Naomba upite hapa, natafuta kazi

Naomba upite hapa, natafuta kazi

Nasakadoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
343
Reaction score
169
REPOST:

Sina Elimu ya Juu saana, lakini naweza kufanya kazi mojawapo kati ya hizi:

√-Marketing
√-Project/Firm Managements(naweza kusimamia miradi mbali mbali kama Restaurant,Bar&Pub,Ranch,Duka la aina yoyote,n.k.)
√-Udreva (hapa nina leseni nilipata mwaka 2013 yenye daraja A,B,D&E). Naweza kuendesha magari ya mashirika,kampuni,mtu binafsi kama kumpeleka kazini na some occationals, e.t.c
√-Kuuza Duka,Stationary, n.k.

Nomba kama kwenye Kampuni/Asasi uliyopo wewe msomaji kuna kitengo mojawapo kati ya hivyo, please kuwa msaada kwangu! Sina kazi kwa sasa… 

Unaweza kuwa wewe binafsi unatafuta mtu wa kukufanyia kazi kwenye mojawapo ya hizo kada au akawa jirani yako, ndugu, jamaa, n.k. Naomba unisaidie kupata kazi.

Ndugu, mimi naishi Dsm, maeneo ya Mbezi ya Kimara ,jinsia yangu ni Me miaka 26 sasa. Nipo tayari kufanya kazi eneo lolote, mkoa wowote muda wowote halali.

Nitashukuru saana kama nitafanikiwa kupitia wewe.
UBARIKIWE SAANA.

+255 718 651 174
WhatsApp and Normal Calling&Sms.
 
sasa mwanangu kuna pori liko
mzenga kuna miti ya kutosha na maji pia
kama vp tufanye project ya mkaa na kuni
kitakachopatikana tugawane.
 
nzalendo… mimi sina tatizo,ni kuelewana tu! Kazi ni kazi mradi ilipe! Kama uko dar namba ndo hiyo tuwasiliane hata kama haupo dar
 
Last edited by a moderator:
Uzi wako umenigusaaa...hope utapata wa kukusaidia usijalii, wapo watu wanatafuta watu walio serious, hope one day yes!

Mwenyewe nasota kuzisakaa hizi kazi...ila naimani ipo siku, Mungu hamtupi mja wake. Nikushauri kitu kama unaweza hata hizi kazi za maloader, zunguka kwenye magodown ya mashirika ya bia kama Serengeti na Kilimanjaro waweza kupata...koz wanahitaji vijana wanaoweza kubeba crates.

kama uko fit unapiga mzigo na unapata hela yako kihalali. Ila usiache kuomba kazi, ujue its better ukaomba ukakosa kuliko kukaa ukakata tamaa..hii ni mbaya sana.

Kuna mtu alishawahi kuniambia, mtu aliesoma na ambae hajasoma ni sawa na abiria wawili walioko stand wanasubiri gari, mmoja ana tiketi mkononi mwingine hana...japo hawajui usafiri utakuja lini ila wa tiketi ana uwezekano mkubwa wa kusafiri kuliko ambae hana.

So katika maisha never give up hats siku moja...u never know the moment unakata tamaa mangapi yanakuja on your way! Yote mema..mshukuru Mungu kwa kila jambo.
 
Utapata mkuu lakini umesema umesoma Financial management ulisoma ngazi ya Cheti, Diploma au Seminar?
 
Dah Uandishi Wako Mzuri Sana Mkuu,Usijali Wapo Walioguswa Na Hitaji Lako I Hope Watakusaidia Mkuu
 
EE mola wetu mwenye huruma mtazame kijana wako kwa jicho la huruma, hajataka kuiba ila ameomba ajira halali apate riziki halali... n wewe tu 1 na huna mshirika, hujazaliwa na wala huna mtoto. Al rawf , al kareem al razzak
 
Asee umenitach kwa kweli. Mungu atajaalia utafanikiwa mdau.
 
Dah nimependa uandishi wako mkuu,hakika utafanikiwa kupata kazi.
 
Dah Uandishi Wako Mzuri Sana Mkuu,Usijali Wapo Walioguswa Na Hitaji Lako I Hope Watakusaidia Mkuu

ni kweli mkuu kwa hii age group ya 20's ya Watanzaia wa leo ni mara chache kumpata mtu anayeweza kuandika akaeleweka vizuri kama mkuu Nasakadoo. i'm convinced jamaa yupo vizuri "upstairs", nafikiri huyu si wale wa "xaxa"
 
Last edited by a moderator:
EE mola wetu mwenye huruma mtazame kijana wako kwa jicho la huruma, hajataka kuiba ila ameomba ajira halali apate riziki halali... n wewe tu 1 na huna mshirika, hujazaliwa na wala huna mtoto. Al rawf , al kareem al razzak

Dah, sawa mkuu.
 
Mkuu kuna kitu nimekukwaza ? ni yeye mmoja 1 tu ndio mtoaji wa rizk.. wengine ni sababu tu..hana mshirika hajazaa wala kuzaliwa

ndiyo mkuu, anyway si mahala pake. Tumsaidie Nasakadoo apate ahueni ya maisha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom