Kwa mm ninae jijua kuwa nina wivu mpaka naugua sio sawa hata kidogo.Hao waomba lift kwann wasisubirie tu hiyo lift itokee kama bahati.Binadamu wa siku hizi walivyo na tamaa sasa!!mara watake kumiliki jumla
Kwa mwanamke mwenye akili timamu, si sawa kumganda mume wa mtu kwa lift kila siku
Lazima mtaishia kitandani.
Na hata kwa wanamme, unamwombaje mdada tena mke wa mtu lift kila siku
Tena unawahi siti ya mbele nusura ubadili na gia
Akiachika, hope utamlinda.
Anyway, mtizamo wangu wa lift huwa naomba mara moja wakati kweli nahitaji, mara nyingi nakuwa na uhuru kupanda vifodi.
kama suala la lift huombwa mara moja tu na kilichobaki ni kutekeleza ... na mara nyingi linakuwa la njia moja ama kwenda ama kurudi na mara nyingi kuna muda maalumu ambao hukubalika na pande zote.. na muombaji shurti awahi na asubiri na si kusisitiza au kulazimisha
Wivu unatakiwa kuwa na mipaka...Msaada unatakiwa kuwa na mipaka pale mtu unapokuwa unaumia.
a) Mwambie asitoke nao kazini kuja nyumbani-labda kama huwa anapitia somewhere atoe excuse. Kuwapa lifti wakati wa kutoka ndio hatari zaidi, kwa sababu hawakawii kusugest wapitie somewhere kama friends halafu yakaenda kuwa mengine..
b) Kwenda nao kazini asubuhi awasaidie tu, kwa sababu hata ukiwazuia kazini watakutana na wata'interact' masaa yote ya kazi na siku zote za kazi ambapo ni muda mrefu sana ukilinganisha na huo wa kukaa kwenye gari na kwenda.
c) Nawashaurini wote kupenda siasa za mwalimu za ujamaa na kujitegemea! tuwasaidie watu na sisi tukisaidiwa sio ndo tunafanya ni wajibu- eti everyday we wapewa lifti tu!
d) Zingatia acbui : :A S thumbs_up: Jioni :A S thumbs_down:
Asubuhi watu wanakuwa wanawaza sana kazi, Jioni wamekaa kimapumziko na kistarehe zaidi....
e)Haya yote yana exceptions, kwa sababu vitu hutokea tu hata ukikaba mpaka kivuli bado haisaidii..so alow youself an occupation error, usije kufa kwa wivu bure.
Raha ya lift uipate kwa bahati yaani ukiwa hujategemea lakini hizo habari za kupeana lift kila siku hata ingekua mie kiroho kingenidunda..
Katika maisha kusaidiana ni kawaida lakini sio kila siku hiyo imekua too much sasa au walitoa mchango kidogo kwenye ununuzi wa gari??
Abiria chunga mzigo mazoea ya lift mwisho wa siku unakuja kugundua mmoja kati yao mke mwenzio,wengine wakipewa lift wanataka kupiga honi kabisa..