Sitaki nifike mbali leo nataka niongee na mzee nimwambie jambo

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
nimemaliza chuo mwaka 2005 . nikafanya kazi maeneo kadhaa wakinizingua naacha.

huwa sipendi kuzinguliwa kazini. kwahiyo usitegemee uniajiri alafu ulete za kuleta eti nikuache

kama sijakuwamba makofi basi naweza kukupa maneno hauwezi kunisahau maisha yako yote mpaka unadead.

so kuna sehemu nafanya kazi mwezi nikiona wanajiona maboss wanataka kunizoea nawapiga chini nalala mbele.

sasa ni miaka 8 sina kazi nipo kwa mzee sisi tupo watoto watatu. wadada wawili kidume nipo moja😁😁😁

nirirudi kukaa na mzee tokea 2014 baada ya kuona nyumba za kupanga wanazingua . mwenye nyumba anataka kuleta mazoea, analeta shoboooo...hasa akiona sisi wengine mambo buli buli yani mambo safi kama wasafi mwenyewe.

basi nikawa nakaa nyumbani tu nakula nacheck movies na music kupunguza mawazo. ndugu zangu wote washaondoka home na wamejenga wana maisha yao.

Jamani mimi hapa nikawaza sasa kama nami nikisema nijenge hii nyumba mzee akifa nani ataitunza wapwaaa...so nisiangaike kujenga ili mimi nitunze hii nyumba .

Sasa naona kama Mzee na Mama hawajielewi hivi. naona wamechange sana . wananipigia kelele nikileta mademu hapa home. Sasa wao wanafikiri nitaishije bila kushiriki tendo la mwili.

nimewaletea wajukuu watano kila moja na mama yake. ili wapate Company lakini hawana shukrani kabisaaaa

wameanza unyanyasaji fulani hivi. mara remote za TV na DSTV sizioni sebuleni. mara nakuta wamechomoa waya ya decoder .Tabia za kiswahili swahili ambazo hawakuwa nazo.

sasa hivi hawamtumi dada wa kazi chumbani kwangu kuja kuniita chakula yani msosi teyali. nakuta wanakula au wameshakula .

Eti wapwaa hivi hawa kweli ni wazazi wangu

mzee funguo ya gari yake anaficha sasa anadhani mimi nitapata wapi gari ya kwenda kuzunguka kusaka mishe mishe. Gari yangu nimeipark kwa sababu engine yake kubwa na mzee ameacha kunipa pesa ya mafuta.

kiukweli nahisi kama hujuma fulani hivi nafanyiwa isije kuwa hawa wazazi wangu wa kambo. maana si kwa kuninyanyasa hivi mtu mzima kama mimi.

Juzi mtoto wa dada kaja na begi lake katazama tazama kacartoon akasinzia ukumbini basi naambiwa eti nimemuibia daftari lake sasa Wapwaa mimi daftari la mtoto wa chekechea nikalifanyie nini

Haya mambo yananikwaza sana wapwaa. Hasa kumfanyia mtu mzima kama mimi ambaye nimejitolea kupigania na kuangalia mali za familia.

Wanadhani wakifa kesho nani ataangalia hizi mali...?

Je nikiamua nami kususa watamlaumu nani ....?

aya mambo ndo maana wakati fulani watoto wengine wanafanya maamuzi magumu tu.

SITAKI TUFIKIE UKO, LEO NATAKA NIONGEE NA MZEE NIMWAMBIE JAMBO
 
Attachments

  • 20220916_105518.jpg
    20220916_105518.jpg
    18.8 KB · Views: 11
To be sincerely honest in my humble opinion without being sentimental of course without offending anyone who thinks differently from my point of view and without hiding any thoughts in my mind and without lies,to the actual truth with my clear open mind and clean heart,expressing what ever is embedded inside me for a long time which I didn't say just because I was nervous.But Today, by gathering all the courage and motivation, I just want to say that I actually feel and think that I have absolutely nothing to say
 
,
Wewe na mtoa post, bora mtoa post
 
Unamzumgumzia nani mkuu?. Maana wewe inaonyesha zimo 100 zote sio kama huyo unaemsema hapo.
Ole wako iwe ndio wewe mwenyewe. Bora mzee akutangulize mapema au akusingizie tu kesi kubaka au hata ya kutaka kumtanguliza inatosha
 
very dangerous, but today I have to talk to my father, I don't agree with me
 
Unamzumgumzia nani mkuu?. Maana wewe inaonyesha zimo 100 zote sio kama huyo unaemsema hapo.
Ole wako iwe ndio wewe mwenyewe. Bora mzee akutangulize mapema au akusingizie tu kesi kubaka au hata ya kutaka kumtanguliza inatosha
akili ya ziada inahtajika mkuu ktk kusoma hlo andiko 😁
 
Back
Top Bottom