaidi ya mara mia moja, mpaka nimempleka nje ya nchi kupumzika, na huko nikalianzisha, in a friendly and lovely manner, kwamba pesa zinatumika vipi, biashara fulani inaendeleaje, imekufakufaje, nikakuta baadhi ya partiners ni family members wake, kwa pesa alizokili watu wamekataa kumlipa ama kwa kutokuonekana au kwa kudai hawana nikamuomba anipe details zao za kutosha ili niwachukulie hatua za kisheria hata kwa ubabe sababu i have networks hakutoa ushirikiano mpaka leo.
Leo jioni naondoka moshi (nyumbani kwao), kakataa kwenda Mwanza kwamba atakuja baada ya mwaka mpya, bado hili sio tatizo sababu as long as atakuja na anabaki kwa wazazi wake natambua damu ni nzito, sio issue.
bado hapo ninatatizo la mawasiliano?
Mkuu ninadhani, kuna shida katika
1.Mawasiliano.
Ninadhani kama mngekuwa mnawasiliana, kwa ukaribu, haya yasingefika huku.
2. Ufuatiliaji.
Kama ulimpatia jukumu la kusimamia ujenzi wa nyumba, ingekuwa vyema kama ingekuwa ndani ya muda fulani, mf. kutokana na uwepo/upatikanaji wa pesa, kuweka malengo kuwa ni lini ujenzi unategemewa kukamilika, mfano baada ya miezi mitatu(kwa kuwa ilikuwa imefika sehemu nzuri), na tuseme labda baada ya mwezi mmoja kuweka umeme n.k.
Hii ingemfanya asimamie kwa karibu, ili kukamilisha lengo na pili ingefanya kuomba ushauri anapokwama mf. toka kwako(na kuwafanya mwe karibu zaidi).
3. Utafutaji.
Mkuu sina nia mbaya ila wakati fulani mambo haya kwa upande mwingine yanategemea uelewa (elimu).Ni ngumu sana kwa mtu asiyetafuta pesa kupewa jukumu la kusimamia jambo akalikamilisha (kwa kuwa kwa gharama anazoambiwa anaweza akakubaliana nazo kirahisi, kwa kuwa si yeye anayetafuta)..ingekuwa ni vyema kwa mtu kama huyo kuwa na chanzo gulani cha pato, ambacho kwacho anaweza kupata pesa ya kusimamia jambo jingine.
4. Matumizi.
Watu hubadilika, sisemi ndivyo mkeo alivyo, lakini nonasema kuna baadhi ya wanawake wenye kuonyesha umakini mkubwa kabla ya ndoa na baadae kuwa na mtazamo tofauti, hasa kutokana na marafiki kubadilika, kutaka kuonyesha hali tofauti kabla na baada ya ndoa! Kwa kuwa unasema hafanyi kazi yeyote, hebu katika pesa inayokuja asipate hata kidogo, kuonyesha uhitaji wako kwa sasa (simaanishi umfiche bali umweleze kwa nia njema tu, pili umfanye awe na rekodi ya matumizi (kiasi cha pesa kilichopokelewa na mchanganuo wa matumizi yake angalau kwa mwezi kama si kwa wiki.
Unanicheka??
Sijakucheka kakangu, sana sana nakuonea huruma kukutana na type ya ufoo, nimeshangaa na kusikitika kuona mkeo anatuma picha kwa wanaume wawili tofauti
Nakubali kosa langu, lakini pesa nilizokuwa nampa kwanza alinieleza anakusanya ili akianza kujenga ajenge amalize mara moja, kisha ghafla akaziweka kwenye biashara (by then nikiwa nje ya nchi kwa kama miezi miwili nimerudi na kukuta tayari yuko busy vibaya sana na biashara), sikuweza kumzua abruptly sababu tayari pesa zingine ziko mikononi mwa watu nakadharka.
Pili, siwezi kukaa na mwanamke nisiyemuamini, na hata napofikiria kumuacha, ni kwa sababu baada ya kuacha kumshirikisha kwenye mambo ya pesa, mahusiano yetu yamehabika sana, sio kwa upande wake tu, ila hata mimi, kwa nini nisiweze kumuamini mke wangu??
Mmmh! Ndoa ngumu aisee,sasa hapo ndugu unamtuhumu mkeo kwamba anafuja pesa that means hana malengo ya kifamilia naww je mna watoto kwamba angeweza kufikiria future ya watoto? halfu umesema baadhi ya business parterners ni upande wa familia yake ulipomuuliza kuhusu hilo alisemaje? kwa mtazamo wangu huyo mwanamke kuna makubwa anayafanya ambayo huyafahamu na anaweza kuwa anafanya na ndugu zake,Haiwezekani mwanamke aliyeolewa akafanya maamuzi bila kumshirikisha mumewe hata kama yuko mbali angefanya hata mawasiliano ya simu,kwanini aamue yeye kama yeye kuzungusha pesa wakti ww umempa maagizo ya kumalizia nyumba? na inakuwaje unapomuuliza ili ujue ukweli anakuwa mkali lazima kuna udanganyifu hapo, fuatilia vizuri ujue pesa zinaenda wapi maana muda mwingine hawa ndugu zetu huwa wanakuwa na tamaa iliyokithiri yuko katka mazingira mazuri anapewa kila anachotaka sasa sijui nini shida
Kwa hali hiyo unaweza ukakuta mtu anajinyonga halafu tukamcheka na kumzodoa lakini kwenye ndoa kama hamna ushirikiano,mmoja anafanya kwa ajiri ya wote mwingine anafanya kwa ajiri yake mwenyewe ndoa huwa inakuwa ngumu kweliu a very ryt
huyo mwanamke kuna bness anafanya na ndugu zake ndo maana anakuwa mkali unapomuuliza
pole mkuu
Kwa hali hiyo unaweza ukakuta mtu anajinyonga halafu tukamcheka na kumzodoa lakini kwenye ndoa kama hamna ushirikiano,mmoja anafanya kwa ajiri ya wote mwingine anafanya kwa ajiri yake mwenyewe ndoa huwa inakuwa ngumu kweli
Bro nashauri tena,huyu mke hakufai.Kama afya yako haijali anajali gari,utakufa bure achana nae mrudishe kwao.Huyo ni mmachame nn? Kaka huyo atakuua ili yeye aendelee kumliki mali funguka tua mzgo huo haraka sana.Vp hajakutarfu kwamba ashaona uzi huu?
Bado dada angu, lakini sasa nafikiria kuliwasilisha kwa mwanasheria.
sangarara za kuambiwa changanya na zako.
huyo sio mwanamke alikuwa anatafuta ndoa na amewin
bt nakwambia nenda kanisani na kwa mwanasheria vunja hyo ndoa kuanza upya c ujinga
huyo c o mwanamke utakufa kabla ya wakati wako