Naomba msaada kuhusu kazi ya Proccesor katika Computer

chuxxe

Senior Member
Feb 4, 2019
158
195
Habari wanaJF,

Nitangulize shukrani kwenu wana JamiiForums nimekuwa muuliza mkubwa kidogo coz nahitaji ufahamu

Nilikuwa nahitaji kujuzwa ufanyaji wa kazi wa "Proccesor" katika "Computer" haswa kujua hizi Core

Je, husaidia nini katika "Computer Performance". Au Quality ya Graphics

Naomba msaada please
 

sjosh4

JF-Expert Member
Apr 10, 2020
906
1,000
Processor ndio engine kwenye computer
Core i ni matoleo yake, eg core i3, i5, i7 currently kuna i9
Kuna generation mfano unakuta i7-47..

Then hiyo 4 inamaana ya core i7 kizazi cha 4,ikiwa 5 kizazi cha tano mpaka cha tisa
Na kuna cores, hii kama ni engine ya gari, basi hizi tunaweza fananisha na cylinder. No of cores per processor kuna single, dual, quad na octa core

Mimi sio mzuri kudadavua vizuri, kama ujaelewa watakuwa wengine kudadavua zaidi
 

chuxxe

Senior Member
Feb 4, 2019
158
195
Processor ndio engine kwenye computer
Core i ni matoleo yake, eg core i3, i5, i7 currently kuna i9
Kuna generation mfano unakuta i7-47.. Then hiyo 4 inamaana ya core i7 kizazi cha 4,ikiwa 5 kizazi cha tano mpaka cha tisa
Na kuna cores, hii kama ni engine ya gari, basi hizi tunaweza fananisha na cylinder. No of cores per processor kuna single, dual, quad na octa core
Mimi sio mzuri kudadavua vizuri, kama ujaelewa watakuwa wengine kudadavua zaidi
kuna kitu bado cjaelewa mkuu hapo kazi kubwa ya izi processor upande wa generation naelewa Ila hapa kwenye ufanyaji wa kazi wa izi core
 

Chief-Mkwawa

Platinum Member
May 25, 2011
23,811
2,000
Nitangulize shukran kwenu wana jf nimekuwa muuliza mkubwa kidogo coz nahitaji ufahamu
Nilikuwa nahitaji kujuzwa ufanyaji wa kazi wa proccesor katika computer haswa kujua hizi core je! husaidia nini katika computer parfomance. Au quality ya graphics msaada pliz!
hii ni definition toka wikipedia
processor is the electronic circuitry within a computer that executes instructions that make up a computer program. The CPU performs basic arithmetic, logic, controlling, and input/output (I/O) operations specified by the instructions in the program

kwenye hio definition kifupi processor yenyewe kazi yake ni kuhakikisha maelekezo yote ya program yanafuatwa, kuanzia kutoa data zako kwenye hard disk, kuzipeleka kwenye ram, zisomwe, kama kuna mahesabu yafanyike, mfano unacheza game na umebonyeza x kwenye pad pale una ingiza kitu processor itasoma input yako na kuifanyia kazi then itakupa matokeo yake, kama ilikuwa ni pasi kwenye game la mpira na umeipiga vizuri majibu yatakuja kwa kuona pasi imemfikia mlengwa.

kuhusu msaada wa core kwenye perfomance.
kwenye processor kuna nguvu za aina mbili kwenye core
1. single core/thread perfomance
2. multi core/thread perfomance

kutokana na program ilivyotengenezwa kuna program zina uwezo wa kutumia core moja tu na nyengine zina uwezo wa kutumia core nyingi, nitakupa mifano
-video editing programs, server programs na hata software kubwa za super computers zina uwezo wa kutumia core zaidi ya moja hivyo ukiwa na processor yenye core nyingi zaidi inakuwa vizuri zaidi na unapata perfomance kubwa
-tech za games kama open gl, tech za web browser kama javascript zenyewe zinatumia core moja zaidi hivyo ukiwa na core yenye nguvu sana zitafanya kazi vizuri kuliko core nyingi zisizo na nguvu.

ndio maana mara nyingi kwenye machine ambazo zinamlenga mtumiaji wa kawaida zinakuwa na core chache 2 mpaka 8 mara nyingi, ila kwenye machine za proffesional, servers, super computers na workstation mbalimbali unakuta zina core nyingi mpaka 64 kwa cpu moja.

unaweza angalia hii video

kuhusu core kusaidia kwenye graphics, indirectly cpu inaweza kuifanya gpu ikawa slow, ila cpu haiongezi nguvu ya graphics, kama gpu yako ipo slow hata utumie cpu kali graphics zitakuwa ndogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom