Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,936
Source: Abiria 18 wateketea ajali ya basi, lori - Kitaifa - mwananchi.co.tz
Nikianza mimi mwenyewe kufanya uchambuzi:
1. sheria za barabarani: haiwezekani magari kugingana uso kwa uso kama moja halijahamia upande mwingine bila kufuata sheria za barabarani zikiwemo alama za barabarani. Picha hiyo inaonyesha ajali imetokea kwenye kona kali, na mistari ya katikati hairuhusu ku-overtake, je ni dereva wa chombo kipi cha usafiri amevunja sheria hiyo? je abiria wote hawajui sheria hiyo kiasi kwamba wamkanye dereva?
2. mara nyingi nasikia mabasi yakigongana uwaka moto, sasa sijui kama yana system kama za ndege, ila basi kuwaka moto kiasi hicho kwenye picha, je, ni kwa sababu ya mafuta? je, ni kwa sababu ya electric wiring system yake? je, lori nalo limewaka moto? je, waundaji wa hayo mabodi nchini wanazingatia vigezo vyote vya usalama juu ya electric wiring system mfano insulation na resistance level za wires? hivi ma-engineers wanaozalishwa kwenye vyuo vyetu hawajaifa?
3. sio wakati sasa kwa serikali kuchunguza kwa undani vyanzo vya ajali, mfano, kwa nini hilo basi limewaka moto, vitu gani vyaweza kusababisha moto kwenye basi, system ya umeme hiko sawa?
4. je sio sasa muda muafaka kuwa wajibisha wale polisi wa kwenye kitengo cha polisi - vehicle inspectors? je wanajua magari ndani - nje, yaani mfumo mzima wa gari na kubaini gari bomu na gari zima?
5. je madereva wote akili zao ni timamu au wengi wao ni psychopaths?
Ni heri wagome maisha kuliko kuwepo barabarani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1