Haiko hivyo chief...mimi nilikuwa nafanya kazi kampuni fulani huku mkoani...sasa nilikuwa na contract ya miaka 2...after end of contract...nikaona nifatilie michango yangu..mara ya kwanza nilikuwa LAPF baadae wakaiita PSSSF...baadae tena ikapita sheria kuwa Private sector wote tuwe NSSF...so nikajiunga na NSSF...kwahiyo nikawa nimechangia sehemu mbili ambayo ni PSSF na NSSF...kimbembe kikaanza nilipoanza kudai mafao yangu...nikienda NSSF kuchukua statement inaonyesha michango haijalipwa na kampuni...na nikimpigia mwasibu wa ile kampuni anasema imeenda,siku nikajaa sumu..mguu mpaka kwa meneja wa NSSF nikamwambia scenario yote...nikashangaa ananiambia mtu anayepost hiyo michango hayupo ila michango yangu mwajiri alishaileta ..hapo ndo nilibaini NSSF kuna mambo ya rushwa..meneja akaniambia next week itakuwa posted nikaondoka...PSSF hakukuwa na shida hawa jamaa wako vizuri...wiki iliyofata nikaibuka NSSF..nikakuta michango ime reflect..nikajaza fomu za ku claim nikaenda na PSSF nikachukua statement nika attach na ile ya NSSF ili itoke pamoja ..after completion ya kila kitu wakaniambia after 30 days..itakuwa deposited kwenye account yangu...mamaweee siku thelathin zikapita hadi ikawa mwezi wa pili cheche...nikampigia simu meneja wa NSSF nashangaa ananiambia kuwa kuna taratibu wanafanya ili wanilipe..sasa nimechoka nataka niende PCCB nikachukue za moto nije niwashikishe mana ndicho wanachokitaka. Ila utaratibu wanalipa ndani ya siku thelathini sio hadi miaka 60...