Naomba msaada wa ushauri wa kisheria

Northern empire

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
358
459
Habari za usiku. Mimi ni mtumishi katika taasisi moja na nimetumikia kwa kipindi cha miaka minne mpaka Sasa .

Changamoto inayonitokea ni kuwa huu ni mwezi wa sita sijalipwa mishahara yangu . Nimejaribu kuongea na watu wakanishauri niende mahakama ya maridhiano (sikumbuki kwa kifupi inaitwaje) ila nikiongea na waajiri wangu wao wanasema watanipa ila kwasasa hawana na hawajakataa kuwa siwadai.

Sasa wasiwasi wangu ni kuwa huko nikienda kuwashtaki itachochea wanipe haraka? au nao wanaweza kuomba wapewe muda wa kutafuta fedha ili wanilipe kitu ambacho kitachukua muda mrefu tuu mpaka kupata haki Yangu.

Naomba ushauri kama kunanjia nyingine ya kupata utatuzi Wa jambo hili.
 
Nadhani kwenda mahakamani ni hatua ya mwisho sana kwanza inabid uangalie kwa kipindi chote cha miaka mitatu na miez minne ulikua ukilipwa vizuri? Miezi sita ambayo hujalipwa tatizo ni nini? Kampuni haina hela? Au wameamua tu kutokukulipa? Wamekuachisha kazi au bado wanakuhitaji?
 
Kimsingi hapo una mkataba uwe wa mdomo au maandishi tayari ni makubaliano. Andika barua kwa uongozi kuomba kulipwa kwa siku unazodai toa nakala na subiri nafikiri kwa siku ambazo ni chini ya 90.

Wasipokujibu wapeleke idara ya kazi na baadae kotini. Huko utapata haki yako pamoja na fidia. Waajiri wengine hupenda kufanya lobbing so jipange uwe na mtu wa kukusimamia au kwenye uwezo kotini.
 
Kimsingi hapo una mkataba uwe wa mdomo au maandishi tayari ni makubaliano.
Andika barua kwa uongozi kuomba kulipwa kwa siku unazodai toa nakala na subiri nafikiri kwa siku ambazo ni chini ya 90.

Wasipokujibu wapeleke idara ya kazi na baadae kotini.Huko utapata haki yako pamoja na fidia.

Waajiri wengine hupenda kufanya lobbing so jipange uwe na mtu wa kukusimamia au kwenye uwezo kotini.
Samahani lobbing sijaielewa unamaanisha nini?
 
Mkuu I meant lobbying kutafuta uwezekano wa kukushinda kisheria ili usifanikiwe.Ama kwa kutoa rushwa au kufanya mbinu ya kupata maamuzi ya kesi ili uamuzi ukitolewa yeye akushinde.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom