Naomba ufafanuzi kuhusu hili la Bima ya afya

Ballack-13

Member
Jul 8, 2018
61
79
Wakuu habarini za jioni,

Naomba kufahamishwa uelewa kuhufu Bima ya NHIF ukishaitumia mara moja mpka ipite siku saba ndio unaweza kuitumia tena kwa matibabu hii imekaaje
 
Bima ya Afya haina kikomo kwa ugonjwa na Huduma tofauti kwa siku moja.

Na hizo siku saba nani alikwambia?

Kama ulitibiwa malaria kituo x kwa siku hiyo hiyo unaweza tibiwa UTI kwa kituo y...
 
Kwa NHIF huwezi.

1: Unaweza kufanya rufaa kwa specialities ndani au nje ya kituo.

2: Ukienda kituo cha pili bila rufaa kwa siku hiyohiyo imatakiwa iwe ni kwa emergency case na si cold case/ugonjwa wa kawaida.

Mfumo utaonyesha umetibiwa sehemu nyingine option ni ku-activate emergency na iwe emergency kweli. La sivyo, utashuhudia maumivu baadaye kwenye malipo.
 
Ndo nilichozungumzia Hapo juu sema wwe umekifafanua zaidi Ndugu Lukonge..
Kwa sababu yeye alitaja siku saba...

Binafsi nikushukuru zaidi...

Kwa kuongezea Tu ni kwamba vituo vingi tunatumia emegency case katika kupokea Mgonjwa alioKuja baada ya kutibiwa Katika vituo vingine na hakukuwa na rufaa ya matibabu (Japo ikiwa tu Dawa na Magonjwa tunayotibu hayafanani)

Nakubaliana na wewe kwamba mfumo wa NHIF kwa Tangu mwaka 2019 na kuendelea ukitibiwa hapo hapo unaonyesha kuwa umetibiwa sehemu fulani...

Hakuna maumivu yoyote kwenye malipo Yaliyowahi kutukuta Kwakuwa tunazingatia STG , No polypharmacy na Hakuna kumpa mgonjwa Dawa alizokwisha pata kituo kingine na hakuna kutibu ugonjwa uliokwisha kutibiwa unless its Complication ya ugonjwa huo...
 
Angalia maelezo yako, kuna concepts mbili:

1: kusubiri siku saba: si kweli, inatakiwa ku-activate follow-up option.

2: kutibiwa siku hiyohiyo vituo viwili tofauti: inawezekana , lakini kwa kutekeleza vigezo vifuatavyo:

A: kwa kupata rufaa
B: Emergency case
C: ugonjwa wa kawaida kama mafua haiwezekani.
 
Angalia maelezo yako, kuna concepts mbili:

1: kusubiri siku saba: si kweli

2: kutibiwa siku hiyohiyo vituo viwili tofauti: inawezekana , lakini kwa kutekeleza vigezo vifuatavyo:

A: kwa kupata rufaa
B: Emergency case
C: ugonjwa wa kawaida kama mafua haiwezekani.
Na ndo nilichoandika..
Ngoja kwanza
🤣🤣 Kwani mafua bado wanaenda hospitalini mara mbili kama ni mafua haiwezekani Maybe iwe complicated case ya flue 🤣🤣
 
Daktari mafua ya siku hizi watu wanalazwa, ingawa kwa hapa tunaongelea ya kawaida. Hayo mengine atakuja na viambata.
 
kama yakiwa Ni complicated hutakiwi kumuacha hata kama bima ikukate folio zima la matibabu cuz Umeokoa Uhai wake..
Na Umejikita katika Misingi ya Kitabibu kwahyo Utakuwa umelinda hadhi yako na Heshima yako kama Daktari japo utapunguza Hadhi na heshima kama mkusanya mapato..
Ila negligence is an offense Chief
 
Kweli suala kubwa ni kujenga hoja yake ya kwa nini asiachwe. Kwa wema na kutimiza wajibu kadri ya miongozo na sheria.

Ila wengi huwa hawazingatii hili suala. Wengi huambiwa haya mambo ya kusubiri siku saba au kuwambia waende vituo vingine tofauti na alichopata tiba mwanzo. Fikra kuu ikiwa kukwepa makato, badala ya ku-activate follow-up option.

Tatizo wapewa huduma pia hawaombi ufafanuzi pale wanapopata taarifa tofauti, ingawa mawasiliano yako nyuma ya kadi.
 
Unaweza itumia hata mara 5 kwa siku

Sio kweli.
Bima inatakiwa itumike mara moja ndani ya siku 1 kwenye hosp 1. Ikitokea unahaka hosp siku hiyo hiyo wanatakiwa wakupe namba ya rufaa ili iweze kufanya kazi hosp. Ya pili kwa siku hiyo hiyo
 
Hauruhusiwi kujipimapima ovyo ovyo maana waligundua watu wakianza kutumia wanajipimapima ovyo ovyo tu kisa wana bima,
 
Sio tuu kujipima, kulikuwa na case nyingi za udanganyifu kwa hospitali ili kujipatia fedha. Yaani bima moja inatumika mara zaidi ya 5 kwa hosp tofauti
 
wakuu namimi naomba niongeze vimaswali vyangu va aya mambo ya bima ili kupanua uelewa wa aya mambo

i. ile bima ya kizalendo km sikosei inaitwa chf, je inatumika kwenye hospitali zote na kwa magonjwa yote au ni kwa magonjwa na hospitali fulani tu?

ii. Je nikikata bima wakati ninaumwa je inakubalika nianze kutumia mara moja au adi upite muda fulani kwanza?
 
Back
Top Bottom