Naomba msaada wa kimawazo wa kumsaidia mdogo wangu

Mrs minel

Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
74
Reaction score
86
Habari zenu wakuu,

Nina mdogo wangu alihitimu Form 6 mwaka 2017 na kupata division two na kuchaguliwa kwenda UDSM kusomea BED akaripoti kama mwezi hivi zikatokea nafasi za kwenda JKT akaacha chuo na kwenda huko na bahati mbaya zaidi hakuhairisha masomo kisheria aliondoka tu kienyeji.

Sasa wiki hii katupigia simu kua wanajiandaa kurudishwa mwezi wa 12 kwani mkataba wao JKT umeisha na hawakufanikiwa kupata ajira ndani ya hiyo miaka 3.

Kiukweli imetuumiza sana ila ndio hamna namna, so nilikua naombeni mawazo yenu wadau nianzie wapi jinsi ya kumsaidia mwenye wazo lolote aniambie tu. Na hata mwenye uwezo wa kumsaidia hata kiajira cha kijishikiza usisite kumsaidia.

Na je, nauliza km mtu aliacha chuo kienyeji anaweza ku-apply tena na akapata?

Asanteni
 
Alikosea kuondoka kienyeji chuo si mbaya kuanza upya arudi chuo umri unamruhusu hakuna namna
 
Pamoja na kwamba sina ushauri kwa hili, lakini ngoja niseme hivi.....
Binafsi nimekua nikiwaambia watoto wangu mara kadhaa kwamba, hata uwe na akili kama malaikia then ukakosa adabu/nidhamu, wewe ni sawa na takataka.
Alicho kifanya huyo mdogo wako ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa kuacha chuo kienyeji. Na nadhani alijaribu kufanya shortcut ili kufikia mafanikio chap, na leo sasa imemgharimu yeye na inawaumiza hadi familia yake.
 
Sasa hapa umetoa ushauri au utopolo?
 
Sasa hapa umetoa ushauri au utopolo?
Mungu alituumba kila mmoja na uwezo ama utashi wake kwenye kila jambo.
Na sio kila panapo ombwa ushauri, basi wote lazima tushauri. Lakini pia kuto kushauri haukumaanishi basi marufuku ya kuchangia hoja.
Na kwakumakizia, nikukumbushe tu kwamba kabla ya kuchangia hoja, nilitoa angalizo.
 
Mimi nimekuelewa, tatizo kila anae sema ukweli daima hapendeki, anachukiwa. So sad!
 
Sasa hapa umetoa ushauri au utopolo?
Hiyo sio vita au siasa zenu,,, uncle katoa into zuri,, huenda dogo akaaply chuo then akawa mwaka wa 3 katikat ajira ikamuhitaji kwa ujuaji wake ataacha masomo akimbilie ajira baadae kuja kugundua ndani ya ajira hana cheti cha ujuzi au kazi kwishey ilikuwa ni ya tempo huoni ni ujinga?

Kila kitu Fanya kwa wakati wake usidandie tren kwa mbele.

Ndio alichosistiza huyo mkuu kuwa na nidhamu la sivo tutapata viongozi wapumbavu hapo baadae wenye tamaa tamaa.
 
Mungu alituumba kila mmoja na uwezo ama utashi wake kwenye kila jambo.
Na sio kila panapo ombwa ushauri, basi wote lazima tushauri. Lakini pia kuto kushauri haukumaanishi basi marufuku ya kuchangia hoja.
Na kwakumakizia, nikukumbushe tu kwamba kabla ya kuchangia hoja, nilitoa angalizo.
Msamehe maadam na yeye akili zake zipo km za mtoa mada
 
Habari zenu wakuu,

Nina mdogo wangu alihitimu Form 6 mwaka 2017 na kupata division two na kuchaguliwa kwenda UDSM kusomea BED akaripoti kama mwezi hivi zikatokea nafasi za kwenda JKT akaacha chuo na kwenda huko na bahati mbaya zaidi hakuhairisha masomo kisheria aliondoka tu kienyeji.

Sasa wiki hii katupigia simu kua wanajiandaa kurudishwa mwezi wa 12 kwani mkataba wao JKT umeisha na hawakufanikiwa kupata ajira ndani ya hiyo miaka 3.

Kiukweli imetuumiza sana ila ndio hamna namna, so nilikua naombeni mawazo yenu wadau nianzie wapi jinsi ya kumsaidia mwenye wazo lolote aniambie tu. Na hata mwenye uwezo wa kumsaidia hata kiajira cha kijishikiza usisite kumsaidia.

Na je, nauliza km mtu aliacha chuo kienyeji anaweza ku-apply tena na akapata?

Asanteni
Katika Maisha na hata kwa Mwenyezi Mungu huwa hakuna Neno Kuchelewa au Kuwahi hivyo yaliyotokea kwa huyo Mdogo wako chukulia kama Changamoto za Kimaisha na wala zisikuumize au Kukuvunja Moyo. Kuhusu Kuendelea na Masomo ya Chuo Kikuu si lazima sana akasome Chuo hicho hicho japo hata akisema aombe tena nafasi hapo pamoja na kwamba aliacha Kienyeji bado ana nafasi kama ukipangilia vyema Hoja zako.

Kuhusu Ajira nadhani kwakuwa ana Mafunzo hayo ya JKT nashauri atafute Kazi katika Makampuni ya Ulinzi au akubali Kujitolea mahala fulani ili apate uzoefu zaidi, ajenge Imani na Wahusika ambapo bidii na ufanisi wake waweza kuwa Kichocheo kizuri kwa Yeye Kuajiriwa moja kwa moja. Hata hivyo tatizo la Ajira ( Kazi ) ni la Kidunia japo kwa hapa Kwetu Tanzania limekuwa kutokana na Sera mbaya ya Elimu na Mifumo dhaifu.
 
Kwanza hongereni na kuwa na moyo wa kumsaidia mdogo wenu ni wachache ndugu wanasaidiana.

Pili hajakosea kuacha kusoma BAED kwani angesoma angerudi nyumbani kuja kuwachanganya akili zaidi.

Tatu Huko JKT amejifunza mengi kuhusu maisha sasa ni muda arudi nyumbani aangalie upya moyo wake unataka asomee mambo gani au ajiajiri vipi maana huko kaona fursa nyingi pia za kujiajiri.
Kila lakheri akiomba chuo na mkopo atapata mwakani mwezi wa saba.
 
Mungu alituumba kila mmoja na uwezo ama utashi wake kwenye kila jambo.
Na sio kila panapo ombwa ushauri, basi wote lazima tushauri. Lakini pia kuto kushauri haukumaanishi basi marufuku ya kuchangia hoja.
Na kwakumakizia, nikukumbushe tu kwamba kabla ya kuchangia hoja, nilitoa angalizo.
Huyo insane achana nae
 
Habari zenu wakuu,

Nina mdogo wangu alihitimu Form 6 mwaka 2017 na kupata division two na kuchaguliwa kwenda UDSM kusomea BED akaripoti kama mwezi hivi zikatokea nafasi za kwenda JKT akaacha chuo na kwenda huko na bahati mbaya zaidi hakuhairisha masomo kisheria aliondoka tu kienyeji.

Sasa wiki hii katupigia simu kua wanajiandaa kurudishwa mwezi wa 12 kwani mkataba wao JKT umeisha na hawakufanikiwa kupata ajira ndani ya hiyo miaka 3.

Kiukweli imetuumiza sana ila ndio hamna namna, so nilikua naombeni mawazo yenu wadau nianzie wapi jinsi ya kumsaidia mwenye wazo lolote aniambie tu. Na hata mwenye uwezo wa kumsaidia hata kiajira cha kijishikiza usisite kumsaidia.

Na je, nauliza km mtu aliacha chuo kienyeji anaweza ku-apply tena na akapata?

Asanteni
aki apply atapata. lakini nashauri asisome BED aangalie kozi nyingine itakayomfaa. vyuo vya kuapply ni TIA CBE UDSM Mzumbe, Uhasibu - Arusha hivi vyuo ada zao sio kubwa

mfano wa kozi ni:-
procurement
Human resource
accounts
Law
 
Naiondoa Law kwenye list. Ni Tumaini na Mzumbe pekee wanatoa ya miaka mitatu. Vyuo vingine Law ni miaka minne, ongeza na miwili sijui mmoja wa Law School.
Zingatia form six katoka mwaka 2017.

Na hiyo Law sio ugali kila mtu aweze. Kuna kada unatakiwa usome ukiwa na kipaji sio uvamie. Mtu aliyeacha chuo kimagendo hunishawishi kama anaweza faa kwa Law.
 
Umeongea fact mkuu.....koz ya law inataka mtu fresh from school
 
Back
Top Bottom