Naomba namba ya Waziri wa Ujenzi. Tunajenga jengo la TANESCO Geita chini ya TBA, hatujalipwa

T 2021 SSH

Member
Apr 26, 2021
20
42
Habari zunu ndg zangu,

Nimekuwa nikifanya kazi TBA mkoani Geita, hapa wanajenga jengo la TANESCO mkoa wa Geita.

Hapa tunafanya kazi kama day worker, tunalipwa kwa wiki, ila toka mwezi wa pili tumefanya kazi bila malipo yoyote(ikimbukwe tumetoka mbali tumeweka kambi hivyo tulijikuta tunaendelea tu kufanya kazi kwa kukosa nauli)

Hawataki kutulipa pesa yetu, wameamua kutuzungusha tu, tuna familia tunaendeshaje maisha miezi miwili hatuna pesa?

Tumeenda mara kadhaa ofisi ya mkuu wa mkoa Geita bila mafanikio (hatukuwa tunakutana na RC), tukaamua kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya, hapo pia hatujakutana na DC ila tulifanikiwa kukutana na DAS akatusikiliza.

Aliwapigia simu viongozi wa TBA na wakandarasi wakaja ofisini kwake akawasikiliza na akawasisitiza watulipe pesa yetu ndani ya siku mbili ilikuwa ni jumatano ya tarehe 21 ila mpaka leo kimya.

Jamani tunaomba mtusaidie namba ya Waziri wa Ujenzi au Waziri wa Kazi na Ajira(vijana) watusaidie kupata stahiki zetu kama kuna wawakilishi wa TANESCO na TBA humu msisahau kuwatagi pia waone uonevu tunaofanyiwa TBA Geita.

Ahsanteni!
 
TBA ni pasua kichwa miradi mingi wanadelay sana ukianzia ikulu ya chamwino(JPM aliwatoakabisa wakabaki kama wajenzi washauri tenda ikahamia Suma JKT moja kwa moja) Songea kule mkuu wa mkoa aliwafukuza na akasema wasiombe tena tenda mkoani humo.

TBA ni mzigo Rais Samia futa hiki kikundi cha wazembe hata TANESCO sijui waliwapaje tenda ya ujenzi wa ofisi zao mkoani Geita nasikia wanajenga na ofisi ya Tanesco Chato.
 
Mgome tu kama wale madogo wa jkt
Tumeshagoma tayari mkuu, ila ndo hivyo tunadai hatuwezi kwenda kokote mpaka tulipwe kwanza.

Hapa chakula tunateseka sana, hatuna chochote, waziri mkuu Kassim Majariwa anatuhimiza vijana wake tufanye kazi ila ndo kama hivi tunajitoa ila tunafanyiw a udhalimu.
 
TBA ni jipu kubwa sana, sijui tuna kwama wapi aise,..terminate the whole systems
Tusaidieni wakuu hapa hata chakula hatuna, mwezi wa pili huu bila chochote, wengi wetu sio wakazi wa Geita tulikuja tu sababu ya mradi
 
TBA ni pasua kichwa miradi mingi wanadelay sana ukianzia ikulu ya chamwino(JPM aliwatoakabisa wakabaki kama wajenzi washauri tenda ikahamia Suma JKT moja kwa moja) Songea kule mkuu wa mkoa aliwafukuza na akasema wasiombe tena tenda mkoani humo

TBA ni mzigo Rais Samia futa hiki kikundi cha wazembe hata TANESCO sijui waliwapaje tenda ya ujenzi wa ofisi zao mkoani Geita nasikia wanajenga na ofisi ya Tanesco Chato
Tusaidieni mkuu, tunateseka huku Geita
 
Tusaidieni mkuu, tunateseka huku Geita
Mimi ni mkazi wa hapa Geita mkuu nahisi ww utakuwa mgeni kwenye huu mradi, mradi wenyewe umeanza 2019 ilitakiwa ukamilike 2020 mwishoni TBA wamechelewesha mradi ulisimama tarehe 20 mwezi wa tano mwaka jana umekuja kuanza tena Januari mwaka huu

Kipindi kile wenzenu wamevamia sana mashamba yetu wakisaka chakula nahisi walilipwa januari hii wakapita hiviii ndo mkaja nyinyi, kiukweli watu walioanza mradi wanajua kinachoendelea pale na sidhani kama wanaweza kurudi kufanya kazi na TBA, poleni ila kuna hatari ya kukaa miezi zaidi ya sita bila malipo.
 
Mimi ni mkazi wa hapa Geita mkuu nahisi ww utakuwa mgeni kwenye huu mradi, mradi wenyewe umeanza 2019 ilitakiwa ukamilike 2020 mwishoni TBA wamechelewesha mradi ulisimama tarehe 20 mwezi wa tano mwaka jana umekuja kuanza tena Januari mwaka huu

Kipindi kile wenzenu wamevamia sana mashamba yetu wakisaka chakula nahisi walilipwa januari hii wakapita hiviii ndo mkaja nyinyi, kiukweli watu walioanza mradi wanajua kinachoendelea pale na sidhani kama wanaweza kurudi kufanya kazi na TBA, poleni ila kuna hatari ya kukaa miezi zaidi ya sita bila malipo
Kumbe tutakufa njaa jaman, maana hata mama mpishi pale site kagoma kupika nae anadai pesa alipwe, hapa tunaunga unga kupata chakula.
 
Sorry, wewe ni jinsia gani, kama ni MALE, unapoweka avatar yako kwa jinsia KE, unajidhalilisha, ndio maana unabaki unalia lia tu, jichunguze wewe kama wewe, then jiongeze.
 
Sorry, wewe ni jinsia gani, kama ni MALE, unapoweka avatar yako kwa jinsia KE, unajidhalilisha, ndio maana unabaki unalia lia tu, jichunguze wewe kama wewe, then jiongeze.
Mkuu mambo ya picha achana nayo, hapa tunataka msaada kwa haya yanayotukuta

Mbona watu wa siku hizi mmezidi kejeli, kama wewe una maisha usituzarau sisi ambao tunalialia

Kama unaweza kutusaidia tusaidie tu mkuu
 
Tumeshagoma tayari mkuu, ila ndo hivyo tunadai hatuwezi kwenda kokote mpaka tulipwe kwanza.

Hapa chakula tunateseka sana, hatuna chochote, waziri mkuu Kassim Majariwa anatuhimiza vijana wake tufanye kazi ila ndo kama hivi tunajitoa ila tunafanyiw a udhalimu.
Kama mmegoma bac inatosha sasa subirin tamko
 
Tumeshagoma tayari mkuu, ila ndo hivyo tunadai hatuwezi kwenda kokote mpaka tulipwe kwanza

Hapa chakula tunateseka sana, hatuna chochote, waziri mkuu Kassim Majariwa anatuhimiza vijana wake tufanye kazi ila ndo kama hivi tunajitoa ila tunafanyiw a udhalimu
Kama mmegoma bac inatosha sasa subirin tamko
 
Tumeshagoma tayari mkuu, ila ndo hivyo tunadai hatuwezi kwenda kokote mpaka tulipwe kwanza

Hapa chakula tunateseka sana, hatuna chochote, waziri mkuu Kassim Majariwa anatuhimiza vijana wake tufanye kazi ila ndo kama hivi tunajitoa ila tunafanyiw a udhalimu
Kama mmegoma bac inatosha sasa subirin tamko
 
Mkuu mambo ya picha achana nayo, hapa tunataka msaada kwa haya yanayotukuta

Mbona watu wa siku hizi mmezidi kejeli, kama wewe una maisha usituzarau sisi ambao tunalialia

Kama unaweza kutusaidia tusaidie tu mkuu
Wewe ni jinsia gani?........hujajibu
 
Kumbe tutakufa njaa jaman, maana hata mama mpishi pale site kagoma kupika nae anadai pesa alipwe, hapa tunaunga unga kupata chakula
Ndo nafikiria msaada mtaupata wapi maana hata jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa hapo magogo linalojengwa na Mayanga Constraction ujenzi wake ni wa speed ya kobe kila siku naona mafundi form work wamening'inia tu juu hakuna kinachoendelea leo aje awasaidie nyie wakati hata jengo lake mwenyewe limemsinda!
 
Back
Top Bottom