Naomba speech ya makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba speech ya makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KakaJambazi, Apr 13, 2011.

 1. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,228
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuvuliwa gamba.

  kuna sehemu alisema "Sisi wadogo tumejiuzulu ili kukinusuru chama, ila walipaswa na viongozi wa juu wajiuzulu pia"

  Kauli hii inautata wakuu. Viongozi wake wa juu ni akina nani?
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ile hotuba kwa maoni yangu ilikuwa imejaa viloja vingi; Alianza kwa kufuru, kwa maana ya kujilinganisha na Yesu (ule usemi "mnaniona na muda mfupi hamtaniona tena kwakuwa nakwenda kuwaandalia makao," ni wa Yesu). Baadaye akatamba ya kuwa watu walitaka ahenguliwe peke yake lakini hilo lisingeliwezekana kwakuwa hakuwa akifanya kazi peke yake. Zaidi ya hapo alionyesha hisia zake zinazo ashiria kwamba haamini kuwa hatua za kumtosa yeye zitaitakasa CCM. ndiyo maana aliwatahadhalisha wale waliochukua nafasi yake kwamba na wao wataendelea kulalamikiwa.
   
Loading...