Naomba uniulize chochote kuhusu kufanikiwa katika Biashara na Ujasiriamali

Ontario jamani hapo kwenye mifuko hapo ndio nachanganyikiwa kabisa embu niambie nawapa hadi mifuko 37 kwa kuku 500 ndio maana sioni faida kabisa
Kwenye ufugaji wa kuku kuna kitu kinaitwa Conceptual Framework hii inatumika sana kwenye ufugaji kuku la sivyo hutaona kitu.
 
daaah we dogo saafi saaana aisee nikija bongo nitakutfta mdogo wangu. Mimi nilikuwa na na nina experience saaana na vitunguu maji kwa miaka kama kumi hivi nimelima kitaaalam saana ila tatzo niligundua kuwa soko linazngua saaana saaana hapo bongo. ilifikia hatua nikaachaga kulima nikaenda kuwa dalali wa vitunguu huko mabibo hii yote ilikuwa ni mbinu ya kufanya research ya masoko ya vitunguu nilikaa miez minne nikaelewa saaana na baada ya hapo nilirudi shambani nikawa nalima kinyume na msimu. Hapo nilipata faida saaana. kuna kipind nilitembelea israel nikaona vitunguu swaum so nikapanga nikarud tz nikamwambia kakaangu tulime vitunguu swaum lakini jamaa akakataa akasema vinakubali maeneo ya baridi. wakat israel niliona vinalimwa open space jamani. sikukubaliana nae. nikajipanga nikalima ka shamba kangu ka nusu hekari nikatumia utaalamu waangu woote wa zao la kitunguu maji na nilisoma na nikaenda kuwatembelea baadhi ya wakulima huko mbeya nikajifunza nikaja kufanya kwa practical aisee amini usiamni kaka nilipiga gunia zangu kadhaa za vitunguu swaum tangu hapo nikawa mkulima mzuri saana wa vitunguu aisee. kwa hyo jamani msisikilize ya watu mimi home tz nalima had zabibu. kilimo kinalipa ila KILIMO AFRIKA BILA KUJUA SOKO NI SAWA NA KUPAKA RANGI UPEPO. Zaid ya Mbwa wa ulinzi wa kipolisi/kijeshi, mbuzi, bata mzinga na ng'ombe wa maziwa sijawah fuga. Mimi nimejifunza kuwa specific ktk jambo unalofanya. yaani amua nini unataka kufanya na ujikite huko. mimi nilijikita ktk vitunguu na hapo hunidanganyi lolote may be masoko ya nje ndio sijawah uzia huko na hapo ontario mdogo wangu utanisaidia nikija bongo. Nalima mbaazi, mpunga na ninasaga nyama na kutengeneza sausage pia na mikate. kwa hyo naenjoy, NIMESOMA FINANCIAL ENGINEERING lakin moyo wangu uko kwenye kilimo jamani. i miss home nikija nitakutfta mdogo wangu. nikusaidie forex (japo nimesimama kidogo).
Mkuu naomba kujua zaidi inachukua mda gani vitunguu maji kwanzia kulima mpaka kuvuna,na changamoto zake hasa magonjwa..kwa ufupi tu..pole kwa usumbufu
 
Hongera sana ONTARIO,

Swali langu la kwanza:
Ni wakati gani hasa ulipoamua kuachana na kununua chakula kwa ajili ya kuku wako wa broiler. Hapa naomba utueleze kwa ukubwa wa project ilipofikia. Ulifuata hatua gani mpaka kufanikiwa na changamoto zake ni zipi?

Swali la Pili:
Uliwezaje kwa mara ya kwanza kufanya biashara ya export maana nimeona uliexport vitunguu. Ulipataje Masoko, process za kuexport mpaka kufikisha mzigo. Tueleze na changamoto zake pia

Swali la tatu:
Nimeona umefanya packaging za kuku. Una process mwenyewe kuku wako wote?

Nisaidie kujibu, niendelee na maswali mpaka tuelewane mkuu
Mkuu ONTARIO Pole na majukumu, najua upo busy but bado nasubiri reply ya haya maswali yangu muhimu. Ahsante
 
Ontario hongera sana kwa kujikita kwenye ujasiriamali.

Najua una ventures nyingi sana, swali langu ni unamanage vipi?

Pia ningependa kujua ratiba yako kuanzia unavyoamka mpaka unavyolala... (unaamka saa ngap, mpaka muda unaolala, weekends unazitumia vipi). Huwa naamini sana mtu anavyotumia muda wake inachangia sana katika mafanikio yake.

ONTARIO
 
Kwema wakuu apa ndani nashukulu Mungu ametuweka wazima hadi saiv...nimeanza kufatili nyuzi za Jamaa apa ONTARIO tatu mfululizo sana sana ya FOREX MARKET ndoiliyo nifanya nijiunge JF na nimeanza Ku take action kwakuanza kusoma vitabu..pia nimdau mkubwa wa kilimo kwaiyo nilikuwa naomba nisaidie mwongozo wa project ya DRIP IRRIGATION nimeanza kuandika nimefika Sehem nashidwa kuendelea kuandika kutokana na sababu mbalimbali haswa nimebanwa na masomo najiandaa na UE nipo mwaka wa mwisho natushukuru sana nikipata Majibu na sample ya iyo project au vitu vinavo itajika .. mashamba nisha pata, haswa na tagemea kutumia kisima, nishajua gharama ya kisima na kampuni ya kuchimba kisima nishapta contact zao nishaongea nao maongezi ya mwanzo so shida yangu nikuwa na project plan inayo eleweka kuhusu drip irrigation ili ninavo anza mchakato wa kusaka pesa na Ku implement nijue nafanya kitu gani NATEGEMEA KUPATA MAJIBU TOKA KWAKO KAMA UTAPENDELEA MAZUNGUMZO ZAIDI NITASHUKULU NISHA KUTUMIA MP ...JUAKUWA NYUZI ZAKO ZIMENIFANYA NIJIUNGE NA JF MWANZONI NILIKUWA NAONA JF NIUPUUZI NA UWONGO SASA NIMEJUA JF KUNAWATU WAMAANA natanguliza shukrani mkuu
 
Hakuna mtu duniani atakupa feed formula hata ufanyaje boss, hapa nisikufiche. Sawa na Cocacola kutoa formula ya vinywaji vyake.

Kuku 500 hawatakiwi kula zaidi ya mifuko 26 ya kilo 50
Means kwa kuku 1000 ni kama mifuko 52, hivi bei ya chakula cha starter na finisher kwa broiler huwa zinatofautiana? And basically kuku mmoja kwa siku inabidi ale gram ngapi za chakula?
 
Mkuu Ndebile unaposema picha ni kama kielelezo unamaanisha sio picha halisi za mradi wa jamaa? Kama ndio unamaanisha hivyo mbona yeye juu amefafanua kwa uzuri kabisa kwa picha toka anaanza na mpaka alipofikia sasa au nimekuelewa vibaya?? na mkuu Chasha Poultry Farm unamaanisha kuwa mkuu ONTARIO ametuongopea unaposema picha sio za mradi wake? Mbona kuna picha kaweka hapa zipo hata kwenye interview yake? Ningeweka link ila kutoka na muhusika anaomba privacy siwezi kuiweka hapa au na wewe nimekuelewa ndivyo sivyo mkuu????
 
Asante Ontario na wadau wengine kwa hii elimu munayoitoa humu.
Nitachangia kwenye suala la ufugaji kuku ingawa mimi si mfugaji, ila mama yangu aliwahi kufuga.

Kwenye chakula; wengi wanaulizia formula ya kutengeneza chakula. Yeye alikuwa ananunua then anachanganya anachanganya humo vitu kama pumba za mahindi, mashudu, damu ya ng'ombe iliyokauka, maziwa ya unga na vitamins. Sikumbuki vipimo but kwa mfuko mmoja wa kununua alitoa mifuko mitatu, na kuku walikua wana afya nzuri anauza kuanzia wiki ya 5.5 au 6.
Ninachokumbuka wakati huo walikuwa wakina mama wengi ndio wafugaji na walishirikiana sana, hata hizo formula za kuchanganya chakula walipeana bure na kusaidiana masoko.

Kingine alikuwa anahakikisha ana batch kama 3 za kuku wa umri tofauti: say kuku wa wiki 5, wengine wana wiki 3 na hapo ashaagiza vifaranga wengine. Kwa jinsi hiyo kila baada ya wiki 2 au 3 in kuku wa kuuza.

MAsoko:Enzi hizo kulikuwa nakuna super markets so alikuwa anauzia Mahoteli, na jamaa wa masoko ya Kisutu, Kinondoni walikuwa wanakuja wanachukua kutoka bandani huhitaji hata kuwachinja. Nadhani kwa sasa mambo yamebadilika...ila hata wauza chips ni wateja wazuri au hizi pubs.

Natamani nigeweza kufuga maana ni biashara nzuri ila nilipo siwezi so nikaona ni-share kidogo ninachofahamu.
 
Habari kwa MTU yeyote mwenye interest ya kufuga kuku Nina banda tegeta masaiti nakodisha,banda na vyombo vyangu vya kuku na machine ya kunyonyoa manyoa.mwenye interest ya kufuga kuku anakaribisha kuona.whatssap 0786057996 for pics and details zaidi.
 
● Uliwafuga mkoa gani?!

●Ulifanya utafiti wa masoko kabla haujaanza kuwafuga?!

●Ukianza kuwafuga upya niombe ushauri... nitaona vipi naweza kukuunganisha na watu watakaonunua bidhaa yako.

●Ulikopitia nami nimetokaka huko huko, usipokua kune channel huezi elewa nini kinafanyika, so unaishia kua na kuku bandani lkn mteja humuoni.
Mkuu vp kuhusu soko la kuku wa kienyeji breed za hapa nyumbani na kuroiler pia huko kwenye mahotel, restaurant na bars. Mm nataka kuwasambazia huko huko walipo na usafiri ninao? Can u connect me?
 
Mkubwa jinmtu sikushauri hata kidogo kuacha kazi utaumia kuna kupata hasara kwenye ujasiriamali ukukufanya ukate tamaa kabisa ya maisha, mtoa mada ni kijana mdogo sana hana familia wala majukumu ya kumtunza mtu mwingine hata akianguka leo bado ana muda mwingi sana wa kuinuka. Jiangalie nafasi yako wewe kama wewe sometimes utakuja kugundua kwamba kuishi maisha mazuri si lazima sana uwe na pesa nyingi ajabu. Ridhika kwanza na maisha uliyo nayo then mambo yakiwa sawa tanua kwingineko lakini suala la kuacha kazi usijaribu ujasiriamali si lele mama
Nadhani inategemea sana na uelewa wa mambo wa mtu husika pia, hasa uwezo mzuri wa kufikiri, ubunifu na namna ya kukabiliana na changamoto positively.
 
Back
Top Bottom