Naomba ushauli,kati ya kulima na kufuga

JACKBIZZO

Member
Jul 11, 2013
83
12
wana jf naomba mawazo yenu nina laki tano najikanganya kati ya kufuga kuku wa kienyeji na kulima viazi mviringo, au ninunue shamba nipande miti. nashindwa kuchagua,msaada wenu ni muhim sana tafadhali.
 
Inategemea unataka faida ya haraka au baada ya miaka? Soma kuhusu miti humu faida ya misitu mingi kuanzia miaka 10-50, lakini kuna miembe na matunda mengine miaka 2 nk. Kuku kienyeji miezi sita unaanza kuuza mayai au kuku wenyewe. Ufugaji kuku ukiwatengea eneo waweza kulima sehemu iliyobaki. Labda ungekuwa wazi zaidi kuku ufugie ulipo, shamba ununue mbali?
 
Kama unataka faida ya muda mfupi fuga wa kisasa kama banda unalo hiyo hela yaweza tosha kuanza na kuku 100. Batch utakapouza hao utaongeza, kuuza kuanzia wiki 6 chunguza soko kama lipo
nahitaji faida ya haraka kama miezi kadhaa
 
Wazo lako ni zuri,
Mimi nitakushauri kwa namna hii.
Kwa hio laki tano yako,ni rahisi kuipandisha ukijitoa wewe mwenyewe na sio kutegemea mtu/watu.
Laki mbili unusu inafaa kuwekeza katika ufugaji wa Kuku wa kienyeji.
Nunua kuku ishirini na tano,makoo(20) jogoo(5)Kwa bei ya shilingi 10,000.
Hakikisha kuku wako unawanunua maeneo mbali na mji na usinunue kuku wa kufuga Sokoni,
Na hao kuku akikisha ni kuku wakubwa yaani ukikaa nao muda kidogo wataanza kutaga,
Na usimamizi wa kuku wa kienyeji hauna gharama kama kuku wa kisasa.
 
Kwa laki tano naona ulime tu. Nyanya, mboga mboga, vitunguu, pilipili, n.k... pesa utaiona tu haraka. Kufuga lazima uwe na pesa ndefu.

Sent from my SM-N900 using Tapatalk
 
Hili wazo zuri sana ila kasema anahitaji hela ktk miezi kadhaa na kuku kienyeji wana faida nziuri ila utaiona kuanzia miezi sita kuendelea, kama anaweza kufika muda huo afanye hii.
Wazo lako ni zuri,
Mimi nitakushauri kwa namna hii.
Kwa hio laki tano yako,ni rahisi kuipandisha ukijitoa wewe mwenyewe na sio kutegemea mtu/watu.
Laki mbili unusu inafaa kuwekeza katika ufugaji wa Kuku wa kienyeji.
Nunua kuku ishirini na tano,makoo(20) jogoo(5)Kwa bei ya shilingi 10,000.
Hakikisha kuku wako unawanunua maeneo mbali na mji na usinunue kuku wa kufuga Sokoni,
Na hao kuku akikisha ni kuku wakubwa yaani ukikaa nao muda kidogo wataanza kutaga,
Na usimamizi wa kuku wa kienyeji hauna gharama kama kuku wa kisasa.
 
wana jf naomba mawazo yenu nina laki tano najikanganya kati ya kufuga kuku wa kienyeji na kulima viazi mviringo, au ninunue shamba nipande miti. nashindwa kuchagua,msaada wenu ni muhim sana tafadhali.

Mkuu nakushauri ni kheri ufugaji, kilimo kwa sasa ni kigumu sana. Tanzania mvua zimekuwa ni za kubahatisha sana, nimkheri ufugaji, juhudi zako ndio mafanikio yako. Kilimo kigumu sana, risk yake ni kubwa
 
Kilimo sio2 MVUA anaweza kufanya umwagiliaji lkn DAWA za kuua wadudu zitamtesa manake KILIMO cha kiangazi wadudu wanakula sana Mazao kwahiyo laki 5 yake Afuge2!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom