Naomba muongozo kuhusu chuo cha ADEM, Bagamoyo

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
Wanajamvi habrai za jioni, poleni na Januari kwa hekaheka.

Naomba msaada kwa anayefahamu mazingira ya Bagamoyo yalivyo.

Nafikiria kwenda kujiunga na chuo cha Adem Bagamoyo kozi ya D.S.I

Ila nafikiria zaidi kukaa uraiani kupanga na siyo hostel za chuo maana ni ghali kila kitu kununua.

Nataka nijaribu kubana bajeti za maisha maana gharama za kujisomesha kuanzia tution fees kila kitu ni mfukoni kwangu.

Je, naweza kupata vyumba vya kupanga karibu na chuo na, je bajeti ya hivyo vyumba ni shilingi ngapi kwa mwezi?

Ili niandae bajeti yangu mapema kabisa kabla muhula wa kwenda chuo haujafika maana hela yenyewe ni ngumu kweli kupatikana na huku familia inakutegemea kwa kila kitu.

Asanteni ni watakie jioni njema.

Karibuni mnipe muongozo.
 
Vyumba vinapatikana kuanzia 25 had vya 60 elfu, kulingana na kipaumbele chako chumba unataka kiweje, nyumba zipo karibu na chuo

Kama unaswali lingine uliza

Sent using My phone
Samahani kwa kukuchosha kaka ...ada kwa mwaka kozi ya D.S.I wanalipa sh ngapi... Na pia nilitaka kukuuliza kiwa umesoma hapo Adem bagamoyo ili nijaribu kuuliza na vitu vya ndani kidogo

sent from toyota Allex
 
Ada sijajua ni bei gani, nimeish bagamoyo ila sijasoma adem
Samahani kwa kukuchosha kaka ...ada kwa mwaka kozi ya D.S.I wanalipa sh ngapi... Na pia nilitaka kukuuliza kiwa umesoma hapo Adem bagamoyo ili nijaribu kuuliza na vitu vya ndani kidogo

sent from toyota Allex

Sent using My phone
 
Wanajamvi habrai za jioni, poleni na Januari kwa hekaheka.

Naomba msaada kwa anayefahamu mazingira ya Bagamoyo yalivyo.

Nafikiria kwenda kujiunga na chuo cha Adem Bagamoyo kozi ya D.S.I

Ila nafikiria zaidi kukaa uraiani kupanga na siyo hostel za chuo maana ni ghali kila kitu kununua.

Nataka nijaribu kubana bajeti za maisha maana gharama za kujisomesha kuanzia tution fees kila kitu ni mfukoni kwangu.

Je, naweza kupata vyumba vya kupanga karibu na chuo na, je bajeti ya hivyo vyumba ni shilingi ngapi kwa mwezi?

Ili niandae bajeti yangu mapema kabisa kabla muhula wa kwenda chuo haujafika maana hela yenyewe ni ngumu kweli kupatikana na huku familia inakutegemea kwa kila kitu.

Asanteni ni watakie jioni njema.

Karibuni mnipe muongozo.

Kile chuo kiko mbali kdg na makazi ambayo unaweza kupanga.. so ukiamua kupanga utalazimika kuingia gharama ya usafiri kila siku na obvious itakua bodaboda
 
Back
Top Bottom