Nahisi hawa wote ni wazazi wa Kambo. Pamoja na kunilea miaka yote, nimekuja kugundua ukubwani

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,353
11,492
Mimi nina Elimu ya Chuo Kikuu. Nilimaliza mwaka 2003. Nikafanya fanya kazi maeneo kadhaa nikawa naacha wakinizingua. Huwa sipendi kuzinguliwa kazini. So usitegemee utaniajiri halafu ulete za kuleta eti nikuache.

Kama sijakuwamba makofi basi naweza kukupa maneno ambayo hutasahau maishani mwako. So kuna sehemu nafanya mwezi nikiona wanaojiona maboss wanataka kunizoea nawapiga chini nalala mbele.

Sasa ni miaka mitatu sina kazi nakaa kwa mzee... Sisi tupo watoto wanne. Dada wa 2 na wakiume wawili. Mimi ni second born.

Nilirudi kukaa kwa mzee toka mwaka 2007 baada ya kuona nyumba za kupanga zinazingua. Mwenye nyumba unakuta anataka mazoea,analeta shobo hasa akiona sisi wengine mambo safi.

Basi nikawa nakaa home tu nakula nacheck movies na music ili kupunguza mawazo. Wadogo zangu wote washaondoka home na wamejenga wana maisha yao. Mimi hapo nikawaza sasa kama nami nikisema nijenge hii nyumba mzee akifa nani ataitunza. So nikaona nisihangaike na ujenzi ili mimi nitunze hii nyumba.

Sasa naona mzee na mama kama hawajielewi hivi. Naona wame change sana. Wananipigia kelele nikileta mademu hapa home. Sasa wao wanafikiri mimi nitaishije bila kushiriki tendo la mwili? Nimewaletea wajukuu watatu kila mmoja na mama yake. Ili wapate company lakini hawana shukrani.

Wameanza kama unyanyasaji fulani hivi. Mara remotes za TV na DSTV sizioni sebuleni. Mara nakuta wamechomoa nyaya za TV na Decoders. Tabia za kiswahili ambazo hawakuwa nazo.

Sasa hivi hata dada wa nyumbani hawamtumi kuja kuniita chumbani kuwa msosi tayari. Nakuta wanakula au wameshakula. Hawa kweli ni wazazi wangu?

Mzee gari zake funguo anaficha sijui anadhani mimi nitatumia usafiri gani kwenda kutafuta mishe mishe. Gari yangu nimepark sababu engine yake kubwa na yeye ameacha kunipatia pesa ya mafuta. So huwa nategemea kutumia gari ambayo atakuwa ameiacha kwa siku husika akienda kwenye ofisi yake.

Kiukweli nahisi kama kuna hujuma flani nafanyiwa. Mpaka naWaza isije ikawa hawa ni wazazi wa kambo. Maana si kwa kuninyanyasa hivi mtu mzima kama mimi.

Mpaka kufikia kunambia room kwangu nisiwe nafunga na funguo,dada wa kazi wamempiga marufuku asije kusafisha room kwangu. Yaani ni full kero na manyanyaso. Sielewi ni kwa nini wamebadilika kiasi hiki.

Haya mambo yanakwaza sana. Hasa kumfanyia mtu mzima ambaye amejitoa kupigania na kuangalia mali za familia. Wanadhani wakifa kesho nani ataangalia hizi mali ? Je nikiamua nami kususa watamlaumu nani? Haya mambo ndo maana wakati flani watoto wengine wanafanya maamuzi magumu tu.

Sitaki tufike huko. Na leo nataka niongee na mzee nimweleze jambo
 
Dah, wazazi wana hasara sana, wanakusaidia hata kisaikologia ukapambane na maisha ufanikiwe lakini wewe ni zero kabisa,

Mhitimu wa chuo mwenye upeo mfupi namna hii kweli, ni chuo gani hicho umesoma, labda vile vya kuongea kiingereza mtaani
 
Nitoke niende wapi? Nyumba hii ni kubwa wapo wao tu sasa mimi niende wapi? Mambo mengine ni ya kizamani sana. Kwani hii nyumba watakufa na kuzikwa nayo? Mimi naona kusema nikapange ni kuharibu tu pesa. Nyumba ina vyumba vya kutosha tu why nikahangaike? Si sawa
Dah! Yaani wewe jamaa huoni wanataka utoke huko ukaanze life lako. Uza gari urudi kupambana.
 
Nitoke niende wapi? Nyumba hii ni kubwa wapo wao tu sasa mimi niende wapi? Mambo mengine ni ya kizamani sana. Kwani hii nyumba watakufa na kuzikwa nayo? Mimi naona kusema nikapange ni kuharibu tu pesa. Nyumba ina vyumba vya kutosha tu why nikahangaike? Si sawa
Asee sawa mkuu.
 
Huyu anatakiwa aende kwa manabii au mitume wakamwombee.

Bomu limeweza kuja kuandika uzi JF.
 
Hi ni hadithi tu, kwa uandishi wako ulivyomzuri na weledi wako wa kupangilia maneno, sentensi na aya huwezi kuwa mtu anayezungumzwa (mwanaume mtu mzima, mwenye uelewa mdogo anayeshindwa kuchanganua/kupembua mambo, na anayegandamana kwa kuishi kwa wazazi wake) ktk hadithi hiyo.
Jamaa ni kichwa aiseee. Huyu ni mtu anaejielewa anafikisha ujumbe kwa jamii. Anataka kuona kuna wajinga wangapi watamuunga mkono
 
Back
Top Bottom