Kuorodheshwa kwenye wosia hakufanyi mali hizo kuwa za marehemu automatically. Vivyo hivyo, kutoorodheshwa kwenye wosia, hakufanyi mali na madeni ya marehemu kutokuwa yake. Inategemea na ushahidi uliopo. Kwa mfano, ukiandika wosia leo, halafu kesho ukanunua gari na keshokutwa ukafa....hilo gari kuna uwezekano mkubwa lisiwepo kwenye wosia wako (kama umeataja mali na madeni). Na pia wosia unaweza kuwa kwa baadhi ya mambo tu (e.g. sehemu unayotaka kuzikwa n.k lakini mali ukaachia igawanywe kwa kufuata sheria).
Kwa ufahamu wangu, msimamizi wa mirathi ni lazima awepo either kuna wosia au hakuna.
Kazi ya msimamizi kubwa na kukusanya (taarifa za) mali na madeni halali ya marehemu na pia kuwatambua warithi halali (kisheria na kwa mijibu wa wosia). Kutumia mali ya marehemu kwanza kulipa madeni ya marehemu na sehemu inayobakia (kama ipo), kuigawa kwa wanaostahili kwa kufuata wosia na sheria.
NB: Mimi sio mwanasheria.