Naomba nafasi yoyote ofisini kwako

Naomba nafasi yoyote ofisini kwako

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
1,476
Reaction score
2,798
Habari wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 24, nipo Dar es salaam, Kurasini maeneo ya uhasibu.

Nipo hapa leo kuomba nafasi ya kazi yoyote kulingana na uzoefu wangu huu.

1. Nimefanya kazi ya stationery, nina uzoefu sana upande wa kazi za internet cafe, zile online applications za aina mbalimbali nafanya.

2. Nimefanya kazi za kutengeneza social media accounts mbalimbali kwaajili ya biashara, yaani kutengeneza Facebook accounts, sponsored ads za Facebook na Instagram, kutengeneza blogs, kutengeneza channel za YouTube.

(Kiujumla naweza fanya digital marketing)

3. Pia nina ujuzi mzuri wa computer.

4. Nimefundisha physics na mathematics kuanzia form one hadi six. (Nipo vizuri sana kwenye masomo ya mathematic)

5. Ni mbunifu hasa katika kufanya biashara na kuongeza thamani katika biashara husika.

6. Nina uwezo wa kutengeneza maudhui katika social media accounts, blogs au websites pia (nimefanya blogging pia ni msomaji mzuri wa vitabu mbalimbali)

7. Ni muandaaji mzuri wa vitini vya masomo ya physics, chemistry na mathematics (nimefanya kazi na baadhi ya wamiliki wa apps na blogs za elimu).

8. Kusimamia miradi na biashara ( nina uzoefu hasa katika kusimamia masuala ya ujenzi)

9. Kiafya niko vizuri na hata kazi za kutumia nguvu pia nafanya.

Kuna ofisi nilikuwa nafanyia kazi ila mmiliki alihama kutokana na changamoto za kifamilia December 2020, hivyo kwasasa nimeona nitafute shughuli yoyote walau kuendesha maisha wakati najipanga kuandaa ofisi yangu rasmi.

Elimu yangu nimefika chuo, ila kutokana na Changamoto za kijamii na uchumi nilisoma hadi mwaka wa tatu na sikuweza kuendelea.

Mimi ni mtu mwenye malengo katika maisha na hii kazi naomba ili kuendelea kupanua uelewa wangu zaidi na kupata uzoefu kiujumla na kuendesha maish kwa muda huu ambao najipanga ili kuanza kufanyia kazi ndoto zangu.


Pia kwa yeyote mwenye maswali, ushauri pia ntashukuru kupata mungozo.

Mungu awabariki wote mtakaoguswa katika hili.
 
Unafahamu kazi za Graphics? Mfano kutengeneza Flyers, posters, leaflets?
Mkuu upande wa graphics bado najifunza na hizo flyers, bannes logo huwa natumia simu kutengeneza. Bado sipo vizuri sana ndiyo maana sijaiweka katika list yangu hapo juu.

InDesign
Illustrator
Photoshop

Na programs zingine nipo katika hatua ya kujifunza.
 
Mkuu upande wa graphics bado najifunza na hizo flyers, bannes logo huwa natumia simu kutengeneza. Bado sipo vizuri sana ndiyo maana sijaiweka katika list yangu hapo juu.

InDesign
Illustrator
Photoshop

Na programs zingine nipo katika hatua ya kujifunza.
Sawa Mkuu. Nimekusoma vema.
 
Kigezo cha kujieleza umekitendea haki sana mkuu, naimani kama atapita mtu mwenye mahitaji au mwenye kujihusisha na hivo vitu lazima atakutilia maanani, anyway kila la kheri mkuu acha sie tuendelee kujitaftia ugali kwa nyanja tofauti na zako.
 
hio sio fan..jifunze hata kuchomelea...hapa ofisini kwangu kuna kijana kamaliza drs la tano yote anafanya mpaka graphics...
 
Ulichofanya wewe ni social media marketing ambayo ni part ya digital marketing. Digital marketing ina mambo mengi, all the best
 
Kigezo cha kujieleza umekitendea haki sana mkuu, naimani kama atapita mtu mwenye mahitaji au mwenye kujihusisha na hivo vitu lazima atakutilia maanani, anyway kila la kheri mkuu acha sie tuendelee kujitaftia ugali kwa nyanja tofauti na zako.
Shukrani sana mkuu. Bado nina matumaini boss.
 
Ukipata ulete mrejesho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usjali mkuu. Mrejesho lazima. Hata huu wakati wa mpito ukipita na nikafanikiwa kutekeleza baadhi ya malengo yangu hapa bila kupata nafasi popote pia lazima ntaleta mrejesho mkuu.

Maisha ni kujifunza na sometimes unaweza jifunza kupitia watu kama hivi.

I promise, mrejesho ntauleta, tena na ushauri ndani yake.
 
Usijali MUNGU akufungulie milango ukatimize hitaji lako
 
hio sio fan..jifunze hata kuchomelea...hapa ofisini kwangu kuna kijana kamaliza drs la tano yote anafanya mpaka graphics...
Ni kweli mkuu. Siyo fani. Ila target yangu ni kufanya shughuli zenye kuhitaji ujuzi wa computer.

Napenda masuala ya online.

1. Digital markets kiujumla (kuna vipengele bado najifunza mpka sasa kam web design hasa hizi e-commerce websites)

2. Online application za aina zote (ulimwengu unaamia mtandaoni mkuu, leo tunakata tiketi za basi on-lin)

Kiujumla nalenga shughuli za mtandaoni na mambo ya computer kwa kufanya na kufundisha pia.

Napenda na ina faida sana maana nimeshaifanya.

Kumiliki apps na website pia.

Kiujumla kwasasa natafuta backup walau nipate kazi ambayo itanisaidia kwa muda huu ambao nipo tu na mtaji wa kuanzisha ofisi yangu rasmi bado sina.


Kiufupi nina mengi sana mkuu zaidi ya hayo niliyoyaeleza.
 
Ulichofanya wewe ni social media marketing ambayo ni part ya digital marketing. Digital marketing ina mambo mengi, all the best
Ni kweli mkuu. Shukrani sana boss
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom