Hard drive inategemeana na ukubwa ziko mpaka za laki mbili na nusu.Ila nahisi ili tatizo linaweza kutatuliwa,Moja kuna weza kuwa na mdudu katika boot sector ambaye kila ukiwasha inakwenda mpaka kwenye display window xp then in shutdown then inawaka tena..kama restart.
Kwanza kama huna data za muhimu ndani unaweza format hdd...na kurudishia OS upya ila hili ni baada ya kukosa kabisa njia mbadala.
Pili unaweza chukua hiyo HDD na kuifanya kama slave hdd kwenye computer ingine unatoa data zako na kuformat.
Tata hii usifanye mwenyewe kama huna uzoefu na mambo haya..waone mafundi...wakusaidie...ili uwe kwenye safe side.
Regards
Buswelu
mi nadhani tatizo la laptop yako kuji-restart kipindi unapoiwasha sio kubwa sana kwamba hard disc yake imekufa,kuna kitu kinaitwa hard disc killer,hii inaua completely hdd yako,sasa ni kwamba usifanye uamuzi wa haraka kununua hdd, itoe hdd yako kwenye laptop then i-test kwenye desktop,ikiwa haifanyi kazi basi hapo huna ujanja,nunua tu nyingine,na ikifanya kazi basi tatizo ni OS imecorrupt,ipe format laptop na mambo yatakuwa sawa,kwa sasa nipo india,nilishangaa kidogo ulivyouliza hdd yenye 30 GB inauzwaje,labda kutokanan na mazingira,ila kwa huku hiyo laki moja ya kibongo unapata hdd yenye ukubwa wa 120GB,na ni mpya sio feki........sasa kama una mtu india jaribu kuwasiliana nae akutumie,kwani ukiweka ya 30GB naona sio satisfactory sana,anyway labda ni matumizi ya kawaida...........
Kama unatumia hdd ya ide then lazima iwe gali na kwa tanzania sasa ziko chache sana hiyo technologia ndio inaishia ishia hiyo --- kwa bei hiyo uliyotaja ya dola 89 hata hivyo ungesema hiyo hdd ina capacity gani hapo mjini dar hdd ya kuanzia 80 gb inakwenda kuanzia dola 50 hiyo ni sata so inabidi upite madukani ujue
tatizo lako inaweza kuwa mwanzo ilipatwa na virus je huyo fundi amekupa report ya computer nzima iko kwenye hali gani ? Inawezekana hata ni memory pia au kitu kingine kutegemeana na mazingira ya kuhifadhi kifaa
Si rahisi kushauri kwa mbali lakini nakubaliana na sizinga ni muhimu uhakikishe kama ametoa hdd na kuijaribisha kwenye mashine nyingine. Halafu kuwasha kompyuta yako kwa hdd tofauti. Wakati mwingine huwezi kuwa na uhakika kuhusu fundi je anajua kweli anachosema? Haitakuwa rahisi kwako kama mwenye hujui mambo lakini umwulize swali hili.
Papizo kama hujapata solution na uko bongo please ni PM nikupe mawasiliano ya mtu akufanyie kazi hiyo.Naona wengi tuko mbali nawe...pengine kusoma maelekezo ni ngumu pia tunatofautiana katika kuelewa jambo moja mpaka jingine...atakufanyia kwa free...hii ni ku kuweka privacy ya number ya mtu...