Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Hutegemei kuziuza?
AKIJA MTEJA MZURI NAUZA, NAUZA KWA MILIONI 7 ZOTE KWA PAMOJA, ALAFU NI FURSA NZURI SANA KWA KUHIFADHIA VITUNGUU, YAANI KUNA ILE MIEZI WANAVUNA VINGI THEN UKAHIFADHI KWENYE CAGE ZILE UKAPIGA PESA KIPINDI CHA UHABA WA VITUNGUU MWEZNI WA NNE,TANO NA SITA MWANZONI
 
Fanya kununua mazao msimu wa mavuno kama mahindi, mpunga ,vutunguu na kuleta sokoni. Una angalia bei ikoje sokoni halafu unajumua shamba unaleta dar .
 
Fanya kununua mazao msimu wa mavuno kama mahindi, mpunga ,vutunguu na kuleta sokoni. Una angalia bei ikoje sokoni halafu unajumua shamba unaleta dar .
Asante sana mkuu kwa ushauri,ila naona uletaji mazao mjini inahitaji kidogo uwe na godown in case hujapata mteja wa kununua
 
Laki 3 kwa sasa haitakufikisha sehemu boss, kama ungekuwa na vifaa say feeders, drinkers nk ungeweza kuanza na japo broilers 50. Napo faida itakua kiduchu sana
nikitaka kupata faida nzuri kidogo, nianze na mtaji kiasii gani?
 
Nimekuelewa hapa acha tu..
 
Kwanza pole sana

Mkuu kilicho kuangusha ni soko, ulianza miradi bila kuwa na soko la uhakika.

Wengi huwa tunafeli hapo na hata hizi taarifa tunazopeana kwenye mitandao kuhusu ufagaji na kilimo utakuta tuna ongelea zaidi gharama na faida lakini Mara chache mno watu wataongelea soko kwa undani.

Rudi tena kwenye miradi mkuu Ila Safari hii anza kwanza kulijua soko vizuri la kitunguu na kuku. Uzuri mkuu Ontario kajitolea kuunganisha watu na soko la uhakika la kuku.

Kingine kwenye kilimo jifunze ni wakati gani soko linakuwa limejaa zao husika kwa maana wakulima wengi wanakuwa wanavuna na wakati gani zao linakuwa halipatikani kwahiyo wewe hakikisha unalima ili uvune kipindi ambacho zao husika (kitunguu) halipo kwa wingi sokoni. Ila hapa nitoe angalizo, Mara nyingi kulima ili uje kuvuna kipindi ambacho kitunguu kipo kichache sokoni huwa kuna Changamoto sababu Mara nyingi huwa ni msimu ambao Hali ya hewa hairuhusu kitunguu kustawi Kama wewe ulivyo kumbwa na ukungu Ina maana ulilima kipindi ambacho sio favorable kwa kitunguu, kwahiyo kipindi hili inabidi uwe na uangalizi wa Hali ya juu mnoo, ukifanikiwa kuvuna hata gunia 60 kwa ekari kipindi hiki umetusua


Kila la kheri

Aluta continua
Mapambano yanaendelea
 
Hongera kwa mafanikio mkuu ONTARIO nilikuwa na uliza kama ulishawah kufanya kilimo cha greenhouse na experience yako ikoje katika ulimaji wa mboga mboga!
 

Mkuu naomba kupata taarifa hasa vibali na namna ya kupitisha mzigo boarder na connection za kuuza kitunguu huko kenya.
 
Asante mkuu kwa ushauri wako
 
Alishakataa hiyo kitu! Ukipitia comments za mwanzo kuna Jamaa aliomba hiyo formula!
Mwenyewe natamani hata akipatikana mtu wa uhakika nimlipe anifundishe

Mimi niko kwenye hii biashara ya kuku wa nyama na kweli vile vyakula vya makampuni bei imekua mbaya sana. Nina formula tatu mpaka saiv ambazo zote nimeanza kuzifanyia majaribio. Nimelipia kuzitengeneza na zinanipa majibu tofauti tofauti. Hii ya mwisho majibu ntayapata mwez July mapema. Naanza kuwalisha weekend hii.

Ikikamilika nitawapatieni hio formula hata kwa kuchangia kidogo.
Ila mpaka sasa hivi mfuko wa dukani ni 70,000 na mimi ninapochanganya natumia 50,000
 


Mkuu kwenye hio ya kuku wa nyama naweza kukusaidia. Biashara yake tatizo inahitaji connection kupata masoko. Fahamiana na wafugaji wengine. Mimi nna mwaka mmoja toka nianze nilianza na kuku 100 sasa hivi wako 600.

Tulichofanya sisi ni kushikilia masoko na tunakua tunapokezana kuagiza vifaranga kwa interval ukiwa na soko la kuku100 kila siku manaake ni kwamba mimi kuku wangu ndani ya siku 34wanakua wameisha wakati huo mtu mwingine anakamatia lile soko mi naagiza vifaranga(mwanzoni nilikua naona aibu hata kwenda kwenye vile vikao lwakua ni wamama tu ) ila nilipofanikiwa kuingia katika hio club raha msatarehe.

Nilipojaribu mara ya kwanza ilibaki kidogo wanidodee na mimi nilikaa nao hadi wiki 7 na wanaendelea kula tu. Nusura niache ila nikarudia pamoja na kuzunguka zunguka kupata masoko mambo mazuri.

Kwa maana hiyo kama mimi binafsi ningekua na mtaji nina uwezo wa kutoa kuku 100 kila siku(Faida ni zaid ya 150,000) na ukiwa na kuku wa kila umri manaake uweze kuchinja kuku 3000 kwa mwezi fikiria faida yake.

Ishu inakuwaga pale unapouza ukimaliza uanze kukuza upya ukirud soko limekabwa na wengine na ni muda wa kutoa kuku....hapo ndo nilikua natembea naongea peke yangu kama chizi. Huku nilipo tunauza 7000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…