Naomba nimsahihishe Joshua Nassary (mb), mimi nitapinga vingi sana!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Joshua Nassary kamanda mwenzangu na mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki amenukuliwa akimsifu rais John Pombe Magufuli kwa hatua yake ya kukusanya mapato
ya Tshs. Trillion 1. 3 kwa mwezi huku akiongeza kuwa tutajitegemea kwa 100% kwenye bajeti yetu!

Kwanza nimueleze ndugu Nassary kuwa aliyosema bwana Mpango ni neno "Tunatarajia" na siyo tunakusanya! Bwana Mpango alisema kuwa TRA inatarajia kukusanya Tshs 1. 3 trillion kwa mwezi kama mapato! Hivyo kiuhalisia fedha hizo bado hazipo!

Baada ya Magufuli (rais) kumpongeza bwana Mpango kwa kile kinachotarajiwa na hakipo kwa sasa, niliweka akiba ya maneno! Kumbe Magufuli aliandaa uteuzi asiotaka kuulizwa na ndiyo maana akatanguliza sifa!

Aidha bwana Nassary aelewe kuwa wakati akiongeza 'kinachotarajiwa' tayari tukapoteza the same amount (1. 3 tshs trillion ) ambazo ni za uhakika kutoka bodi ya MCC kutokana na kushupaa kwa Magufuli na CCM kwa ujumla! Tutafakari kabla ya kutoa pongezi zisizo na tija!
 
1.3 Trillion is expected hasa baada ya vitisho vilivyofanywa kwa walipa kodi waliokwepa

Trend ya 900 Bn itarudi palepale kwa miezi ijayo

Utawala huu utakuwa mbovu kulko zote tangu Uhuru
 
Kwa nini uongee Maneno yao kukarisha Tamaa utawala uliopo madarakani na hapa hata miezi mitatu back mnaanza lawama au mmetumbuliwa niani maana yakikukuta lazima upige kelele hapa kazi tu
 
1.3 Trillion is expected hasa baada ya vitisho vilivyofanywa kwa walipa kodi waliokwepa

Trend ya 900 Bn itarudi palepale kwa miezi ijayo

Utawala huu utakuwa mbovu kulko zote tangu Uhuru

Lengo lako halitatimia
Pole sana
 
Ni Kamanda punguani tu atakayempongeza Magufuli mapema kiasi hiki.hizo trioli kaziona au nae anapotoshwa na ziara za kushtukiza.utampongezaje eti kwa kukusanya kodi na wakati huo hataki tuhoji,anataka kufanyia nini hizo kodi
 
Kwa nini uongee Maneno yao kukarisha Tamaa utawala uliopo madarakani na hapa hata miezi mitatu back mnaanza lawama au mmetumbuliwa niani maana yakikukuta lazima upige kelele hapa kazi tu
na kwa nini huoni ni mapema kumpongeza kama uonavyo mapema kumpongeza
 
Nassari ni mmoja wa wabunge wa chadema wanaojitambua sana. Amebadilika sana sio yule Nassari wa kupiga kelele siku hizi muda mwingi yupo jimboni anafanya kazi ya maendeleo. Ila namhurumia muda sio mrefu atatangazwa msaliti.
 
Mpango kateuliwa tarehe 27 november kuwa kamishna TRA
ilikuwa ijumaa so kama kuanza kazi alianza kazi jumatatu tarehe 30..
ilipofika december tarehe 23 akamteua kuwa waziri wa fedha
which means kama kufanya 'miujiza huko TRA'
kafanya kwa siku 24 tu including weekends......

Kwa hiyo kwa siku 24 huyu Mpango ndio alibuni
na kuleta miujiza ya kukusanya mapato mengi zaidi?
......Yaani sijui hii nchi iko namna gani
cc Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
1.3 Trillion is expected hasa baada ya vitisho vilivyofanywa kwa walipa kodi waliokwepa

Trend ya 900 Bn itarudi palepale kwa miezi ijayo

Utawala huu utakuwa mbovu kulko zote tangu Uhuru

Wewe lazima uwe jipu tu. Jiandae kutumbuliwa.
 
Wewe lazima uwe jipu tu. Jiandae kutumbuliwa.
Mpaka utakapobaini maisha yako yanazidi kuwa duni ndio utajitambuwa na kuelewa duniani umeletwa ili uwe nani, uwe mshabiki au upate maisha bora, hakuna hata jipu moja utakaloambiwa zile pesa unapewa wewe. endelea kushangilia ujinga tu.
 
Mpango kateuliwa tarehe 27 november kuwa kamishna TRA
ilikuwa ijumaa so kama kuanza kazi alianza kazi jumatatu tarehe 30..
ilipofika december tarehe 23 akamteua kuwa waziri wa fedha
which means kama kufanya 'miujiza huko TRA'
kafanya kwa siku 24 tu including weekends......

Kwa hiyo kwa siku 24 huyu Mpango ndio alibuni
na kuleta miujiza ya kukusanya mapato mengi zaidi?
......Yaani sijui hii nchi iko namna gani
cc Nyani Ngabu
Bado tu hujachoshwa na mambo ya nchi hii?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom