Naomba msaada wa ramani na makadirio ya vifaa

Goguryeo

JF-Expert Member
May 17, 2019
2,505
4,504
Goguryeo nimeamua nisihonge tena, baada ya msoto mkali wa Ajira bila kuwapo Kwa tumaini, nimeona sasa kidogo nachokipata nianze nunua walau tofali.

Wakuu wangu naamini mnaweza nisapoti walau nipate ramani Kwa wale wakongwe mlowahi Jenga nyumba kama hii mnisaidie mdogo wenu.

Nyumba ya sifa hizi
Sebule kiasi Tu
Dining
Jiko
1 master room
2 single room
1 single room (store)

Goguryeo nimeanza na bati 3 nimewekeza kwenye Duka la vifaa vya ujenzi. Plan yangu ni kuweka bati 3 kila mwezi za chap ya kiboko.

Shida yangu ni ramani (vipimo ambavyo plan yangu ni vyumba vya kawaida Tu, ) vipimo na idadi ya material kama bati, tofali, nondo nk...

Sihitaji GHARAMA za material maana nitaogopa na mwishowe nikaenda kuchukua hela yangu ya bati 3 nikaghairi bure.

Nitashkuru sana.🙏
 
Kiasi gani chief nikutafutie nione kama nikazitoe zile bati nikipate ama la
 
Safi kumbe wapambanaji ni wengi ....mtusapoti wakongwe msije sema vijana tunawaza kuhonga t.
 
FB_IMG_16673773089052905.jpg
 
wakuu ,nimepata haka karamani nikaomba mwamba anikadirie vifaa ....
Kaniambia tofali elfu 4300 .......nimehisi kichwa kuwaka moto aisee....

Naomba mnishauri hapo wakuu
 
maana kama tofali tu milioni 6 ambayo hata kuishika sijawahi Bora nighairi tu kujenga ....Nile Bata tu sasa 🤣🙌
 
wakuu ,nimepata haka karamani nikaomba mwamba anikadirie vifaa ....
Kaniambia tofali elfu 4300 .......nimehisi kichwa kuwaka moto aisee....

Naomba mnishauri hapo wakuu
Nyumba ni ya kawaida ila complicated! Nyumba ina vikorido vingi, so lazima tofali ziende nyingi. Vyumba nadhani ni vikubwa.... mfn. sitting room ya 5.00M.
 
Nyumba ni ya kawaida ila complicated! Nyumba ina vikorido vingi, so lazima tofali ziende nyingi. Vyumba nadhani ni vikubwa.... mfn. sitting room ya 5.00M.
Chief msaada wako .......vyumba nataka viwe tu standard ya kawaida vipungue maana japo sijui ni taaluma za watu ila nimehisi tu hii shughuli sio ya kitoto 😃🙌

mimi Wala sitaki mambo makubwa ..nataka vyumba standard tu vya kawaida .....Ili walau nitumie tofali kati ya 3200-3500 tu.
Msaada wako chief
 
Chief msaada wako .......vyumba nataka viwe tu standard ya kawaida vipungue maana japo sijui ni taaluma za watu ila nimehisi tu hii shughuli sio ya kitoto

mimi Wala sitaki mambo makubwa ..nataka vyumba standard tu vya kawaida .....Ili walau nitumie tofali kati ya 3200-3500 tu.
Msaada wako chief
Ramani ya vyumba vitatu iliyochorwa vizuri huwa inachukua tofali kati ya 3200 mpaka 3500, hii inategemea na factors kama kina cha msingi, idadi ya madirisha & milango, urefu wa boma n.k
Ramani ninazo ndugu, karibu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom