Naomba ufafanuzi kuhusu Suala la kushika ugoni Kisheria

Stamina

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
1,029
561
Habari za majukumu ya kila siku,

Kwa wenye ujuzi wa sheria naomba kujua hili jambo, nini haki ya mwenza aliyemshika ugoni (kumfumania) mwenzawake (Mke au Mume).

Maana nimesikia kuwa ugoni sio kosa la jinai (crime) Kwa sheria za Tanzania Bara (sijui huko Zanzibar), ila linaweza kusababisha jinai! Mimi sio mjuvi sana Wa mambo ya sheria lakini mambo haya ya fumanizi (ugoni) yapo sana kwenye jamii yetu.

Sasa je, nikweli ugoni sio kosa la jinai? Ni kosa la madai au?! Na kama sio kosa la jinai, nini haki ya mwenza ambaye amemfumania mwenza wake?! Na ikitokea mwenza ameshikwa na hasira za ghafla akamshambulia mgoni wake kutokana na hasira, hapo sheria inasemaje?

Sote tunajua maumivu ya kusalitiwa, je, ikitokea umemfumania mwenzawako na mtu mwingine ndani kwako tena kitandani kwako nini haki yako kisheria? Na unapaswa kuchukua hatua zipi kisheria?!

Asanteni sana!
 
Sina hakika, ila naskia ukikuta live, hata ukitenganisha dushee na mwili, sheria itakukingia kifua
 
Back
Top Bottom