Naomba niongee na wazazi

UrbanGentleman

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
2,585
1,883
Salam sana waungwana

Nimeona niongee sababu kuna mambo wengi tunajifanya tumefumbia macho au tunajisahaulisha which is very worse katika jamii yetu na inagharimu sana hasa wale wanaojiingiza huko bila mipango thabiti.

Jana nilipita Shule ya Msingi Muhimbili nikiwa nimetokea kumuona mgonjwa wangu hapo Muhimbili Hospital, sasa kuna watoto niliwaona wananyeshewa na mvua kwenye kituo cha basi mpaka nikaumia roho ikabidi nisimame niwapakie bila kujali katika kuuliza wanaelekea wapi wakadai wanaenda Makumbusho Uzuri nilikua naeleke njia hiyo i had to escort them.

Kilichoniumiza ni jinsi walivyo innocent wadogo worse part ni darasa la 2 na 3 nikawaza ubaridi ulivyowapiga na mvua zile pale kituoni haikua sawa kabisa.

Nilienda mbali nikawaza sana hivi inakuaje watoto kama wale mvua zile mzazi asichukue hatua yeyote?

Ndugu zangu hasa wanaume wenzangu niseme tu inakuaje tunakimbilia majukumu ya kuanzisha familia alafu tunashindwa kuyatawala majukumu na yanatutawala?

Mtoto ni jini linalo nyonya damu yako unapoamua kumleta duniani jua umeleta jini kama unashindwa kumtunza means umeandaa tabaka jipya katika jamii ambalo limesababishwa nawewe kwa uzembe wako mwenyewe.

Chanzo cha watoto kua wasumbufu ni kushindwa kuwajibika kisawa sawa kama mzazi kwa nafasi yako sehemu yako hasa kama hawa unakuta mtu yuko nyumbani ansubiri mtoto arudi tena wengine wamekaa busy kwenye makochi wakiperuz jamiiforums like serious guys?

Umeamua kuanzisha familia maana ake umeamua kusimamia maamuzi yako bila kuyumbisha.

Unakuta Mwingine hakua tayari kua na family lakini mladi tu mwishowe anaishia kuja kusumbua watu.

So guys please hasa Wazazi wenzangu please na mnaotarajia kuwa wazazi kama huwezi kuhandle majukumu usiyakimbilie hayana mantiki yeyote hawa ni viumbe wa Mungu sisi ndio tuliamua kuwaita duniani hakuna alitulazimisha

Gentleman!
 
Naunga mkono hoja. ingawa life nalo linachanganya mkuu na usilaumu sana wazazi! nakupongeza at least ulitenda wema kwa kuwapa lift watoto wa Mungu na kumbuka tumepewa ridhiki kwa aina tofauti. huwezi jua among those kids, labda mmoja wao hana baba or baba alimpa ujauzito mama na kuukana..or anaye mama tu naye afanya kazi ya mama lishe ili kutafuta ridhiki na ada ya mwanae...or just an orphan...you never know!.......though, mwenye masikio na asikie..
 
kuna wengine watakuja na kusema.
asante tumeshajua unagari.
kweli wazazi wajirekebishe unakuta mtoto amebanwa kwenye daladala mpaka anakosa pumzi, hongera na endelea na moyo wa huruma hivyohivyo ndugu
 
Ishu sio wazazi kutokujua umuhimu wa usafiri kwa watoto wao,,rizki zimetofautiana jamn..Aliekupa wewe ndie kamnyima mwingine.

Swali ni kwamba,kwa nini mnapeleka watoto wakasome shule za mbali wakati shule za karibu zipo?!!! Hio muhimbili na mapambano c shule zinafanana tu?!
Kwanza unampa mtoto adha ya kuwahi sana asubuhi kuamka awahi usafiri,akagombanie daladala bado wakati akirudi shule akagombanie tena magari..!!
Mnawapa shida watoto wenu jamn.

Unakuta mtoto anaishi kimara,anasoma shule upanga au posts,school bus linapita 5:10 kimara,huyo mtoto aamke sa ngapi?!,ajiandae na shule,akawahi school bus..akirudi shule anakaa masaa mawwil kwenye foleni,akifika kimara yupo hoiiiii!!!
Msiwahangaishe hivo watoto elimu yenyewe ya primary..lol
 
They say Honest is an expensive Thing dont expect it from cheap people....thanks any way
 
Ishu sio wazazi kutokujua umuhimu wa usafiri kwa watoto wao,,rizki zimetofautiana jamn..Aliekupa wewe ndie kamnyima mwingine.

Swali ni kwamba,kwa nini mnapeleka watoto wakasome shule za mbali wakati shule za karibu zipo?!!! Hio muhimbili na mapambano c shule zinafanana tu?!
Kwanza unampa mtoto adha ya kuwahi sana asubuhi kuamka awahi usafiri,akagombanie daladala bado wakati akirudi shule akagombanie tena magari..!!
Mnawapa shida watoto wenu jamn.

Unakuta mtoto anaishi kimara,anasoma shule upanga au posts,school bus linapita 5:10 kimara,huyo mtoto aamke sa ngapi?!,ajiandae na shule,akawahi school bus..akirudi shule anakaa masaa mawwil kwenye foleni,akifika kimara yupo hoiiiii!!!
Msiwahangaishe hivo watoto elimu yenyewe ya primary..lol
Umeongea vizuri byana.... mawazo yako yafanyiwe kaz
 
Hii ni ile kasumba waliyo nayo baadhi ya wazazi kwa kupeleka watoto shule kwa kuangalia majina ya bila kujali adha ambayo mtoto anakutana nayo.

Nadhani ni muda wa wazazi kubadilika kama huna uwezo wa kupeleka mtoto shule yenye bus ni vyema kumpeleka shule iliyo karibu ili kuepusha usumbufu kwa mtoto hasa kwenye suala la usafiri.
 
Salam sana waungwana

Nimeona niongee sababu kuna mambo wengi tunajifanya tumefumbia macho au tunajisahaulisha which is very worse katika jamii yetu na inagharimu sana hasa wale wanaojiingiza huko bila mipango thabiti.

Jana nilipita Shule ya Msingi Muhimbili nikiwa nimetokea kumuona mgonjwa wangu hapo Muhimbili Hospital, sasa kuna watoto niliwaona wananyeshewa na mvua kwenye kituo cha basi mpaka nikaumia roho ikabidi nisimame niwapakie bila kujali katika kuuliza wanaelekea wapi wakadai wanaenda Makumbusho Uzuri nilikua naeleke njia hiyo i had to escort them.

Kilichoniumiza ni jinsi walivyo innocent wadogo worse part ni darasa la 2 na 3 nikawaza ubaridi ulivyowapiga na mvua zile pale kituoni haikua sawa kabisa.

Nilienda mbali nikawaza sana hivi inakuaje watoto kama wale mvua zile mzazi asichukue hatua yeyote?

Ndugu zangu hasa wanaume wenzangu niseme tu inakuaje tunakimbilia majukumu ya kuanzisha familia alafu tunashindwa kuyatawala majukumu na yanatutawala?

Mtoto ni jini linalo nyonya damu yako unapoamua kumleta duniani jua umeleta jini kama unashindwa kumtunza means umeandaa tabaka jipya katika jamii ambalo limesababishwa nawewe kwa uzembe wako mwenyewe.

Chanzo cha watoto kua wasumbufu ni kushindwa kuwajibika kisawa sawa kama mzazi kwa nafasi yako sehemu yako hasa kama hawa unakuta mtu yuko nyumbani ansubiri mtoto arudi tena wengine wamekaa busy kwenye makochi wakiperuz jamiiforums like serious guys?

Umeamua kuanzisha familia maana ake umeamua kusimamia maamuzi yako bila kuyumbisha.

Unakuta Mwingine hakua tayari kua na family lakini mladi tu mwishowe anaishia kuja kusumbua watu.

So guys please hasa Wazazi wenzangu please na mnaotarajia kuwa wazazi kama huwezi kuhandle majukumu usiyakimbilie hayana mantiki yeyote hawa ni viumbe wa Mungu sisi ndio tuliamua kuwaita duniani hakuna alitulazimisha

Gentleman!
Walio wengi wenye familia za hivi wakati wanazileta duniani huwa wanasema kila mtoto huja na sahani yake, kulea ni kazi ngumu sana kama hujiwezi ni heri usilete mtoto duniani, ni kitu cha ajabu wewe mwenyewe hujiwezi na hujui utajiweza lini alafu unataka kuzaa.
 
Hii ni ile kasumba waliyo nayo baadhi ya wazazi kwa kupeleka watoto shule kwa kuangalia majina ya bila kujali adha ambayo mtoto anakutana nayo.

Nadhani ni muda wa wazazi kubadilika kama huna uwezo wa kupeleka mtoto shule yenye bus ni vyema kumpeleka shule iliyo karibu ili kuepusha usumbufu kwa mtoto hasa kwenye suala la usafiri.
Kuna wazazi wanajisifiaga jinsi walietambea 8km to and from school walipokuwa wanasoma. Wanasahau mazingira yamebadilika na risks za barabarani ni nyingi siku hizi ukilinganisha na walipokuwa wanasoma. Hata kama shule inaprovide usafiri na ni mbali bado mtoto anateseka kuamka mapema mno na kupoteza muda mwingi barabarani.
 
Walio wengi wenye familia za hivi wakati wanazileta duniani huwa wanasema kila mtoto huja na sahani yake, kulea ni kazi ngumu sana kama hujiwezi ni heri usilete mtoto duniani, ni kitu cha ajabu wewe mwenyewe hujiwezi na hujui utajiweza lini alafu unataka kuzaa.
Rafiki yangu sana, ingawa naona nikianza kumpiga chenga na urafiki ufe. Mume wake alishafariki kitambo kidogo akamuacha na watoto watatu, hakuna mwezi hana madeni na kulialia asaidiwe. Nimeshangaa kuona tumbo linasogea tu, kuuliza naambiwa "ngoja niongeze watoto hawa ndio ndugu zangu" baba wa hiyo mimba mume wa mtu. Inawezekanaje mtu hakumbuki shida zake anapoamua kujiongezea mzigo?
 
Back
Top Bottom