"Hatujaingiliwa".
Lkn kati ya hayo hapo juu "waizi" sio kiswahili. wingi wa mwizi ni wezi. Ingekuwa umoja ni "muizi" ndio labda wingi ingekuwa "waizi". Lkn sivyo.
"Mijizi" ni wingi wa "jizi" ni neno sahihi la kiswahili. Ni vivumishi vya sifa vya neno mwizi. Hapa ni kivumishi cha sifa mbaya au sifa ya ukubwa au kuzidi ule ukawaida wa kitu chenyewe kulingana na mtumiaji anataka aeleweke vp. Mwizi ni wa kawaida, bali jizi ni mwizi aghalabu aliyekubuhu n.k.
Mifano mingine ni kama hii:
Gombe-ng'ombe mkubwa kuliko kawaida na pengine wa saizi au sura kutisha!
Jibwa-mbwa mkubwa sana na pengine mkali sana
joka-nyoka mkubwa sana wa kutisha kuliko tuliozoea kuwaona.
Buzi-mbuzi mkubwa sana pengine kuliko kawaida.
NB. Wakati mwingine mtumiaji anaweza tu kuyatumia ili kutia chumvi kumbe kitu chenyewe cha kawaida tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.