Naomba msaada wa wazo la kibiashara

Mla vitumbua

Mla vitumbua

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Messages
253
Points
250
Mla vitumbua

Mla vitumbua

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2019
253 250
Habari za asubuhi wanajamvi

Nina mshukuru Mungu kwa kunipa uhai na pia kuniwezesha kuwa mmoja wa wanajamvi. Suala la muhususi ninahitaji ushauri wa kibiashara,

Nina laki sita hapa kwenye HALOPESA yangu ambayo ninataka kufanya biashara ila mpaka sasa hivi sijajua nifanye biashara gani ambayo kwa mtaji wangu inaweza ikanisaidia kupata hata elfu moja moja kila siku kwajili ya matumizi ya familia yangu.Natanguliza shukrani wakuu
 
Hance Mtanashati

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2016
Messages
6,549
Points
2,000
Hance Mtanashati

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2016
6,549 2,000
Hiyo laki sita ndogo sana haitoshi hata kulipia frame.

Tafuta angalau milioni 5 nikupe mawazo ya biashara.
 
benny gilbert

benny gilbert

Member
Joined
Jul 4, 2018
Messages
72
Points
95
benny gilbert

benny gilbert

Member
Joined Jul 4, 2018
72 95
Habari za asubuhi wanajamvi

Nina mshukuru Mungu kwa kunipa uhai na pia kuniwezesha kuwa mmoja wa wanajamvi. Suala la muhususi ninahitaji ushauri wa kibiashara,

Nina laki sita hapa kwenye HALOPESA yangu ambayo ninataka kufanya biashara ila mpaka sasa hivi sijajua nifanye biashara gani ambayo kwa mtaji wangu inaweza ikanisaidia kupata hata elfu moja moja kila siku kwajili ya matumizi ya familia yangu.Natanguliza shukrani wakuu
Ingia playstore pakua app inaitwa "Makala za biashara" kuna biashara nyingi sana unaweza ukachagua unayoweza kufanya.
 
Mr. Purpose

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Messages
382
Points
500
Mr. Purpose

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2016
382 500
Kupata best business idea jiuliza kwanza hapo ulipo
1. Una ujuzi gani? Kitu gani waweza fanya na kikakuingizia kipato.

2. Unapendelea nini hasa wewe kama wewe ambacho upo tayari kujitoa kwa hali na mali ili kukifanya kwa ufanisi.

Kwanza ni njia gani uliyotumia mpka kupata hiyo laki sita Je, ni juhudi zako katika harakati fulanifulani au umepewa tu zote kwa pamoja bila hustling ya aina yoyote.

Kama umezipata kwa njia ya hustling jiulize Je nikiendelea kuhustle baada ya Mwezi au miezi kadhaa utakuwa na faida yoyote unayoipata na hicho kiasi kuendelea kukua??

Kama umepewa tu zote kwa pamoja, jua unahitaji akili na maarifa ya ziada katika kuikuza hiyo hela.

Kiukweli binafsi huwa napinga mtu kuulizia biashara gani nifanye pasipo yeye kuwa na mwanzo au mawazo yoyote juu ya kile anachokiwazia kukifanya.

Wengi wamezoea biashara zilezile za sikuzote ma ndiyo maana kuna mmoja hapo juu kadai laki sita ndogo hata fremu haitoshi, moja kwa moja huyu tayari unaelewa nini anachokifikiria.

Mtoa mada binafsi sina business idea ya kukupa coz business idea huwa kwanza inahitaji utashi wako kwanza kukubaliana na hali halisi ya biashara husika ila kaa jiulize unapenda kufanya nn ambacho utakuwa tayr kukifanya kwa moyo mmoja na kiukweli kwa kufanya hili utapata idea nyingi sana kama utatuliza kichwa vizuri. Tofauti na hapo utakuja ingia kwenye kundi la wajasiriamali ambao biashara za hufa miezi ya mwanzoni na kutokaa zaid ya miaka mitano.

Ideas zipo nyingi sana kama endapo unaelewa ujuzi na uwezo ulio nao.
 

Forum statistics

Threads 1,336,292
Members 512,585
Posts 32,533,664
Top