Naomba ufafanuzi kuhusu kupewa Mkuki na Ngao wakati wa Kuapishwa Marais

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Niliona kwa JK na kwa Magufuli, sijajua kwa Mh Mkapa na Mwinyi na Nyerere kama wazee wa mila waliwakatisha na kuwapa mkuki na ngao.

Naomba kujua/picha kama Mh Rais Samia Suluhu kama pia alipewa.

JPM.PNG
Kikwete.PNG
 
Havina maana yoyote.Sisi tunataka nafuu ya kiuchumi.Hatutaki mambo ya vita vita.
 
Ngao NI ishara ya kuilinda nchi kwani kazi ya ngao NI kujikknga
Mkukk n zana ya kushambiulia maadui
Hvyo Rais anakaz ya kilinda nchi anayoiongoza na kushambulia maadui watakaovamia nchi anayoiongoza
 
Mkuki na ngao ni moja kati ya alama zilizopo kwenye nembo ya taifa "coat of arms" na vina ashiria ulinzi.

Kwahiyo Raisi kupewa hiyo maana yake ni alama, kwamba atatulinda na hatari zote kama Taifa.
Ukiangalia hapo utaviona ngao na mkuki.

images (1).jpeg
 
Zana za asili za kitanzania na kiafrika kwa ujumla za kulinda himaya, ufalme, na mamlaka ni mkuki na ngao. Toka zamani jukumu la kwanza la wafalme ni kulinda falme zao na watu wao na zana kuu ndio hizo. Kwa maelezo haya machache hope umejua sababu ya marais kukabidhiwa hizo zana.
 
Kuna mtu pia wamakamo wakati tunajadili swala la rais mpya akaniuliza swali kwanini mama hakupewa ngao na mkuki? Jibu nililo mpaka ni kwamba walishakabidhiwa tangu kipindi cha mwendazake yeye akiwa ni makamu kwaiyo bado vipo ikulu na kilichofanyika ni kuhama tu kwa nafasi ila utawala ni ulele sasa sijui kwa wengine humu mngejibu nini
 
Back
Top Bottom