Asante sana Jaasusi kwa mchango wako, kwa kweli umejibu swali langu (ingawa bado kuna majibu mengi sahihi kwa swali hili). Nikikusoma vizuri, maendeleo yanatakiwa kuendeleza binadamu, na sio taasisi, Pia maendeleo ni utunzaji wa mazingira. Ila nataka kuelewa maendeleo hayo yatazalishwa na nini? sioni jibu la kuelekea upande wa nchi na uchumi...Hayo ndiyo maswali aliyokuwa anajiuliza Mwalimu Nyerere. Afrika bado ni chanzo cha mali ghafi rahisi za kuendesha Ulaya. Na hiyo hiyo Benki kuu ya dunia ndiyo iliyokuwa inamshauri Mwalimu asiwekeze kwenye elimu, ili tubaki duni, na asiwekeze kwenye afya, ili tuendelee kufa at the age of 40 na watoto wetu wakifa kabla ya kufikia umri wa miaka 5. Mwalimu alikataa. Mwinyi alipoingia akaanza kutekeleza maagizo ya World Bank, IMF matokeo yake tukatoka 85% literacy rate na kushuka kufikia 60%. Hivi leo nadhani tumeshafika asilimia 70% ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika na Kikwete anajisifia kwa shule za kata ambazo kuna mwalimu mmoja kwa wanafunzi 120. Umeuliza maendeleo ni nini. Kwa maliasili tulizo nazo ningependa kuona Tanzania tuna shule nzuri, tuna huduma nzuri za afya, tunapunguza matumizi ya mkaa wa miti kwa nishati yetu na kutumia zaidi gesi tuliyo nayo na nishati ya jua, upepo etc. Ningependa kuona Watanzania tukivaa nguo nzuri, na siyo mitumba. Sisi tunazalisha pamba. Siyo lazima tuwe kama Marekani au Ulaya. Lakini tunaweza kuinua kiwango cha maisha ya raia wetu kwa kuwawezesha kuachana na nyumba za matope na makuti na kujenga nyumba za kisasa. Kwa nchi iliyo na dhahabu na madini mengineyo sioni sababu kwa nini katika miaka 20 ijayo hatuwezi kufikia living standards za Dubai au Saudi Arabia.
Salam kwako pia Bi Roullete,RussianRoullete said:Natanguliza salam kwa members wote, hasa wazowefu wa jukwaa hili.
Leo nimeona swali langu nililete hapa ili ninufaike kwa mawazo yenu kama great thinkers.
Katika pita pita zangu nimeona picha ya world wealth distribution (usambazaji wa mali duniani) ambayo ikanipeleka kuchimba zaidi ili nijue ni kitu gani kinasababisha dhulma hii, hasa tukizingatia malighafi (raw material) ya kujenga muindombinu ulaya na north america zinatokea in 'underdeveloped world'.
Picha yenyewe hii hapa:
View attachment 39955
Utafiti wangu ukaendelea kwa kuelekea taasisi zinazohusika na maendeleo kimataifa ambazo ni International Bank for Reconstruction and Development (ikijulikana kama The world Bank, au THE Bank), na International Monetary Fund (zote pamoja zikijulikana kama Bretton Hood institutions). hawa watu wanafanya nini? na mbona reconstruction ya nchi za ulaya baada ya WWII ilienda haraka sana ila za Africa na Asia zinachelewa? Nilisoma reports zao, na methods zao nikagundua (nadhani) kosa lipo kwenye Ufafanuzi wa neno Maendeleo.
Hapa ni ngumu kutenganisha kwasababu maendeleo huletwa na infrastructures bora,yani miundo mbinu.Hizi institution zinachukulia maendeleo ya nchi kama "kuishi kama ulaya". Kwa hiyo, nchi yoyote isio na GDP kama ulaya, wasomi kama ulaya, mabarabara kama ulaya na kadhalika inaonekana kua nyuma kimaendeleo. Na hata leo, indices za kusema nchi fulani iko 'developed' au 'developing' inatumia vigezo hivyo.
Ni kweli world resources are limited.Tabu ni kwamba ressources zilizo leo duniani haziwezi kutosha ikiwa kila mtu ataamua kuishi kama watu wanavoishi ulaya, na chanzo cha vita nyingi ni kujaribu kupigania na kuwahi kudhibiti ressources hizo. Tabu ingine ni kwamba wenye kumiliki hizo institutions wanabadili vigezo mara kwa mara ili nchi fulani zibaki kua 'developed' na zingine 'developing' na category hizo ndio zinatoa nguvu katika uwanja wa kimataifa. kwa kifupi, tunaendelea kukandamizwa sababu hatuwezi kujitoa katika hali ya maendeleo duni sababu wanaosema nani kaendelea na nani hajaendelea ni wale wale.
So hapo juu,utaona kuwa bottom line ni interests za corporations ambazo ndizo zinaendesha serikali zao.I hope nimejibu baadhi ya maswali yako.If not i am more than happy to contribute more.Na kufatana na vigezo hivyo wanatoa 'misaada' (mikopo yenye very high interest) na kuzilazimisha nchi zinazofaidi mikopo mitazamo yao ya namna ya kusimamia uchumi wa nchi (kupunguza ushuru kwa biashara toka nchi zao, kupunguza ushuru kwenwye malighafi zinazoenda kwao, na kuongeza ushuru kwenye biashara zinazotengenezwa nyumbani, kupunguza mishahara ya watumishi wa umma na kadhalika)
India na china zimejitoa katika harakati za maendeleo, kama ilivyo fafanuliwa na Bretton Whods institutions, na kuleta ufafanuzi wao wenyewe, toka kwa wanainchi wao. Leo katika vigezo vya hizo institution bado wako nyuma sana ila ukweli ni kwamba nchi hizo zinaenda kuitawala dunia.
Hivi, tukijaribu kufikiria, sisi kama waafrika kuhusu swali hili, nini maana ya maendeleo kwetu? Kweli tunataka kuishi kama wazungu (destruction of social and environmental stability for the benefit of consumerism and industrialization) au tuna matarajio tofauti ?
Swali langu, wana JF, na hasa wazoefu wa jukwaa hili: Maendeleo ni nini kwetu sisi? na tunajitoaje katika hali hii?
Nawakilisha.
hawa watu wanafanya nini? na mbona reconstruction ya nchi za ulaya baada ya WWII ilienda haraka sana ila za Africa na Asia zinachelewa?
hawa watu wanafanya nini? na mbona reconstruction ya nchi za ulaya baada ya WWII ilienda haraka sana ila za Africa na Asia zinachelewa?
Umejibu maswali ila hujasema what is the way forward... tufanye nini, kama taifa, kama communities, kama individuals?Salam kwako pia Bi Roullete,
So hapo juu,utaona kuwa bottom line ni interests za corporations ambazo ndizo zinaendesha serikali zao.I hope nimejibu baadhi ya maswali yako.If not i am more than happy to contribute more.
Merci beaucoup!
So ushauri wako ni kurudi kwa Mungu? Unajua kama there are more religious people in africa than in the western countries? kama dini itatuokoa, tunafanyaje? just by going to church au tunajaribu kutengeneza development theories from the bible (and Qur'an?) tafadhali nielewesh hapo...In metaphysical narratives...................Africa inundated by official graft is both incapable and unwilling to absorb telling donor help................the capacity is not there........................and now the World is fighting the largest threat to human survival............................you may as well forget about..............African development.....................................MDGs are only a distraction but sometimes a reminder of how helpless Africa has always been..........................a captive of spirits of tradition...............we are idol worshipers........gods that can not even walk or talk like Mwenge wa uhuru.......................wasomi wetu huenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta busara.............................sasa what do you expect when you see even religious leaders are enslaved in the kingdom of darkness............this is a spiritual battle ..hence can not be fought and won by flesh and blood......................encapsulated as humanistic reasoning.......
Asante kwa kunielewesha King'asti. Shida ni kwamba tayari wanatudai. ashakum si matusi, they hold us by the balls. na sababu tunashindwa kulipa wanaleta more loan to fuel 'geowth' ambazo zinakuja na masharti magumu kutekeleza etc.RR, ina maana sie tuko hapo kwenye mkia kwa bluu, sharing 20% of the 1.4% world income. Mi nadhani it is all explained in the selfishness and greedy of pple on position. Huwa najiuliza haja ya sie kuwa na mikataba mibovu ambayo inasemekana ina nia ya kuvutia wawekezaji kwa kuwapa madini bwerere. tunatengeneza sera za ku-favor wao zaidi. why should we be desperate for their investments? na hao investor wanachukua mikopo world bank etc, why cant we as a country do the same and run the engine? wasomi wapo, na hata kama hawatoshi (kama kwenye nuclear energy and stuff) tungeweza kuajiri anybody as long as plans zipo. im afraid mental slavery is also an issue here....
Sijui kama watatuacha tufanye hivyo hao mabepari.Kuungana kutatoa nguvu zaidi.Umejibu maswali ila hujasema what is the way forward... tufanye nini, kama taifa, kama communities, kama individuals?
Asante sana JG (BB...).sasa hicho kitabu kinaitwaje na kina patikana wapi?Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja japo nmeguswa sana na wachangiaji wote!
Kusema za ukweli RR (GG lol....), jibu la msingi la swali lako ni AZIMIO LA ARUSHA.... (naomba nisipigwe mawe, maana siku hzi kijana kutaja hii kitu unaonekana kama mwendawazimu vile)
Nmefuatilia thread yako na majibu uliyoyatoa kwa Jasusi, Ben na Jmushi (heshima zenu wakuu)
nikagundua majibu yako yapo kwenye hichi kitabu nmekishika hapa, (sorry sipo kwenye position ya ku-attach hii mambo ili niweze ku-highlight vitu kidogo).
Azimio la Arusha limefafanua hyo situation inayotokea duniani saiv kuwa ni uchumi wa fedha, katika sehemu ya 3 (siasa ya kujitegemea) aya ya 2 MNYONGE HAPIGANI KWA FEDHA, kuna falsa pana sana pale imejadiliwa jinsi tunavyotafsiri na kupima maendeleo na uwekezaji kwa kuthamanisha na fedha, hivyo tutashindwa sababu hzo fedha hatuna na tutakwama kwenye mitego ya IMF na WB.
Naomba ulitafute hili azimio japo usome hyo sura tu. (achana na ujamaa???)
Azimio linajibu kiurahisi sana swali lako, way forward ni tuipange nchi yetu katika namna kuwe na hzi effective combinations 4.
1. Watu
2. Ardhi
3. Siasa safi
4. Uongozi bora.
Tunaweza kuwa na mjadala mpana zaidi katika kila element hapo, lakini ni lazima tuhusishe fikra zetu kutoka nje ya sanduku.
Ni lazima tukubali kuwa, tupo nyuma zaidi ya miaka 150 ukilinganisha na marekani na ulaya.....
Ili kupata nini hasa cha kufanya kutoka hapa (nyuma zaidi ya miaka 150) ni lazima tujue wenzetu walifanya nini kipindi hcho?
Japo najua mataifa ya ulaya na marekani yanaweza yasiwe mfano mzuri zaidi, basi twende China labda na kwa mbali India au Brazil.
RR,binfasi naamini kwetu sisi watanzania, maendeleo yatapatikana only tukiweza kuzisimamia rasilimali zetu vyema.Tukianzia hapo basi tutakuwa pia tunapambana na umasikini.Tukiweka msisitizo hapo,basi utagunduwa vigezo vyao havitakuwa na maana yeyote kama vina nia mbaya kwetu.Umejibu maswali ila hujasema what is the way forward... tufanye nini, kama taifa, kama communities, kama individuals?