Naomba tofauti ya Suzuki Swift new model vs Old Model

Naomba tofauti ya Suzuki Swift new model vs Old Model

IsaacMG

Member
Joined
Dec 6, 2019
Posts
91
Reaction score
124
Habari zenu Wana ndugu nina mpango wa kumiliki Suzuki swift ila sasa nimeshindwa kufanya chaguo sahihi kati ya hizi new model toleo la 2006/8 na zile za kawaida za zamani.

Naomba kujua kwa wenye uelewa na magari, ipi nichukue ambayo ni Bora, imara, stahimilivu na inayotumia mafuta kidogo.

Asanteni sana.
 
Unayosema ww new model ni second generation.
1280px-2010_Suzuki_Swift_(RS415)_5-door_hatchback_(2018-10-30).jpg
Swift new model ni 4th generation.
Suzuki_Swift_(2024)_hybrid_IMG_8820.jpg


Ukitaka SS nashauri tafuta SS-Sport, iyo 2nd gen ukiagiza total unapata below 15m.

Ila kabla haujafanya maamuzi, ebu fanya uangalie Honda Fit. Ni more reliable.
 
Okay, kwahiyo unaongelea hii 1st gen:
Suzuki_Swift_001_(cropped).jpeg

Against hii walioibadirisha kuanzia 2004, second gen.
1280px-2010_Suzuki_Swift_(RS415)_5-door_hatchback_(2018-10-30).jpg

Lazima 2nd gen itachukua point kwa kila sector kasoro ground clearance tu
 
  • Thanks
Reactions: I M
Ndio nndio mkuu namanisha kati ya hizo mbili ipi Bora kuliko nyingine.
 
Zote ni Bora,zote ni ngumu zote ni imara, zote engine zake ni roho ya paka.Tofauti yake ni hii.

First generation ina ufinyu wa nafasi kidogo, halafu muonekano wake ni kama wa kizamani kidogo, ila Hilo suala la kisaikolojia, halina maana yoyote.

Second generation, nayo ni imara vile vile, tena inakuja na engine tofauti tofauti na gearbox tofauti tofauti. Zipo zenye engine ya M13A, ambayo unatumika hata kwenye first generation, zipo zenye engine ya K12B, zipo zenye engine ya M15.

Engine zote hizo ni roho ya paka. Pia zipo zenye gearbox ya manual, zipo zenye gearbox ya Automatic yakawaida na zipo zenye gearbox ya CVT. Ila Mimi mashauri chagua yenye Engine ya M13A na gearbox ya manual au automatic. Sababu hizo gearbox na engine zake zimezagaa kama uyoga.

Ila kimsingi, yote ni Magari NGANGALI kabisa.
 
Back
Top Bottom