Naomba niongee na dada zangu future wives, fiancee, baby mamas

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
Habari dada zangu,

Kuna kitu sikielewi sana.Mfano unakutana na mtu may be anakutongoza au bado he is on process mnajuana mnakuwa marafiki anakukaribisha kwake mnapika na kupakua na kuenjoy. mnamchukuliaje?

Mfano ana ka vitz ka mkopo kajitahidi kapanga ki appartment ka 2 rooms, ili ndugu na jamaa wakitoka bush kuja mjini matibabu wasikose room yao may be ana ka dstv kidogo analipia hata bomba package ya 23,500 ili asikose TBC na sasa bitz, je mnahisi huyu mtu ana hela sana lazima mumpige mizinga?

Maana mtu mnakutana leo hamjuani, kesho una shida ya laki 3 kweli?Hamna huruma hata anavyotafuta kodi ya nyumbani kwake, msosi, mafuta ya kivitz chake na hapo hapo ujenzi wa kajumba kake Chanika huko.

Kiukweli mnatukwaza vijana sema wengi wetu tunashindwa tu kuwaambia muwe na huruma na aibu pia kuomba omba kila mwanamke unaekutana nae ana shida tu zamani nilijua wanachuo tu hata awe anafanya kazi ni yale yale tu. why this? Mtu anatafuta sababu tu anaweza kukwambia mama anaumwa nahitaji hela, mbona sisi wanaume mama zetu wakiumwa tunapambana kuwapa huduma kimya kimya.
 
alafu mida saa 12 jioni umejichokea zako utaona ki txt...baby nibebee kazawadi chips yai na nyama!

nomaaa!
 
he he he wanaume tumeumbwa matesooo. kama ni mzur mpe mpeeee mpeeee tu kwann bwana
 
Khaaaaaa nyumba, vits, dstv we mbona Tajiri kabisa unastahili mizinga, wenzio wanaishi kwao wanakula ugali wa Shkamoo na vizinga wanapigwa.
Kama hutaki vizinga tulia kwako uangalie TV, na makochi si unayo? Au hujaunua
 
kuishi ki primitive sio ujanja.. so wapi nimeonesha sifa kwenye kutongoz?? kuwa na vitz ni utajiri?? kwa dar mtu wa mishe yeyote kamkweche ni basic need au mnafikiri kila sehem kuna mwendo kasi???

Unaonesha una misifa kwenye tongoza zako kama ulivyoandika hapo ndiyo maana nao wanakukomoa...
 
tatizo humu nyumbu wengi.. hii ni fasihi tu kuonesha hali halisi wanayokutana nao vijana wengi..

so binafsi sina hata kimoja nilichoandika.. ila mizinga ya girls nilishakutana nayo sana na kijana wa kisasa ambavyo vitu kama hivyo anavyo ndio anaonekana tajiri eti na kuombwa laki 3 kiurahisi tu... je huwa mna fikiria tuna hela sana au ni nini???

wengi wanalalamika hali wanayokutana nayo ya umatonya wa girls..

so ni assumptions tu kwamba mtoto wa kike akikuona una ka vitz anafikiri una maisha mazuri sana au anakuonaje??
Kukuonaje haijalishi wala sio ishu kabisa kitendo cha kutongoza tu means umejisajiri kwenye mpambano , mzinga tu ndo unaomatter, swala la kukuona may be mdogo angu atoto anajua ila mi naona si ishu
 
hao kina dada usiwalaumu, ni MFUMO DUME ambao tangu anazaliwa kwa wazazi wake mwanamke wa nchi za mfumo dume anaambiwa hawezi!
Akili yake imefungwa kwa kuwaona wanaume wote ni kama baba zao au kaka zao wa kuomba msaada! Harithishwi ardhi katika mirathi!, lakini namshukuru MOLA kwani mambo yaabadilika kabisa... MWANAMKE ana uwezo wa hali ya juu sana!.. ukimpata mmoja ambaye anamuelekeo wa kujifunza jaribu kumwelewesha atafute pesa za kwake na ajiamini! barikiwa my friend!
 
ha ha ha wanafikiri nyumba unakaa bure??

ni bora wampige mzinga mwanaume anaeishi kwao kuliko anayejitegemea... maana anaekaa kwao hana majukumu so hela ipo...

ila anaejitegemea ni ana njaa kali na stress nyingi maana baba mwenye nyumba kodi, bado billz kibao..

hapo mshahara hautoshi... na bado mtoto wa kike unaongelea laki 3.. hajui hiyo laki 3 unanunua umeme, maji, kingamuz star time au bomba dstv kwa mwaka mzima

Khaaaaaa nyumba, vits, dstv we mbona Tajiri kabisa unastahili mizinga, wenzio wanaishi kwao wanakula ugali wa Shkamoo na vizinga wanapigwa.
Kama hutaki vizinga tulia kwako uangalie TV, na makochi si unayo? Au hujaunua
 
Mkuu nakushauri usiweke kambi kwa mtu mmoja utaumia.
Pia sio lazima kutoa pesa.
Ukiombwa pesa achana nae.
 
Back
Top Bottom