Naomba mwenye kupajua Ikunkwa - Kaliua Mkoa wa Tabora

Mngurimi

JF-Expert Member
May 27, 2020
819
789
Bila kupoteza muda naomba mtu mwenye uelewa na kijiji cha Ikunkwa kilichopo wilayani Kaliua huko mkoani Tabora.

Katika ufafanuzi wa mwenyeji wa eneo hilo naomba kujua fursa za kiuchumi, huduma za kijamii kama hospitali, maji na umeme.

Kama kutakuwa na sifa za ziada pia, naomba msaada huo. Barikiwa sana.
 
Ikunkwa huko ni pori hakuna Umeme kwani unataka kwenda kuwekeza kwenye asali na mbao?
Wekeza kwenye Rasilimali za Misitu. Nunua Mizinga yako ya Nyuki weka Porini utapiga pesa ya Asali. Anzisha Kiwanda kidogo cha kutengeneza Milango ya Mininga then Unaisafirisha kwenda Dodoma au Dar ambako ujenzi umepamba moto unauza bei juu. Wekeza mashine za kupasua na kuchana magogo nk. Kaliua Treni inapita kwenda Mpanda kupitia Mto Ugalla hivyo usafiri wa Mzigo ni Uhakika.
 
Nashukuru kwa msaada wako japo umeongelea Kaliua yote kwa ujumla. Ungekuwa na uelewa kuhusu Ikunkwa ningefurahi zaidi
 
Bila kupoteza muda naomba mtu mwenye uelewa na kijiji cha Ikunkwa kilichopo wilayani Kaliua huko mkoani Tabora.

Katika ufafanuzi wa mwenyeji wa eneo hilo naomba kujua fursa za kiuchumi, huduma za kijamii kama hospitali, maji na umeme.

Kama kutakuwa na sifa za ziada pia, naomba msaada huo. Barikiwa sana.
Maji ya kisima yapo kwa wingi tu na hata maji ya kununua yanapatikana pia. Kule shughuli kubwa ni kulima tumbaku, kufuga nyuki, na uchawi. Hospitali zipo ila si za maana na wakati mwingine dawa hakuna wanategemea mizizi ya porini.
 
Nashukuru
 
mkuu sorry naomba kufahamu jina Kaliua linawakilisha wilaya ndani ya tabora au ni kijiji tu.
Na kama ni kijiji kipo ndani ya wilaya gani?
Wekeza kwenye Rasilimali za Misitu. Nunua Mizinga yako ya Nyuki weka Porini utapiga pesa ya Asali. Anzisha Kiwanda kidogo cha kutengeneza Milango ya Mininga then Unaisafirisha kwenda Dodoma au Dar ambako ujenzi umepamba moto unauza bei juu. Wekeza mashine za kupasua na kuchana magogo nk. Kaliua Treni inapita kwenda Mpanda kupitia Mto Ugalla hivyo usafiri wa Mzigo ni Uhakika.
 
mkuu sorry naomba kufahamu jina Kaliua linawakilisha wilaya ndani ya tabora au ni kijiji tu.
Na kama ni kijiji kipo ndani ya wilaya gani?
Kaliua ni Wilaya katika Mkoa wa Tabora, inapakana na Wilaya za Uvinza na Mpanda za Mkoa wa Kigoma na Katavi.
 
Back
Top Bottom