Naomba niwe mgeni wako/room mate kwa mwezi 1 hapa Dar

Oscar Amedeus

Member
Sep 21, 2015
16
1
Good afternoon brothers & sisters!
Natumaini mko poa. Hatimae nimekuwa na account yangu, now I can share stuff! Moja kwa moja kwenye swala:

Nimekuja Dar nikitokea Mwanza, ni baada ya kupata kazi kwenye makao makuu ya Benki moja hapa mjini. Baada ya kutumia fedha nyingi katika kutafuta ajira na hadi safari yangu hii, nimeishiwa salio la kupanga nyumba/chumba. Najua ofisini kuna policy ya kulipwa mshahara in advance, lakini sitaki kuclaim benefit zozote kwenye kazi hii mpya.

Naomba kwako dada/kaka/mzee unikaribishe kwako kwa siku 30 (1 month) kwaajili ya malazi tu, chakula ninajimudu, na nitakuwa willing kushare expenses za hapa na pale. Baada ya mwezi mmoja ntakuwa na uwezo wa kuhamia kwangu na tutabaki marafiki.

Kuhusu option ya kuwaomba wafanyakazi wenzangu: hilo sitajaribu kwasababu ya maslahi ya kazi. Na Dar sina mwenyeji. Kuhusu validity yangu; nina vitambulisho vyote, mkataba wa kazi na makaratasi mengine ya kunitambulisha, pia naweza kukutambulisha kwa senior wangu.

NiPM kama unaweza nisaidia au kwa maongezi zaidi.
Shukrani sana.
 
Bado nahitaji msaada ndugu zangu, bwana issa ramadhani yupo willing ila yupo mbali sana. Hivyo karibuni kwa mwenye uwezo wa kunisaidia.
 
Naweza kukusaidia kama nikijua, sio mbakaji, child molester, mchawi, mshirikina nk.
Bahati mbaya hivyo vitu haviwi proven na vyeti, au muajiri wako.

Na pia wewe huwezi jua mimi host wako kama mchawi,mshirikina au muuzaji wa viungo vya binadamu. Hivyo bora ukope tu kuliko kukaa kwa total stranger
 
Naweza kukusaidia kama nikijua, sio mbakaji, child molester, mchawi, mshirikina nk.
Bahati mbaya hivyo vitu haviwi proven na vyeti, au muajiri wako.

Na pia wewe huwezi jua mimi host wako kama mchawi,mshirikina au muuzaji wa viungo vya binadamu. Hivyo bora ukope tu kuliko kukaa kwa total stranger

Hata ndugi yako anaweza kuwa total stranger
 
Unafanyia kazi maeneo gani hapa dar tuangalie namna ya kukusaidia?
 
Humu ndani wengi ni WENYE MAGARI kuliko WENYE NYUMBA bora huyo senior wako akusaidie hukohuko
 
Back
Top Bottom