Naomba msaada wa kisheria wa kuwakataa TUCTA

Naomba msaada wa kisheria wa kuwakataa TUCTA

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,045
Reaction score
1,503
WanaJF, salaam!

Kutokana na historia ya watumishi na wafanyakazi nchini kupitia katika nyakati mbalimbali za mateso yasiyozungumzika kwa baadhi ya waajiriwa huku TUCTA ikishuhudia bila kuchukuwa hatua naomba mwenye uelewa mzuri anifahamishe njia za Kisheria niwezazo kuchukuwa ili kuwakataa viongozi wa TUCTA. Sababu zinazonisukuma kuwakataa ni hizi hapa:-

(i). Imekuwa kawaida wanasiasa kupanda majukwaa na kuwawajibisha baadhi ya watumishi bila kuzingatia sheria na kanuni za kiutumishi (kuwekwa Cell, Kutukananwa, Kufukuzwa) nk lkn wakati haya yakitokea chama kinachojiita TUCTA kiko kimyaa as if kinaongoza watumishi na wafanyakazi wenye raha tele!!!

(ii). Imekuwa kawaida waajiri kutumia vitisho - kwenye baadhi ya sekta lkn TUCTA imelala usingizi!!!

(iii). Kumekuwepo na sheria kandamizi kwenye utumishi (Sheria ya Fao la Kujitoa, Sheria ya Pension kwa wastaafu 25%) lakini badala ya TUCTA kupaza sauti mapema wanaonekana nyuma ya baadhi ya wanasiasa - kwa mtindo huu kwa nini TUCTA muendelee kuwa viongozi!!!

Kwa ufupi sana najuwa wakati mwingine baadhi ya watu wachache wanamchonganisha Mhe. Dkt. Magufuli kwa watumishi kupitia mahuisho ya Sheria mbalimbali - na sehemu walipomchonganisha na watumishi ni hili suala la pension ya uzeeni (watumishi) hawawezi kuielewa Serikali.

Yote kwa yote, nipeni ushauri wa jinsi ya kuiwajibisha TUCTA kwa kukaa kimya pindi mambo yasiyopendeza na yanayokiuka mkataba wa ajira yanapovuma na kushamiri

Nawasilisha kwa maoni na ushauri wenu
 
Back
Top Bottom