Naomba unisamehe sana my ex girl Veronica

Naomba unisamehe sana my ex girl Veronica

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,585
Reaction score
2,666
Habari za muda huu wana Jf matumaini yangu wote muwazima wa afya.
Lengo kuu la kuanzisha huu uzi ni kutaka kumuomba msamaha girlfriend wangu wa zamani ambaye tuliachana takribani miaka 7 iliyopita. Sio kwamba nina nia ya kutaka turudiane hapana bali nimeamua kuja kutoa dukuduku langu hapa hata kama yupo humu aweze kusikia kwa sababu nahisi tukio linaniumiza kisaikolojia.

Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumamosi December 2013 mimi na mpenzi wangu Veronica hiyo siku nakumbuka tumetoka maeneo ya Bamaga Sinza tukaenda hotel moja inaitwa travertine ipo maeneo ya Magomeni Usalama. Tukawa tumeingia zetu ndani tukachukua room pale kwa ajili ya kupumzika. Mara kidogo kukatokea kaugomvi kati yetu tuligombana baada ya kukuta text kwenye simu yangu ambayo alihisi ni ya mwanamke mwingine, basi kaugomvi kakasababisha hadi akaamua kuninyima utamu yaani alininyima papuchi ilifika hatua kila nikiwa nataka kumshika sehemu basi anapiga kelele balaa hadi wahudumu wa hotel wanakuja kutugongea kwamba tunapokuwa tunafanya basi tucontrol hisia maana sauti zinasikika hadi kwa wateja wengine. Daaah yani likawa haipiti nusu saa yule mhudumu anakuja kutuambia tupunguze kelele tunaponyanduana kumbe wapi mwenzie sinyandui wala nini bali nanyimwa mgegedo.

Baada kama ya masaa matatu ya vuta nikuvute bila mafanikio yeyote basi nakumbuka ilikuwa kwenye mida ya saa 6 usiku nikaamua kuondoka zangu kule hotelini ili nikapande gari nirudi home, nikiwa natembea zangu kwa unyongeeee kwa kunyimwa mzigo ile namalizia ngazi ya mwisho chini nikasikia sauti ikiniita babumawe please maramoja nikageuka alikuwa veronica akanambia naomba unisikilize nikasimama kwa umakini nikawa namsikiliza anataka kunambia nini, basi akanisogelea kwa upole na kunambia anaomba nimlipie chakula ale kwani alikuwa na njaa na alikuwa hana hata senti tano na pia kama hela ya room sijatoa alikuwa anaomba nitoe maana yeye hana hela.

Nikamwambia tushuke chini usijali huku moyoni nikijisemea huyu si ameninyima mzigo basi tutaona leo, kwenye ile hotel kwa chini kuna huduma ya vyakula sasa tukafika tukakaa nikamwambia agiza unachotaka, akaagiza zake chipsi na kuku sekera mishikaki pamoja na juice ya matunda. Pindi anakula nikamwambia ngoja nitoe hela kwa M - PESA kwa nje kidogo, kumbe ile ilikuwa ni gia ya kuondoka zangu ili kumuacha pale. Baada ya dakika 25 alipiga sana simu lakini nilikuwa nazitazama huku nikijisemea kimoyomoyo " si unajifanya ndege mjanja sasa utajutia leo" nilizima simu na sikuona umuhimu wowote kutoka kwake maana niliona amenidhalilisha sana kwa kuninyima mzigo.

Sasa basi hadi leo hii sijajua gharama ya hotel alilipa vipi na vile vyakula alivyokuwa anakula alivilipaje.
Mwisho wa yote nimeona leo niandike hii kitu popote ulipo my ex veronica nakuomba msamaha kwa tukio nililokufanyia mie ni binadamu kama binadamu wengine sometimes tunakosea, najua unaweza ukawepo humu my beautiful ex girlfriend veronica. hivyo basi popote utakaposikia hama utakaposoma hii thread naomba unisamehe sana sio kwamba nahitaji turudiane hapana ila tu ni tukio ambalo halitokagi kwenye saikolojia yangu.

AHSANTE
 
Ulifanya kosa kubwa sana anyway hope alikusamehe next time hata ukinyimwa mzigo unatakiwa kuonyesha tofauti yako na maturity yako .
Ulitakiwa umsikilize malalamiko yake, Kama anahitaji chakula fanya kumpatia ikiwezekana kaa mpaka amalize kula, mrudishe chumbani hakikisha amekaa na karidhia.

Kisha mpe nafasi anakuwa bado amekasirika na baada ya masaa kadhaa mwamshe na zungumza nae taratibu hapo kwa lugha nyepesi ulipaisha!
 
Umenikumbuka kisa kimoja kilinitesa sana moyoni, na bado nikikumbuka naumia sana. Sijui tu kwanini nilifanya vile na kushindwa kumpa nafasi. Hakika nilimtendea ubaya na ninajua hatanisamehe milele.
Tuhabarishane kidogo, mkuuu
 
Baada ya wewe kuondoka niliingia kwenye hiyo hotel, nikakuta huyo dada analia nikamuuliza nini shida akaniambia ulivyomfanyia, me nikamlipia chakula na room then nikapiga show kali. ilikuwa kama kula tunda kimasihara
Kumbe ndo ile story uliyo shusha kwenye uzi wetu pendwa sasa hapa nimekupata hongera Sana kwa kuokoa jahazi
 
Back
Top Bottom