Naomba upite hapa, natafuta kazi

Naomba upite hapa, natafuta kazi

Pole sana ndugu yangu, nakupa tu wazo mkuu ulifanyie kazi, Kampuni ya Sukari Kilombero Kwa sasa wamefunga msimu wa uzalishaji. Watafungua msimu ujao May mwaka huu na wataanza kuajiri wafanyakazi sekta mbalimbali ikiwa pamoja na madereva. Kama una ndugu, jamaa au rafiki aliyeko Kilombero fika pale ukaanze kupeleka maombi yako. Pia kuna Kampuni ina tenda ya kufanya kazi za mashamba ya miwa UNITRANS kajaribu bahati mkuu. Mimi Siwezi kukuunganisha moja kwa moja, ila ukipm ntakupa majina ya watu pale watakaoweza kukusaidia.
 
Bado... watu wanaishia PM then hakuna mwendelezo! Msaada jamani? Mnataka Nifanyeje kijana wenu?
 
Bado... watu wanaishia PM then hakuna mwendelezo! Msaada jamani? Mnataka nijinyonge kijana wenu?

Hapa sasa unaanza kuharibu , kuwa mvumilivu. Hakuna kizuri kinachokuja kirahisi

Kama Mungu amepanga upate msaada Hapa ni lazima tu utapata hakuna wa kuzuia but manung'uniko yasiyo ya msingi yatakushushia credit ulizopata huko juu kwa uandishi na hekima ulizotumia

Mungu akufanyie wepesi kwenge za ya moyo wako .
 
Bado... watu wanaishia PM then hakuna mwendelezo! Msaada jamani? Mnataka nijinyonge kijana wenu?

Umeanza vizuri lakini sasa unaharibu!

Kujinyonga? ili iweje? na kama ukijinyonga utakua umemkomoa nani?

Mtu makini atakupuuza mara moja baada ya kusoma maneno haya!
 
Umeona ndo la maana sana hlo?.. pita hivi dada yangu...

wewe ndio umeona la maana, do u think kila anayepita hapa ana kazi hadi utangaze kutaka kujinyonga??? Unadhani unamtishia nani? Zaidi unatia mashaka kwamba hata kazi utakayopata ikipitia kipindi kigumu utajitoa au ndio utajinyonga? Mtoto wa kiume hachagui kazi ila wewe inaonekana za ofisini kwako ndio kazi, endelea kusubiri huruma kwa kutishia kujinyonga
 
Mkuu mwanzisha uzi...nilienda last week kwenye ofice za lake oil kibaha, eneo la shel, nilipeleka application zangu, bt wenyewe wakasema kwa sasa wanapokea maombi ya udereva tuu...so jaribu kupeleka pale...kama uko free peleka kuanzia jumatatu...Mungu akutangulie mkuu
 
Back
Top Bottom