Wazo lako ni zuri,
Mimi nitakushauri kwa namna hii.
Kwa hio laki tano yako,ni rahisi kuipandisha ukijitoa wewe mwenyewe na sio kutegemea mtu/watu.
Laki mbili unusu inafaa kuwekeza katika ufugaji wa Kuku wa kienyeji.
Nunua kuku ishirini na tano,makoo(20) jogoo(5)Kwa bei ya shilingi 10,000.
Hakikisha kuku wako unawanunua maeneo mbali na mji na usinunue kuku wa kufuga Sokoni,
Na hao kuku akikisha ni kuku wakubwa yaani ukikaa nao muda kidogo wataanza kutaga,
Na usimamizi wa kuku wa kienyeji hauna gharama kama kuku wa kisasa.