Naomba msaada na ushauri wa kisheria

Banzi

Member
May 25, 2011
30
9
Scenario:
Case No 1. (Madai ya nyongeza-Mshahara)

Situation:
Mimi kama kiongozi wa idara pia (Makamu mkuu wa idara), nilipokea malalamiko ya vijana kuhusu kuongezewa mishahara, hii issue ilianza na mkuu wa idara lakini hakuwa amelipa uzito na kulisimamia kuwa madai utaratibu uedelee kufuatwa (Salary council itafanya kazi kulingana na sera ya kampuni).

Vijana hawakuwa wameridhishwa na majibu ya mkuu wa idara na badala yake hili jambo lilipelekwa kwa Mkurugenzi mkuu kwa njia ya barua (Barua ipo) ilikupata kauli yake rasmi na msimamo wa ofisi.

Mkurugenzi baada ya kuipata barua yetu, yalifanyika mambo yafuatayo:
- Kuagiza idara ya utumishi kufanya usaili wa wafanyakazi wapya kwenye idara yangu (Hearsay) ingawa ushahidi ni tangazo lililotolewa mara baada ya barua yetu kupokelewa, kupitia media za online).

- Baada ya wiki moja vijana waliomba majibu kupitia mimi, kwa kuonana na mkurugenzi nay eye kuahidi kuwa majibu atayatoa kwa kuwa ameshatoa maelekezo kwa idara ya HR kulifnyia kazi.

Mkurugenzi baadae aliamua kukaa na wafanyazi kulizungumzia jambo hilo na akatoa ufafauzi kwanini hawezi kuongeza mishahara ulioomba na wafanyakazi wa idara yangu (Minutes ya kikao ipo).

Case No 2.
Mikataba: (My case)

Mimi nimeajiriwa na kampuni sasa mwaka wa 5, Mkataba wangu wa kwanza ullikuwa wa mwaka 1, uliisha Feb 2016, Mkataba wa pili nilio sign ulikuwa wa miaka 3 ulioisha Feb 2019, baada ya hapo sikuwa nmimepewa mkataba mwingine wowote.

Mikataba: (Other Case)
Kulikuwa na vijana watatu (3) ambao kwa mujibu wa idara ya kazi (HR) mikataba wake unapaswa kuwa inakwisha January hii 2020 na unpaswa kuhuishwa (Renewal).

Utaratibu wa ndani ni kwamba mfanyakazi anapo maliza muda wa mkataba wake anapaswa kufanyiwa tathmini na msimamizi ya kazi ( kwa muktadha huo ni mimi kupitia taarifa ya miezi 12 ya utendaji wake.

Baada ya hilo kufanyika ni kupelekwa kwa mkuu wa idara kwa ajili ya uthibitishi (Approval), yote haya yalifanyika hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni mkataba mpya wa ajira.

Bahati mbaya taarifa nilizo nazo ni kwamba kati ya vijana watatu (3) ambao tumewafanyia tathmini, mmoja inadaiwa hatapewa mkataba na sababu hakuna za msingi zaidi ya hakuna (renewal).

Ushauri:
Kwa kesi yangu- Ambaye sikuwa na mkataba tangu mkataba wa miaka 3 ulipoisha mwaka 2019 February, position yangu ipoje?

Kwa kijana huyu ambae mkataba wake ulikuwa umeisha kweli, lakini tathmini yake imethibitisha anapaswa kupewa mkataba lakini sasa taarifa ni kwamba hatapewa (non renewal) position yake ipoje.

Asante nasubiri ushauri wako mkuu.
 
Mkuu kutokana na sheria za mikataba, ili kuwe na agreement lazima offer iwe made na kwa case 2 ni kuwa hujapewa offer hivyo ni sawa na kusema wewe ni mfanyakazi hewa, ushauri wangu ni kuwa kwa sababu unafanya kazi kwa mikataba na hujapewa ni vyema ukaangalia other options kwa sababu Kampuni is in favor kisheria, kwa sababu wao ndio watoa mikataba yaani offer.

Kwa huyo kijana pia ambae tathmini inamruhusu kupewa mkataba mwingine lakini wamekataa,muna two options kama kwenye mkataba wake uliomalizika hakukuwa na term inayoweza kumbeba kidogo katika negotiations basi hana jinsi hapo ila kama mkataba wake uliopita kuna vipengele ambavyo vinamfavor then anaweza kuitisha na kuanzisha negotiations kwa sababu kashafikia malengo aliyowekewa na kampuni.

Katika mkataba au contract mtoa mkataba ndie ana upper hand kwa sababu hawezi kuweka vipengele vitakavyomfunga yeye, pili Kampuni zinazoajiri kimkataba pale ambapo mkataba unamalizika basi huwa ndipo mnapoishia working relationship yenu, kama wakikuhitaji watakupa new contract lakini wasipokuhitaji wao hata kama wewe unaona umefikia malengo hawatakupa contract. Lastly ni kuwa as long as Kampuni hajaviloate mkataba wenu yaani employer na employee mwanzo wa mkataba mpaka mwisho then employee can not sue for anything.

Don't hunt what you can't kill.
 
Mkuu kwani sheria za kazi zinasemaje juu ya unfair termination?
Je katika mazingira hayo,je hudhani kuna haja ya kuzua aina ya mkataba wenyewe ni ipi?
1. Fixed term Contract-Ina maanisha nini kwenye masuala la mikataba ya ajira
2. Automatic renewal inatokea wakati gani?

Maswali mengine ya kujiuliza katika hili ni je.
1. Ni katika mazingira gani mwajiri anaweza kufanya kazi na mfanyakazi ambae hajampa mkataba lakini akawa bado anamlipa (Hoja ya mfanyakazi hewa inatokea wapi)
2. Kwanini mfumo wote wa ndani ambao unahusika kwa sehemu kubwa kuwa kigezo cha mfanyakazi kupewa mkataba mwingine ni perfomance evaluation na recommendation imefanyika kwamba asipewe mkataba bila sababu nyingine iliyo wazi? Hudhani maamuzi ya Management yanatokana na suala la kudai mishahara? ambayo inaweza kufanya kuwe na unfair termination?
Hebu tuendelee kupeana elimu kupitia hili.
 
upo kazini maana mkataba ukiisha kama hujapewa mwingine unatakiwa uwe ulipewa Notice ili wakufukuze immediately mkataba ulipoish,Kwa maana hiyo wewe mkataba wako uliihuishwa automatically ila sijui kwa muda gani,
 
Hata mimi najua hivyo. Hebu tuone Wataalamu wa sheria ya mambo ya ajira wanasemaje kuhusu hizi scenerio tpate picha na kujifunza zaidi.
 
Scenario:
Case No 1. (Madai ya nyongeza-Mshahara)

Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 15 (1) h kinaeleza wazi mkataba wowote wa kazi unatakiwa kuonesha kiwango cha malipo yani mshahara sasa basi kwa kutumia tena Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 13 kinaelezea swala la upangaji wa mishahara na hili linajibiwa na minimum wage oder 2013 yani ni agizo la serikali kuhusu kima cha chini cha mshahara katika kila sekta sasa hapa kosa litakuwepo endapo tu kama kiwango wanacholipa kipo chini na amri ya serikali ya kima cha chini cha mishahara

Muajiri atajitetea hivi kampuni hailipi kiwango cha chini ya mshara kwa nujibu wa order ya serikali ya mwaka 2013 hivyo hawataweza kuongeza kutokana na gharma za uendeshaji kuwa juu na hapa muwe makini kunakuwaga na technical retrenchment kuwakomoa wale wa mbele mbele

jua kwanza kiwango cha chini cha mshara wa sekta yako husika je kinalipwa chini ya hapo hii ndo hoja ya msingi je aongze au ni haki kwa mujibu wa sheria

Case No 2.
Mikataba: (My case)

Mimi nimeajiriwa na kampuni sasa mwaka wa 5, Mkataba wangu wa kwanza ullikuwa wa mwaka 1, uliisha Feb 2016, Mkataba wa pili nilio sign ulikuwa wa miaka 3 ulioisha Feb 2019, baada ya hapo sikuwa nmimepewa mkataba mwingine wowote.

kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 kifungu cha 4 (2) ikiwa mkataba wa muda maalumu mkataba utakoma wenyewe muda ukiisha kama icho kipengele kimeanishwa kwenye mkataba kama njia ya ukomo wa mkataba huo mkataba ulipofika feb 2019 pande zote mbili zilikaa kimya maana yake wewe ulikuwa unamatarajio ya kuendelea na kweli ukaendelea maana yake ni automatic renew of the contract sasa kuendelea kufanya kazi baada ya mkataba wa muda maalumu kuisha ilo sio kosa na upo safe maana walitakiwa kutoa taarifa kabla ya mkataba ule wa miaka 3 kuisha

Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004, kifungu cha 41 (1) iii ilitakiwa itoke notes siku 28 kabla walivyoshindwa kufanya hivyo tunahesabu hivi mkataba ulitakiwa kuisha feb 2022 hivyo wakitaka kufanya mutual agreement settlement of dispute basi walipe fidia ya idadi ya miezi iliyobaki kwa kuwa ulikuwa na expectation of the renew of the contract na kweli ndo kilichotokea

Case no 3
na yenyewe ni hivyo hivyo bado ni makosa rejea maelezo ya kesi ya 2
 
Hon, salaam.
Nipe wazo la kisheria.
Nimesafirisha korosho kutoka mtwara to Dar es salaam, kampuni ya usafirishaji wametosa gari kwenye Maji baadhi ya korosho zikaharibika. nimechukuwa zilizosalimika, tumepiga jumla ya hasara courier alikubali kulipa.
Amenibabaisha mwezi mzima ndio akalipa nimshitaki kwa kosa gani sababu hapo naamini kanikosea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom