Naomba ushauri jamani

alichokiunganisha MUNGU mwanadamu asikitenganishe so mwombe MUNGU sana atakusaidia "kamwe MUNGU hawez kukuacha bila msaada"
 
ndugu pole sana...hichi kisa kinasikitisha kiukweli....ushauri wangu ni kwamba kwa sasa fanya mambo yako wewe kama ww...yaani ingefaa ujipange upya bila kumtegemea coz kwa hali nilivyoielewa hatajenga hiyo nyumba bali huenda ana mipango yake.

ukifanikiwa kutimiza malengo yako ndipo utakapoelewa majibu ya maswali mengi uliyonayo...

nakutakia afya njema na mafanikio.
 
Kwa ushauri wangu mngepeana nafas kidogo,yan umrudshe kwao kwa mda hata 4mnths huku ujpanga kufanya mambo yako yakae sawa.Kwa sasa sidhan kwamba kutakuwa na suluhsho ambalo litaweza kuondoa uchungu ulioko nao sasa akiwa bado yupo ndani.Mrudshe kwao kwa mda ila n vzr asjue ni kwa mda,alafu ufanye mambo yako kwa uhuru.Pole sana kaka.
 
Pole sana , tatizo hapo ni wewe kushindwa kusimama kama mwanaume ndani na kusimamia maendeleo ya familia. Siku zote unapoingia kwenye mahusiano au ndoa usiweke dhana ya kuona furan ni sahihi kwa kila jambo. Ulitakiwa masuala ya maendeleo usimamie wqewe kwa vile unaujua mwenendo halisi yeye alitakiwa afuate maagizo. Lkn pia ulimpenda sana kiasi ukamwachia mamlaka yote kiasi akakupanda kichwan hasa suala la maamuzi
 
Nadhani ukichwa wa familia ni uwezo wa kutafuta pesa, huo uwezo ninao mkubwa sana na unaongezeka kila siku,
kwa bandiko lako hili, nimeweza "kukuona" na kukufahamu!, ni vyema ku accumulate mali kwa haki kama ufanyavo, lakini si sahihi hata kidogo kuiachia pesa isimame ktk nafasi yako kama baba wa familia! rudi usimame kny nafasi yako uiongoze familia yako na siyo kuachia pesa iongoze. Mkeo usimwache labda kwa uzinzi tu,
 
unaweza kuendesha biashara ila ukashindwa kuendesha familia...sometimes moneys isn't everything...
 
ndio maana huko kukaya wanaogopaga wakiona kijana ameoa mkoa huo uliooa wewe... japo huwa sikubaliani nao, lkn....

back 2 the topic, huyo hana sifa ya kuwa mke. kuna wanawake wanagangamala wenyewe kwa ajili ya families zao hawajui hata 1% ya mishahara ya waume zao ikoje. sasa yeye 80% ya salary anapata, na mihela mingine anailalia ndani halafu bado hawezi kufanya kitu chochote.

huyo mwanamke ni limbukeni na mshamba (amepita hata vidato vile vinne?). kwa nini akae na 5M ndani atembee na 2M kwenye gari wkt banks na mitandao ya simu ipo.

simama kama mwanaume, ndani ya nyumba. umesema baba yako alikuwa akimpa mama yako hela yote. unasahau kwamba unapoanza maisha ya ndoa unaenda kuishi ndoa yako na si ndoa za watu wengine. hakuna formula kwenye marriage life, don't copy your parents life style, tengeneza ya kwako
natamani nikwambie umrudishe kwao hata kwa miezi mi3 akapate kitchen party mara ya pili
 

Ni majanga.
 
Pole sana mkuu @Sangarara kutokana na maelezo uliyoweka inaonyesha fika kuwa kwenye ndoa yako kuna tatizo kubwa.

  • Uaminifu kwenye pesa: hili ni tatizo kubwa sana hasa mwanandoa mmoja anapokua sio muwazi kwenye matumizi yake na namna anavyopata pesa kwani inajenga hisia hasi.
  • Kushindwa kwa mke kusimamia mambo ya msingi kama vile ujenzi hii ni shida
  • Mashaka juu ya uaminifu wake kwenye ndoa mara baada ya kubamba picha akituma kwa wanaume na kufanya mawasiliano na hao wanaume . Mkuu kwangu mimi hili ndio naliona kuwa ni tatizo kubwa na pengine ndilo linalochangia yote yanayoendelea kwenye ndoa yenu. Halafu mwanamke kukataa kwenda na wewe kwenu kisa abaki moshi na wazazi wake atakufuata baadae mmmh hii nayo ni shida mkuu.

Ushauri wangu fanya uchunguzi ujue hizo pesa zinapelekwa wapi na jitahidi ujue uhusiano wake na hao aliowatumia picha . Uchunguzi huu utakusaidia kupata ushahidi au vielelezo vya kutosha ktk kufanya maamuzi magumu. Si ajabu mwenzio kesha jenga na ana mpango wa kuolewa au kuishi peke yake na hivi anajua afya yako imeanza mgogoro be careful.
 
Tatizo la hawa kaka zetu ni kusema "sawa do, ndoho mhayo" inawaumiza sana.
 
Pole ndugu,pesa anazo na akimaliza mipango yake anakumaliza.muombe Mungu akunusuru
 
Dah..I feel so sad about this, you sound so frustrated, kama unaamin maandiko basi soma zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea, nitakushauri, jicho langu likikutizama", Muombe Mungu huwezi amini atakupa amani na jinsi ya kusimama tena na kukuondolea maumivu, usiweke imani sana katika uwezo wako ulionao.

Pia, Unaonekana umekulia familia yenye furaha sana na amani ukajifunza kitu kwa baba yako ukatamani utumie mfumo huohuo kwenye ndoa yako, and it has failed terribly..hukua na nia mbaya..na wala mkeo hakua na nia mbaya nadhani hakuwahi kushika pesa kama ile sasa alipoiona kwa nia njema na ile tabia yake ya kupenda kutafta akajenga picha kichwani ya jinsi akifanya ile biashara mtaendelea zaidi..na njiani of course vikaingia vitabia vya kiburi (humjui mtu mpaka amiliki pesa) na pia management ya pesa ikamshinda na labda watu wakaanza kutake advantage of her etc etc..alikua na tabia nzuri, all she needed was your strict management and guidance..haimaniishi eti ukiwa unamuongoza basi humpendi au yeye hafanyi nafasi yake..noooo..kwa sisi wanafunzi..tunajua kua tupo aina nyingi..kuna wanafunzi wanafanya vizuri bila supervision, yaani ni very independent na anakuletea product nzuri, ila kuna wale lazima umcheki kila wakati, umhimize, umchallenge, na yeye anafanya vizuri kwa mazingira hayo..hapo hamna mbaya wapo tu tofauti

Mungu akusaidie/awasaidie sana maana kuachana sio suluhisho, pia huyo mkeo anahitaji apate wakati mgum kiaina..yaani mda wa kujutia..afunguke macho..kama akiweza kujirudi itasaidia sana, ila kama hatayaona makosa yake..mmmhhh..Mimi na mpenzi wangu tumefanya vitu vingi sana vya maendeleo pamoja na hua ananiamin sana hata bado hatujaoana najua ana sh ngapi na pesa za savings amehamishia zote kwenye account yangu ili kwa urahisi wa mambo yetu, kabaki na mshahara wake tu ndo unaingia kwake, yaani yuko kama wewe kabisaaa..sasa hua nawaza yaani tukioana tutafika mbali sana..sasa nimesoma hapa nimesikitika sana, naomba Mungu mpate mlango wa kutokea.
 
Pole Mkuu,i hope things will get better!Sina experience na ndoa,sina cha kukushauri wengi wamejaribu kutoa Ushauri!just do what is best for you and maybe her.
 
Full kuchanganyikiwa hata kueleza tatizo shida....,au ndo visa visivyoelezeka mpaka kuona?
 
Haiwezekani wewe uwe una tatizo la kiafya badala ya mkeo aende na wewe mza mfikilie jinsi gani mpate pesa za matibabu yako yeye anasema anabaki kwao.

je yy ni mke wa nani?ina maana hana uchungu na wewe sasa na ndio maana ata anasita kuuza gari yake kwa sababu ya kutibiwa wewe.

Hakuna kitu muhimu kama afya yako kwanza.
Mwisho akili ku mkichwa mkeo hawezi kutumia mipicha ya utupu wanaume wengine kama hana mahusiano nao ya kingono.
Cha msingi fight utibiwe kwa pesa zako tu manake huyu mkeo inaonekana anasubiri uhumie (ufe) ili abaki anatanua na pesa ulizompatia mwenyewe.
 

NINGEWEZA KUKUPA POLE LAKINI HAINAMAANA MAANA WEWE NISHUJAA NISEME HONGERA,Baadayakusema hayo nakwambia hivi kaa sehem isiwe kwenyekiti chinikabisa turia ,utapatajibu la kimungu, achana nakaurimbiu alichokiunganisha. mungu,Yesu wakati saa yakuteswaimekaribia alisema iki"wezekana kikombehiki kiniepuke.kwahiyo wewe amuwa kusuka au kunyowa. onyo usimuwazie kufa. afya yako kwasasa unaendereaje ?? ---
 
Mkuu kwanza ninakupa pole Sana narudia tena pole Sana nimesoma kwa makini story yako huku mapigo ya moyo yakiongezeka kwa kasi Sana Kana kwamba ni Mimi yamenikuta!! Narudia tena pole Sana na nimesoma vizuri komenti za wachangiaji wengi wanaona kwamba hukua na mawasiliano ya moja kwa moja,! Kitu Kimoja ambacho kimekuponza ni uaminifu mkubwa Sana kwa mkeo na mkeo ameshakupima akagundua udhaifu wako Ndio maana yote hayo yanatokea! Unaogopa kelele zake na Ndio maana ukimkalisha Hakuna unachopata!! Swala langu ni moja tu MKUU KUANZA UPYA SI UJINGA UMEOA PEPO! Alijifanya mwema kwako wakati wa uchumba kukudhibiti matumizi ili uone huyu anafaa kumbe sio! Baada ya kuingia kwenye ndoa akua mmiliki sasa anafanya hata ambacho hukifanyi! Na kutokana na matendo yake machafu anajua na wewe unaweza fanya Ndio maana ukiwa hata na rafiki zako anakua mkali!! Tokea umemuoa maisha na uchumi unashuka sasa huyo mtu wa nini La mwisho ambalo Kama ni Mimi navunja ndoa siku ya harusi ni kutuma picha za utupu wake kwa wanaume wawili tofauti mkuu nikuulize swali mkeo ulimuolea Mahari milioni Mia sasa unazionea uchungu?!! Mzee ungekua bro wangu mie tungepigana Kama unaendelea kukaa na hilo jini nasikia uchungu Sana yaani!!
 
Kwavile umesema atapita hapa na atajua unamzungumzia yeye basi ngoja nisubiri apite ajibu kwanza tuhuma kama wanasaiasa then nitawashauri kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…